Machapisho

Inaonyesha machapisho yenye lebo ya Rebecca Malope

TAMSHA LA PASAKA MWANZA. ZIKIWEMO NA PICHA ZA REBECCA MALOPE AKIIMBA.

Picha
Hatimae tamasha la pasaka limefanyika kule Mwanza na huku malkia wa gospel Africa Rebecca Malope akikoga nyoyo za wakazi wa Mwanza, tamasha hilo liliandaliwa na msama promotion na huwa linafanyika kila mwaka msimu wa pasaka.  Rebecca Malope kutoka Afrika kusini akifanya kweli kwenye Tamsha la Pasaka Mwanza.    Rebecca Malope akifanya kweli    Mh William Ngereja akiwa amenyanyua albam mbili za muimbaji Grace Mwikwabe baada ya kuzizindua,kulia ni Alex Msama mkurugenzi wa Msama Promotion.  Kushoto ni HK 1 Hadson Kamoga,Alex Msama,John Lisu,The voice,na Mess Jacob.  Upendo Kirahilo kama kawa akifanya kweli mdau wangu.  Mama wa Lisema...Sara K kutoka Kenya akifanya vitu vyake mbele ya mashabiki.   Picha zote na Full Shangwe... KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembele...

MASHABIKI WAMHITAJI MALOPE TAMASHA LA PASAKA 2014

Picha
  JINA la Rebecca Malope si geni masikioni na machoni mwa wengi, hasa kwa wapenzi, mashabiki na wadau wa muziki wa Injili. Rebecca aliyezaliwa mwaka 1968, yu miongoni mwa waimbaji wa kimataifa wa muziki wa Injili kutoka nchini Afrika Kusini, aliyewahi kuja nchini mara moja kwa mwaliko wa Kampuni ya Msama Promotions kupamba Tamasha la Pasaka. Kupitia tamasha hilo ambalo lilifanyika jijini Dar es Salaam Aprili 8, Rebecca akishirikiana na wengine mahiri wa ndani na nje ya Tanzania , walikuwa baraka katika tamasha hilo lililofanyika mara ya kwanza Uwanja wa Taifa mbele ya mgeni rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Umahiri wa Rebecca katika uimbaji na uchangamfu jukwaani, umewafanya wadau wengi watamani awe miongoni mwa waimbaji katika Tamasha la Pasaka la mwaka huu Aprili 20, jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia katika mikoa itakayopata kura nyingi za wadau. Shauku ya kumtaka...

Follow Adonai Media