Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Maadili yameshuka?

TUNAWAPA WATOTO WETU MAFUNDISHO BORA?

Picha
Tanzania bado ina mambo mengi ambayo bado hayajakaa sawa na wala bado hayatazamwi kwa upana au mtazamo endelevu ukilinganisha na mataifa mengine yaliyoendelea na yanayoendelea, na wakati mwingine tunatilia mkazo mambo ambayo kwa mtazamo wa mbali hayatusaidii lolote. Jambo ambalo ni la mhimu na hayatiliwi ni elimu ya malezi ya watoto. Tunaposema kuwa watoto ni taifa la kesho inatakiwa tumaanishe kweli kweli na tuweke msingi wa hilo taifa la kesho. Nitoe mfano wa inchi ya China watu hawa wajua nini maana ya Taifa la kesho na ndio maana watumia gharama kubwa kuwafundisha watoto kwa habari ya uzalendo, uchapa kazi na ukakamavu na ndio maana wanafanya kazi kama mchwa na inawaletea maendeleo makubwa katika nchi yao. Lakini hapa kwetu sivyo ilivyo jukumu la malezi ya watoto wapo kwa wazazi tu na kwa mtazamo wangu ninamini kuwa sio wazazi wote wana uwezo wa kuwafundisha watoto maadili mazuri na je watoto yatima watafundishwa na nani? Nafikiri kuna haja ya elimu kufundishwa kwa watu wote hasa w...

Follow Adonai Media