Uasi ni mbaya sana Mungu hapendi uasi na hapendi watu ambao hawashiki maagizo yake na pia hapendi watu wasio na Imani. Tunapata fundisho kubwa sana kwenye kitabu Cha Hesabu sura ya 14 baada ya wapelelezi 12 kurudi na wapelelezi 10 kuleta habari mbaya na wawili tu ndiyo walikuwa na taarifa nzuri na za kiimani na kutambua uweza wa Mungu. Maneno wa wale 10 yalisababisha Wana wa Israel kulalamika na kimunung'unikia Mungu na kusahau mambo mengi aliyo watendea wakiwa Misiri na jangwani. Na walikuwa watumie mwaka mmoja na nusu kuweza kufika nchi ya ahadi.
Tazama hapo chini
Tangu Wana wa Israeli walipotoka *Misri* hadi siku *Musa alipotuma wapelelezi* kupeleleza nchi ya Kanaani, *ilikuwa imepita takriban mwaka 1 na miezi 2 (miezi 14)*.
*Ufafanuzi wa kihistoria na kibiblia:*
1. *Kutoka Misri:*
- Walitoka Misri mwaka wa kwanza, mwezi wa kwanza, siku ya 15 (Kutoka 12:2, 12:37-41).
2. *Kuja Sinai na Agano:*
- Walifika Mlima Sinai mwezi wa 3 baada ya kutoka (Kutoka 19:1).
- Walikaa hapo muda mrefu (kupokea Torati, kujenga maskani ya kukutania n.k.).
3. *Kuondoka Sinai:*
- Kulingana na *Hesabu 10:11-12*, waliondoka Sinai *mwaka wa pili, mwezi wa pili, siku ya 20*.
4. *Kutuma Wapelelezi:*
- *Hesabu 13:1-3* – Baada ya safari fupi toka Sinai, Musa aliwatuma wapelelezi 12.
- Hii ilikuwa bado *mwaka wa pili* wa kutoka Misri.
*Hitimisho:*
Tangu Kutoka Misri hadi kutumwa kwa wapelelezi, *ilikuwa imepita mwaka 1 na miezi kadhaa (si zaidi ya miwili)*.
Kwa kifupi: *Takriban miezi 14*.
Sura ya 13 na 14 kwenye kitabu Cha Hesabu tunaona tatizo la Manunguniko na kusahau Yale Mungu aliyofanya hapa zilibali siku 40 tu wafike inch ya ahadi lakini kutokana na walichifanya Wana wa Israel siku 40 zilizidishwa kuwa miaka 40 na Mungu alifanya hivyo ili wale ambao hawakuwa na Imani wafe jangwani na kiingie kizazi kipya kwenye inch ya ahadi
Hivyo ni vyema kumwamini Mungu hata kama Kwa Sasa hajafanya hebu kumbuka yake aliyokutendea nyuma ili ikusaidie kujua Bado Mungu ni yule yule anae tenda miujiza na anaweza kufanya tena
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni