WACHUNGAJI WA KIPENDEKOSTE DAR WAVUNJA UKIMYA. WASEMA NA AJULIKANE MUNGU WA ELIA, WAITISHA MAOMBI YA SIKU TATU KAVU, WASIPOOKOKA WAFE
Ni zaidi ya mwaka sasa kumekuwa na uchomwaji na mauaji juu ya watumishi wa Mungu wa Kikristo na kwa muda sasa wakristo wamekuwa wako kimya kuona hatua gani zinachukuliwa na serikali yetu ya Tanzania. baada ya kuona kuwa bado mambo hayo yanaendelea wachungaji wameamua kuvunja ukimya. ikumbukwe kuwa kumekuwa na matamko mbalimbali ya jumuiya za kikristo ili kuishinikisha serikali kuwachukulia hatua kali wale wote wanaohusika na vurugu hizi za kidini mpaka sasa kila kitu kimebaki kuwa kiten dawili kisichoteguka huku baadhi wa wahamasishaji wakiendelea kurandaranda mitaani na huku wakiwa wamesababisha baadhi ya familia kuondokewa na wapendwa wao walio uliwa katika machafuko hayo. lakini haijaishia hapo hivi karibuni watumishi mbalimbali walikutana na kujadili kwa pamoja na kufikia muafaka wa kufanya maombi ya pamoja kwa siku tatu mfululizo. maombi hayo ambayo yataanza Tar 27 - 29 mwezi huu wa March utaratibu wa maombi hayo ni kila kanisa watafunga kwa masaa 24 kwa sik...