KUSUDI lililo FICHIKA
“ 5Na tazama, Sauli akaja akifuata ng’ombe kutoka kondeni; naye Sauli akauliza, Watu hawa wana nini, hata wakalia? Wakamwambia maneno ya watu wale wa Yabeshi ” (1 Samweli 11:5). Kila mtu amezaliwa na KUSUDI tayari, ila HATMA yako ni wajibu wako kuiFIKILIA kwa bidii zako, KAMA ukiweza KUVUMBUA kusudi lako na KULITIMIZA. Kwa lugha nyingine kusudi limeitwa WITO. Kwa bahati mbaya, majina yetu, kwa watu wengi sana, hayataji KUSUDI ndani yao! Sijui kama unajua kwamba kila KUSUDI lina jina, na hilo jina atapewa AFANYAYE mambo katika kusudi hilo. Kwa mfano, kama wewe unaitwa Mary, na ni nabii, lakini hutabiri, jina lako litakuwa Mary, kwa sababu ulipewa utotoni. Utaitwa Mary hadi kufa kama hutavumbua KUSUDI lako na kulitenda. Lakini, kuna jina ulipewa KABLA ya kuzaliwa, hilo jina LINATAJA kusudi lako. Kwahiyo, kama huyo Mary ataanza KUTABIRI, na watu WAKAKUBALI hiyo huduma yake ya unabii, jina lake litakuwa ‘nabii Mary’. Je! Wewe unai...