Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Assemblies of God

UZINDUZI WA BWENI JIPYA LA WANAUME KATIKA CHUO CHA TAG DODOMA.

Picha
Idara ya Elimu ya kanisa la Tanzania Assemblies of God linatekeleza mpango wa maboresho wa vyuo vyake vya Biblia nchi nzima. Mwezi Januari Mwaka 2016, jengo jipya lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi wanaume zaidi ya 200 katika chuo cha Biblia cha Central Bible College (CBC) Dodoma lilizinduliwa katika hafla iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa Tanzania Assemblies of God Rev. Dr. Barnabas Mtokambali. Mradi huu umefadhiliwa kwa ubia baina ya "Priority One"kutoka Marekani na Idara ya Elimu ya TAG. Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Dr. Sam Johnson kutoka Marekani ambaye pia ndiye mfadhili mkuu wa mradi huo alisema mradi huo ni utekelezaji wa Agizo Kuu la Bwana Yesu la kuwafanya mataifa yote kuwa wanafunzi wa Yesu. Dr. Johnson alisema chuo cha CBC kitawavutia watumishi wengi kuja kunolewa na kupata elimu ya theolojia ili waje kuwa watumishi wazuri zaidi, kwa kupata Stashahada, Shahada, na Shahada za Uzamili na Uzamivu. Aliongeza kwamba anaamini kwamba CBC itakuwa kitovu cha...

Follow Adonai Media