Katika hali isiyokuwa ya kawaida kutokea katika chaguzi za
miaka ya nyuma kwa waimbaji wa nyimbo za injili kujitosa na kuamua kuimba
nyimbo zinazowahusu wana siasa hapa inchini. Hadi sasa waimbaji wengi
wameshatoa nyimbo zao zinazowahusu wale wanaowaona kuwa wanafaa, mwimbaji
Bahati Bukuku ametoa wimbo unaomhusu Lowasa na pia mwimbaji chipukizi Abu lev
nae kaimba wimbo unaomhusu Lowasa, mwingine na Flora Mbasha ambaye nae ametoa
wimbo unao mhusu Halima Mdee na ametangazwa kuwa pamoja na chama cha chadema
katika kampeni zinazokuja. Na waimbaji wengine ambao ni Rose Mhando, Bonny
Mwaitege, Martha Mwaipaja, Upendo Nkone wametoa wimbo unaomhusu Mwigulu Chemba
na nyimbo hizo zote zinzpatikana katika mitandao ya kijamii.
Baadhi ya watu waliozisikiliza nyimbo hizo wamekuwa na hisia
za tofauti hasa kwa kundi kubwa kujitosa katika kuwaimbia wanasiasa, na hata
wengine wamediliki kusema yamkini pesa ndizo zinawafanya wakubali kuimba nyimbo
hizo, lakini huo ni upande mmoja wa shilingi na wengine wamesema wagombea wengi
wa chama tawala kuwakimbilia waimbaji wa injili hii imetokana na pengo
liliachwa na mwimbaji maarufu marehemu captain Komba sasa kila mtu anatafuta angalau
wa kujaribu kuziba pengo hilo. Vuguvugu la mchakato wa uchaguzi mkuu unaendelea
inchini ambapo vya vyote vya siasa vinajipanga vyema katika uchaguzi utakao
fanyika mwezi wa kumi.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni