MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMBAYE BAADHI YA WATU HUDHANI KWAMBA NI YESU.
Brian Deacon akiigiza kama Yesu ndani ya filamu ya JESUS. Hii ni historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, filamu hii imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu. hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU. Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS'' Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon, ndoa yake ya pili...