TAMASHA LA PASAKA HIVI NDIVYO KEKE ALIVYOTOKELEZEA
Tamasha la Muziki wa Injili la Pasaka limefanyika katika Mkoa wa Dar-es-Salaam na maelfu ya Watanzania walijitokeza kushuhudia wanamuziki wa Injili kutoka nchi mbalimbali kama Tanzania, Kenya, UK, Zambia na Afrika Ya Kusini. Tamasha la Pasaka ambalo huandaliwa na Msama Promotion hufanyika kila wakati wa Pasaka na Christmas hapa nchini ili kutoa fursa kwa Wakristo kutoka madhehebu mbalimbali.kuweza kukusanyika kwa pamoja na kumtukuza Mungu wao. Katika Siku ya jana Mgeni rasmi wa Tamasha hilo alikuwa Mhe. Bernard Membe aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa sasa yupo nje Kikazi. Baadhi ya Wanamuizi wa injili waliohudumu ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Keke Kutoka South Africa. Malkia wa Muziki wa injili Rose Muhando alipanda Jukwaani Saa 2 Usiku ili kuwahudumia watu. Mhe. Benard Membe akisikiliza risala kutoka kwa Mchungaji Mwasota ambaye ni Mwenyeki...