ni Muhimu kukumbuka Mungu aliyokutendea nyuma usipokumbuka yataleta madhara mbeleni
Uasi ni mbaya sana Mungu hapendi uasi na hapendi watu ambao hawashiki maagizo yake na pia hapendi watu wasio na Imani. Tunapata fundisho kubwa sana kwenye kitabu Cha Hesabu sura ya 14 baada ya wapelelezi 12 kurudi na wapelelezi 10 kuleta habari mbaya na wawili tu ndiyo walikuwa na taarifa nzuri na za kiimani na kutambua uweza wa Mungu. Maneno wa wale 10 yalisababisha Wana wa Israel kulalamika na kimunung'unikia Mungu na kusahau mambo mengi aliyo watendea wakiwa Misiri na jangwani. Na walikuwa watumie mwaka mmoja na nusu kuweza kufika nchi ya ahadi. Tazama hapo chini Tangu Wana wa Israeli walipotoka *Misri* hadi siku *Musa alipotuma wapelelezi* kupeleleza nchi ya Kanaani, *ilikuwa imepita takriban mwaka 1 na miezi 2 (miezi 14)*. *Ufafanuzi wa kihistoria na kibiblia:* 1. *Kutoka Misri:* - Walitoka Misri mwaka wa kwanza, mwezi wa kwanza, siku ya 15 (Kutoka 12:2, 12:37-41). 2. *Kuja Sinai na Agano:* - Walifika Mlima Sinai mwezi wa 3 baada ya kutoka (Kutoka 19...