Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Jennifer Mgendi. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo Jennifer Mgendi. Onyesha machapisho yote

Jumanne, 23 Juni 2015

JENNIFER MGENDI KUZINDUA ALBAMU YAKE YA WEMA NI AKIBA JUMAPIL HII

Mwimbaji wa muda mrefu Jennifer Mgendi anatarajia kufanaya uzinduzi wa albamu ya wema ni akiba. Jennifer amesema pamoja na uzinduzi huo pia atakuwa akimshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 20 akifanya huduma hii ya uimbaji 1995 -2015. yeye ni kati ya waimbaji wachache wa kike ambao wameanza uimbaji siku nyingi, pamoja na kuimba amekuwa akiandaa na filamu za kikristo, Albamu ya kwanza alitoa mwaka 1995 na mpaka sasa kuna alnbamu zisizopungua 8 ambazo alishatoa mpaka sasa na pia movie yake ya kwanza alitoa mwaka 2004 na hadi sasa ameshatoa movie 4, kwa sasa yeye anaishi kwa kufanya kazi ya Mungu kwa kuimba na kuandaa movie.

ennifer alizaliwa  tarehe 02 May, 1972 hospitali ya Ocean Road, Dar es Salaam, mama yake akiwa Mwendapelu Nalaila na baba akiwa Fanuel Mgendi. anao ndugu watatu tuliozaliwa kwa baba ambao ni Mao Mgendi, Mlenge Mgendi na Noel Mgendi. alipata pata elimu yake katika shule na vyuo mbalimbali kama shule ya msingi Mgulani,Shule ya sekondari Kisutu,Chuo cha Ualimu Korogwe, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia alifanya kazi katika taasisi mbalimbali zikiwemo Shule ya Sekondari Handeni, Shule ya Sekondari Tanbaza, Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Chuo Kikuu cha afya Muhimbili. Kuanzia 2007 aliacha kazi za kuajiriwa na kujiajiri katika kazi za sanaa ya kumtukuza Mungu.

Pia jennifer alisema Mwaka 2012 alitoa albam ya DHAHABU ambayo ni mkusanyiko wa nyimbo pendwa zilizochaguliwa kutoka katika albam zake tatu za mwanzo yaani kutoka albam ya Nini, Ukarimu Wake na Nikiona Fahari. Albamu hii inanyimbo kumi na mbili. Sababu ya kutoa album hii ni kuziboresha nyimbo kwani kipindi cha nyuma hasa albam ya Nini na Ukarimu Wake wakati zinarekodiwa teknolojia ilikuwa chini kwa hiyo hata Cd hazikuwapo wakati huo kwa hiyo nyimbo zimerekodiwa upya ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia. Uzinduzi unafanyika jumapili hii 28/06/2015 saa 8 mchana  uzinduzi huo mgeni rasmi atakuwa ni Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dr Barnabas Mtokambali na uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa kanisa la DCT uliopo Tabata shule na hakuna kiingilio chochote na watu wote mnakaribishwa. 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Jumatatu, 30 Machi 2015

HIVI NDIVYO UZINDUZI WA DVD YA MCH MARRY KANEMBA ULIVYOKUWA KATIKA PICHA.

Siku ya jana kulikuwa na uzinduzi wa dvd ya Mch Marry Kanemba sambamba na uzinduzi huo pia kulikwa na uchangiaji wa ujenzi wa chuo cha mziki wa injili kitakachojengwa kwa gharama ya shi 250 milioni. maneno ya Mch Kiongozi Dunstan Kanemba >>>>>
NI KWA NEEMA YA BWANA YESU.
UZINDUZI ULIFANIKWA MBINGU ILIKUWA PAMOJA NASI.
TUMEMUONA BWANA. Asante kwa wote waliotushika mkono.
Jengo lenu la Kanisa halikutosha kubeba watu waliohudhulia tamasha la Mch Mary Kanemba. Kulikuwa na kwaya 80 na zaidi, waimbaji binafsi 60 na zaidi, wachungaji, wawakilishi wa makanisa na viongozi (maaskofu) 40 na zaidi. UWEPO WA JEHOVA ULITUFUNIKA KWA UTUKUFU WA JINA LA YESU KRISTO.
Katasha hilo lililokuwa na waimbaji wengi na mahudhulio makubwa ya idadi ya watu baadhi ya waimbaji waliokuwepo ni Christ boys walikuwepo, Jenifa na Bahati Bukuku walikuwepo, Kiza blessing alikuwepo, Nayothi prophetic singers walikuwepo, Victory singers walikuwepo, Boko basihaya walikuwepo, Living water kawe walikuwepo, AIC kwaya walikuwepo, Next level CCC Upanga walikuwepo, EAGT Temeke walikuwepo, Lutheran Magomeni mviringo walikuwepo, Kawe TAG, Mbezi Juu TAG, Baptist Magomeni walikuwepo, External Mabibo TAG walikuwepo na nyinginezo nyingi..
The blogger Mch Marry Kanemba Mch Mwita na my wife
Mc the blogger Sam Sasali na mgeni Rasmi
Mc sam na Mwita katikati ni Mch harris Kapiga.


The christ Boyz band nao walikuwepo kutoka kushoto ni Michael Mzima, Andrew Didier, Joel Sasali, Nehemiah Chilonhani, Aloyce Didier, Octavian, Ema Heri, Martin Malecela, Sam Sasali.


Bahati Bukuku on the stage
Praise team ya basihaya.
Mwimbaji mkongwe Jennifer Mgendi



na maadimin wa magroup nao hawakuwa nyuma katika kazi yao

Mwimbaji mtoto Rehema Peter hakuwa nyumba




uzinduzi wenyewe








kama kawaida mc ni razima awavunje watu mbavu.

Mgeni rasmi anaongea


Mch Marry kanemba akiimba



meza kuu




meza kuu
Mgeni rasmi na rafiki yake
Mkurugenzi wa section ya Magomeni Mch Mahagara

Ofisi ya Mch Magomeni na wageni. Mch Kanemba akiwakaribisha wageni,
madhari
Mgeni Rasmi akiweka sahihi katika kitabu cha wageni


Mch Sasali nae alikuwepo
Watu wako makini




KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com