UJIO WA WIMBO MPYA WA ROSE MHANDO, JIWE CHINI YA SONY MUSIC
Msanii maarufu namba moja wa Africa Mashariki wa nyimbo za injili amefyatua kibao cha pili kingine kilichotengenezwa katika studio za Sony Music Africa, ambapo kibao cha kwanza kiliitwa Wololo kilichobeba albam ya Yesu Kung’uta chini ya usimamizi wa Rock star 4000 na kupatikana rasmi kupitia kampuni ya Mkito.com Wimbo wa jiwe umetengenezwa na kuchezwa na Rose Muhando ambapo kupangiliwa na kuzalishwa na Yusuph Mayige katika Studio ya Sony Music Afrika na kuendelezwa na kuongezewa vionjo na Rockstar 4000. " Rose Muhando asema wimbo huu unatambulisha kuwa naniataendelea kuitawala hii dunia na kila kilichomo ndani yake, katika dunia hii ya sasa , tunapoteza uaminifu nakumsahau Mungu katika kutawala kila kitu. Ni miminatakiwa kuweka muda wa kumkumbuka na kumsifuyeye kwa nj...