Mwimbaji wa muda mrefu Jennifer Mgendi anatarajia kufanaya
uzinduzi wa albamu ya wema ni akiba. Jennifer amesema pamoja na uzinduzi huo
pia atakuwa akimshukuru Mungu kwa kufikisha miaka 20 akifanya huduma hii ya
uimbaji 1995 -2015. yeye ni kati ya waimbaji wachache wa kike ambao wameanza
uimbaji siku nyingi, pamoja na kuimba amekuwa akiandaa na filamu za kikristo,
Albamu ya kwanza alitoa mwaka 1995 na mpaka sasa kuna alnbamu zisizopungua 8
ambazo alishatoa mpaka sasa na pia movie yake ya kwanza alitoa mwaka 2004 na
hadi sasa ameshatoa movie 4, kwa sasa yeye anaishi kwa kufanya kazi ya Mungu
kwa kuimba na kuandaa movie.
ennifer alizaliwa tarehe 02 May, 1972 hospitali ya Ocean Road,
Dar es Salaam, mama yake akiwa Mwendapelu Nalaila na baba akiwa Fanuel Mgendi.
anao ndugu watatu tuliozaliwa kwa baba ambao ni Mao Mgendi, Mlenge Mgendi na
Noel Mgendi. alipata pata elimu yake katika shule na vyuo mbalimbali kama shule
ya msingi Mgulani,Shule ya sekondari Kisutu,Chuo cha Ualimu Korogwe, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam. Pia alifanya kazi katika taasisi mbalimbali zikiwemo Shule
ya Sekondari Handeni, Shule ya Sekondari Tanbaza, Shule ya Sekondari Benjamin
Mkapa, Chuo Kikuu cha afya Muhimbili. Kuanzia 2007 aliacha kazi za kuajiriwa na
kujiajiri katika kazi za sanaa ya kumtukuza Mungu.
Pia jennifer alisema Mwaka
2012 alitoa albam ya DHAHABU ambayo ni mkusanyiko wa nyimbo pendwa zilizochaguliwa
kutoka katika albam zake tatu za mwanzo yaani kutoka albam ya Nini, Ukarimu
Wake na Nikiona Fahari. Albamu hii inanyimbo kumi na mbili. Sababu ya kutoa
album hii ni kuziboresha nyimbo kwani kipindi cha nyuma hasa albam ya Nini na
Ukarimu Wake wakati zinarekodiwa teknolojia ilikuwa chini kwa hiyo hata Cd
hazikuwapo wakati huo kwa hiyo nyimbo zimerekodiwa upya ili kuendana na
mabadiliko ya teknolojia. Uzinduzi unafanyika jumapili hii 28/06/2015 saa 8 mchana
uzinduzi huo mgeni rasmi atakuwa ni
Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Dr Barnabas Mtokambali na uzinduzi huo utafanyika
katika ukumbi wa kanisa la DCT uliopo Tabata shule na hakuna kiingilio chochote
na watu wote mnakaribishwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni