Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Horatio Gates Spafford 1828 - 1888.

PATA HISTORIA YA UTUNZI WA WIMBO NI SALAMA ROHONI MWANGU. When Peace Like a River. Tenzi 23.

Picha
  Mtunga Liriki/Maneno: Horatio Gates Spafford 1828 - 1888. Mtunga Vokali/Sauti: Philip Paul Bliss 9 Julai 1838 – 29 Desemba 1876 Mwandishi wa wimbo huu Horatio Gates Spafford alizaliwa yapata mwaka 1828 na kutwaliwa mwaka wa 1888 akiwa ameishi duniani kwa miaka ipatayo 60 tu. Mtunzi wa vokali/sauti/tuni anaitwa Philip Paul Bliss ambaye aliishi kwa miaka 38 tu hadi anatwaliwa Mbinguni. Wimbo huu hata hivyo kwa jinsi ya upako wake, umepewa sauti tofauti tofauti na zote zikiwa zina mguso ule ule zinapoimbwa. Mtunzi wa wimbo Mtumishi wa MUNGU Horatio Spafford, alikuwa mwanasheria na alikuwa tajiri sana. Aliishi na kufanya biashara zake huko Chicago Marekani. Alikuwa na familia ya watoto watano, mabinti wanne na mvulana mmoja. Pia alikuwa ni mkristo na mwanafunzi mzuri wa maandiko matakatifu. Katikati ya mafanikio yake, Horatio alimpoteza kijana wake mwaka 1870 aliyefariki kwa ugonjwa uitwao kwa lugha ya kiingereza scarlet fever unaosababishwa na bakteria. Akiwa bado ...

Follow Adonai Media