TUNAJIFUNZA NINI CHAGUZI ZA NDANI YA VYAMA?
Nichue nafasi hii kuwapongeza Mh Peace Lumelezi na Mh Charles Mkama kwa kuthubutu kugombea nafasi za ubunge kwa sisi tuliokoka ni changamoto kubwa wakati Mch D Kanemba akiwapongeza katika ibada ya j2 alisema mimi nawahesabu kuwa ni washindi hamjashindwa na aliongeza kuwa watu tuliookoka ambao ni waaminifu tumejisahau sana na kusababisha nafasi nyingi za uongozi kuchukuliwa na watoto wa mama mdogo. Kweli mimepata kitu hapa. Uchaguzi wa awali ambao umefanyika kwenye vyama ukichunguza wengi wao ni watoto wa mama mdogo hata wewe jaribu kuuliza watu ni watu wangapi waliokoka wenye kadi za vyama vya siasa do ni wachache sana kama ni hivyo ni ndoto kupata viongozi waminifu waliokoka. Je maombi ya kufunga na kuomba tu yanaweza kutupa viongozi wazuri !!! au je hivi kweli wote tuliopo makanisani tunataka kuwa wachungaji na wainjiristi? hasha nitoe changamoto kuwa tuamuke sasa tuwe na kadi za vyama siasa ili na sisi tuweze kupigia kura watu waaminifu nitoe mfano ulitokea tabora samahani kwa kuta...