Watu wawili
wameuwawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya baada ya wapiganaji wa
kundi la al Shabaab kushambulia basi moja la abiria lilokuwa likielekea
eneo la Mandera Kaskazini mwa kenya kutoka Nairobi.
Shambulio hilo la kigaidi lilitekelezwa hii leo asubuhi.
Walioshuhudia wameambia mwandishi wa BBC kuwa abiria wa kiislamu waliwalinda wenzao wakristo kwa kukataa kugawanywa kwa makundi.
Wasafiri
waislamu nchini Kenya walilazimika kuingilia kati kuokoa maisha ya
wakristu waliokuwa nao katika basi lililotekwa na wapiganaji wa
Alshabaab.
Waislamu hao walitahamaki walipotekwa na wapiganaji wa
Al Shabaab kisha wakaanza kutenganishwa katika makundi mawili ya
waislamu na wasio waislamu.
Hapo ndipo waligundua nia yao ni kuwaua kama walivyofanya katika mauaji kama hayo mwaka uliopita.
Mhudumu wa kampuni ya basi la Makkah ameithibitishia BBC tukio hilo katika barabara ya kutoka Mandera kuelekea mjini Nairobi.
Mwezi Novemba mwaka uliopita wapiganaji wa Al Shabaab waliteka basi moja na kuwaua abiria 28 ambao hawakuwa Waislamu.
Kundi hilo liligonga vichwa vya habari mwezi Aprili lilipowaua wanafunzi wakristo 148 katika chuo kikuu cha Garissa.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775
AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni