Historia ya Horatio Spafford na Wimbo wa “It Is Well with My Soul” ( nionapo amani kama swali)
Horatio Gates Spafford, mwanasheria na mfanyabiashara maarufu wa Chicago, aliandika wimbo maarufu wa Kikristo "It Is Well with My Soul" kutokana na majaribu makubwa aliyopitia maishani. Hadithi ya maisha yake ni somo la kuvutia kuhusu jinsi imani ya Kikristo inaweza kudumu hata katikati ya majonzi makubwa zaidi. Maisha ya Kwanza na Mafanikio Horatio Spafford alizaliwa mnamo 1828 na kukulia katika familia ya Kikristo. Alikuwa wakili mwenye mafanikio makubwa huko Chicago na pia alimiliki mali nyingi, hasa ardhi. Yeye na mke wake Anna walikuwa waumini wa kweli na waliheshimika katika jamii. Wakati huo, walikuwa na watoto watano—mtoto wa kiume na mabinti wanne. Hata hivyo, maisha yao yaliyokuwa yamejaa furaha na mafanikio viligeuka ghafla kupitia mfululizo wa majaribu yaliyowapitia. Pigo la Kwanza: Moto Mkubwa wa Chicago (1871) Mnamo mwaka 1871, Great Chicago Fire ulioharibu sehemu kubwa ya jiji la Chicago uliathiri sana familia ya Spafford. Moto huo uliunguza mali ny...