Alhamisi, 13 Machi 2014

ILE FILAMU MAARUFU YA YESU KURUDIWA UPYA

FILAMU YA YESU KURUDIWA UPYA

Brian Deacon katika uigizaji wa filamu ya Yesu, ambayo imeundwa tena kisasa zaidi. ©fb
Takriban baada ya miaka 35 tokea sinema ya Yesu iliyoigizwa na Brian Deacon, muigizaji ambaye baadhi ya watu wa kizazi cha siku hizi huamini kuwa ndiye Yesu, hatimaye imerudiwa tena katika mfumo wa hali ya juu, kuanzia picha na hata uchanganyaji wa sauti.
Jesus, filamu ambayo ndio imevunja rekodi na inaongoza duniani kwa kutafsiriwa kwenda lugha nyingi, kwani kwa mujibu wa kitabu cha kumbukumbu cha Guiness, (Guiness World Record) filamu hio imetafsiriwa kwenda lugha 1,197 tofauti duniani kote, na kutazamwa na zaidi ya mara bilioni moja, huku watu zaidi ya milioni mbili wakiokoka kutokana na kutazama sinema hiyo.
Utengenezaji upya wa filamu hiyo umehusisha kupitia 'frame' moja baada ya nyingine. Sekunde moja ina takriban fremu 24, yaani kwa lugha rahisi, picha 24 ndani ya sekunde moja ambazo zinatengeneza mtiririko wa muondoko, na hivyo kufanya jumla ya fremu 173,000 kupitiwa moja baada ya nyingine na kisha kuihariri upya na kusawazisha rangi ili iendane na mfumo wa kisasa.
Kwa upande wa sauti, mfumo wa 5.1 Surround system ndio ambao umetumika, huku maeneo mengine yakiongezewa sauti kulingana na utayarishaji wa kisasa ulivyo kwa kizazi cha sasa.
Maisha yake, Kifo chake, Tumaini letu ©The Jesus Film fb
Filamu hiyo ambayo imepewa jina la 'The Jesus Film', inatarajia kuwa ya kipekee kama ambavyo wakati inatengenezwa miaka 35 iliyopita, ilikuwa na mashiko kwa ulimwengu, kutokana na namna ilivyoandaliwa, kutayarishwa na kuongozwa.

Filamu hii ilipotoka miaka 35 iliyopita, kwa kweli ilikuwa mbele, yaani imeendelaea kuliko sisi. Mkurugenzi mtendaji wa Jesus Film Project anaeleza, akisifia namna imesukwa ikasukika, ambapo kila kilichoigizwa, kimetoka kwenye Biblia, na kupitia na wachungaji na wanazuoni zaidi ya 450 ili kujiridhisha dhidi ya upotoshaji.

Brian Deacon, muigizaji ambaye katu hatosahaulika kwa wasifu aliouonyesha, mara nyingi amekuwa akichanganywa na Yesu, hasahasa kwa watu ambao wanatazama filamu hiyo bila kuwa na rejea ya mafundisho. Na licha ya kwamba filamu hii imetazamwa na wengi ulimwenguni, ni watu wachache tu nchini Marekani ambao wameiona, ila kwa kuwa imetengenezwa upya kwa namna ya kisasa zaidi katika kuadhimisha miaka 35 tokea kupikwa mnamo mwaka 1979, inaaminiwa kuwa watu wengi zaidi wataiona, ikizingatiwa kuwa nakala moja ya DVD itajumuisha lugha za Kiingereza, Kispanish, Kikorea, Kiarabu, Kifaransa, Kijerumani, Kivietnam, na Kimandarin.

Machi ndio mwezi ambao filamu hiyo inatarajia kuanza kutazamwa kwenye majumba ya sinema ulimwenguni, ambapo kufikia mwezi Aprili, filamu hiyo itakuwa imewekwa pia kwenye mfumo wa DVD na Blu-Ray. Kuwa wa kwanza kuupenda ukurasa wa facebook wa filamu hii na uendelee kupata habari zaidi.

Charisma News imeandika
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: