FAHAMU UNDANI WA VITA KATI YA ISRAEL NA PALESTINA KIBIBLIA. ISRAEL ALIPEWA YAKOBO NA SI YAKUB. MPENDWA ENDELEA KUIOMBEA ISRAEL
Na Douglas Majwala K atika makala hii ya mafundisho ninawaletea hoja ngumu nzito zenye kuhitaji tafakuri, utulivu na umakini wa kutosha kuelewa mgogoro huu mkongwe duniani wenye mwanzo lakini unaonekana hauna mwisho, lakini wenye asili yake katika Agano la Kimbingu. Mimi binafsi nimelazimika kufanya maombi kabla ya kuanza kuandaa makala hii ya mafundisho; jambo ambalo ni nadra katika uandishi. Nikusihi na wewe mpenzi msomaji sasa utwae shajala zako [stationery] kama kalamu na note book au daftari lako na Biblia yako pia unapoanza kusoma mafundisho haya ambayo wengi wanayaonea aibu au hawana ujasiri wa kuyafunua wazi kwa umma ijapo wanafahamu ukweli wake katika maandiko, labda kwa kuogopa gharama za mahusiano na upande wa pili wa imani. Lakini ajabu ni kwamba licha ya Biblia kuwa wazi kuhusu nani ni mmiliki halali wa maeneo husika hasa Yerusalemu lakini ni mara chache sana au hakuna kabisa maandiko haya kufundishwa au kuhubiriwa madhabahuni. Mimi mwen...