Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UPENDO NKONE. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo UPENDO NKONE. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 25 Juni 2015

OMBA YESU ANASIKIA YAZINDULIWA NCHINI MAREKANI NI ALBAMU YA TANO YA PENDO NKONE.

kwa mara ya kwanza Mwanamuziki wa nyimbo za Injili kutoka nchini Tanzania,Upendo Nkonne jumapili hii ameweka wakfu na kuzindua Album yake mpya ya tano inayokwenda kwa jina la ""Omba Yesu Anasikia " toka atoe album zingine za awali, uzinduzi ambao umefanyika nchini Marekani ndani ya kanisa la All Nations BreakThrough Church (ANBC) - Gahanna Ohio. upendo Nkone ni kati ya waimbaji wachache wa Tanzania ambao kwa sasa wanaenda nje ya nchi mara kwa mara kwa miariko ya kufanya huduma za uimbaji wa nyimbo za injili. 

ikumbukwe katika albamu zake za dvd kuna nyimbo nyingine anarekodia nje ya inchi katika kubadilisha mazingila lakini pia kupata ubora wa kimataifa. cd hiyo imezinduliwa katika kanisa la kiswahili huko marekani ambalo liko chini ya mchungaji Nkone na imewekwa wakfu na mchungaji kiongozi wa kanisa hilo.

Mchungaji wa kanisa la ANBC Donnis na Nnunu Nkone wakiiweka wakfu Album yake Upendo Nkonne

Mchungaji Kiongozi na mke wake wakifuatilia tamasha hilo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Ijumaa, 12 Juni 2015

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WAGEUKIA NYIMBO ZA KISIASA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kutokea katika chaguzi za miaka ya nyuma kwa waimbaji wa nyimbo za injili kujitosa na kuamua kuimba nyimbo zinazowahusu wana siasa hapa inchini. Hadi sasa waimbaji wengi wameshatoa nyimbo zao zinazowahusu wale wanaowaona kuwa wanafaa, mwimbaji Bahati Bukuku ametoa wimbo unaomhusu Lowasa na pia mwimbaji chipukizi Abu lev nae kaimba wimbo unaomhusu Lowasa, mwingine na Flora Mbasha ambaye nae ametoa wimbo unao mhusu Halima Mdee na ametangazwa kuwa pamoja na chama cha chadema katika kampeni zinazokuja. Na waimbaji wengine ambao ni Rose Mhando, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja, Upendo Nkone wametoa wimbo unaomhusu Mwigulu Chemba na nyimbo hizo zote zinzpatikana katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watu waliozisikiliza nyimbo hizo wamekuwa na hisia za tofauti hasa kwa kundi kubwa kujitosa katika kuwaimbia wanasiasa, na hata wengine wamediliki kusema yamkini pesa ndizo zinawafanya wakubali kuimba nyimbo hizo, lakini huo ni upande mmoja wa shilingi na wengine wamesema wagombea wengi wa chama tawala kuwakimbilia waimbaji wa injili hii imetokana na pengo liliachwa na mwimbaji maarufu marehemu captain Komba sasa kila mtu anatafuta angalau wa kujaribu kuziba pengo hilo. Vuguvugu la mchakato wa uchaguzi mkuu unaendelea inchini ambapo vya vyote vya siasa vinajipanga vyema katika uchaguzi utakao fanyika mwezi wa kumi.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Jumanne, 9 Desemba 2014

USIKOSE SIKU 3 ZA MATUMAINI VCCT MBEZI BEACH


 KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Ijumaa, 29 Agosti 2014

TAMASHA KUBWA LA COLUMBUS INTERNATIONAL GOSPEL MUSIC FESTIVAL NI LEO NA KESHO

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Jumanne, 29 Julai 2014

KAMA UNA NAFASI USIPANGE KUKOSA

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 4777775 au Whatup, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Jumamosi, 3 Mei 2014

TAMASHA KUBWA MWANZA KESHO,MALOPE NDANI YA NYUMBA WANA MWANZA TUKUTANE CCM KIRUMBA

Lile tamasha kubwa la pasaka linaloandaliwa na Msama promotion linalokwenda kwa jina la tamasha la pasaka kufanyika kesho jijini Mwanza. Katika tamasha hilo malkia wa nyimbo za Injili Africa yaani Rebecca Malope kutoka A Kusini atakuwepo, aidha waimbaji mbalimbali wa hapa nchini watakuwepo akiwapo malkia wa Injili TZ Rose Mhando John lishu na wengine wengi. Wewe mkazi wa Mwanza tafadhali usikose

Jumamosi, 26 Aprili 2014

JESCER MICHAEL NI CHIPUKIZI WA NYIMBO ZA INJILI, MWENYE KIPAJI CHA KUTUNGA NA KUIMBA, MALENGO YAKE NI KUUFIKIA ULIMWENGU KWA UIMBAJI.

Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa ambayo kuna waimbaji maarufu wa injili hapa Tanzania vile vile iko mikoa kama Mbeya, Kigoma, Arusha, Dar na kwingineko. ukitaja jina kama Rose Mhando ni jina linalojulikana sana na ni malkia wa nyimbo za injili hapa Tanzania na hata kuweza kuweka mkataba na kampuni kubwa la mziki hapa Africa.

 lakini katika mkoa huu wa Dodoma kuna waimbaji wengi sana ni under Ground na wengine ndo wana chipukia. Blog hii ilipata nafasi ya kuonana na baadhi ya waimbaji hao mjini Dodoma na kufanya nao mahojiano kujua machache katika huduma zao. kama mnavyojua na ni ukweli usio pingika kuwa kwa sasa mziki wa injili Tanzania umeshika hatamu kuliko miziki wowote. na hii ni kutokana na umahili na kazi nzuri zinazofanywa na watu wote katika muziki huu wa Gospel hii ni pamoja na waimbaji, wapigaji ala za muziki, maproduza wa audio na Video pamoja na wasambaji wa kazi hizi wamekuwa na mchango mkubwa, hii imeleta kutokea kwa uamusho na kuwa na waimbaji wengi wanaochipukia na ambao wana fanya vizuri katika tasnia hii na kuleta changangamoto kwa waimbaji wakongwe.

 Jescer Michael ni mmoja ambaye tuliweza kufanya mahojiano mafupi kujua kwa ufupi amejipanga vip. ni kati ya waimbaji chipukizi wenye kipawa cha uimbaji, na sauti yenye mvuto ambayo haichoshi kusikiliza. sikiliza hahojiano hapo chini

sikiliza wimbo wake hapa chini unaitwa Hakuna kama Yesu



Jescer  anahitaji watu watakao msaidia kukamilisha albamu yake ambayo bado anarekodi amekwama fedha za kumalizia basi kama utaguswa unaweza kuwasiliana nae kwa simu. 0788009030 na 0716584777
au unaweza kumpata facebook https://www.facebook.com/jescer.michael?fref=ts

au unawe kuwasiliana nasi

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Jumatatu, 21 Aprili 2014

TAMASHA LA PASAKA HIVI NDIVYO KEKE ALIVYOTOKELEZEA


Tamasha la Muziki wa Injili la Pasaka limefanyika  katika Mkoa wa Dar-es-Salaam na maelfu ya Watanzania walijitokeza  kushuhudia wanamuziki wa Injili kutoka nchi mbalimbali kama Tanzania, Kenya, UK, Zambia na Afrika Ya Kusini.
 
Tamasha la Pasaka ambalo huandaliwa na Msama Promotion hufanyika kila wakati wa Pasaka na Christmas hapa nchini ili kutoa fursa kwa Wakristo kutoka madhehebu mbalimbali.kuweza kukusanyika kwa pamoja na kumtukuza Mungu wao.

Katika Siku ya jana Mgeni rasmi wa Tamasha hilo alikuwa Mhe. Bernard Membe aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa sasa yupo nje Kikazi.
 
Baadhi ya Wanamuizi wa injili waliohudumu ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Keke Kutoka South Africa. Malkia wa Muziki wa injili Rose Muhando alipanda Jukwaani Saa 2 Usiku ili kuwahudumia watu.
Mhe. Benard Membe akisikiliza risala kutoka kwa Mchungaji Mwasota ambaye ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Pentekoste Ukanda wa Dar-es-Salaam
Keke mwanamuziki kutoka Africa Ya Kusini akihudumu katika Uwanja wa Taifa
Sehemu ya Umati ukiwa unafatilia matukio uwajani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe akiongea  kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya
 Laura Msama Mke wa Msama akiwa amekunja goti wakati akisalimiana na Mhe. Membe
 Mhe. Membe akiwa anasalimiana na Keke
Mwanamuziki kutoka Zambia Ephrahim Sekeleti akiwa anapasha pamoja na Backers Vocalists wake.
 Upendo Kilahiro akiwa anaenda sawa katika Uwanja wa Taifa
 Mise Anaeli akuwa anapuliza tarumbeta Uwanjani
 Sarah K Mwanamuziki Kutoka Kenya akiwa anaimba Wimbo Wake "Liseme"
"Kwani Ni Jambo Lipi hilo, Yeye asiloliweza"
Baadhi ya Waimbaji Wa Glorious Worship Team wakiwa Jukwaani wakienda sawa
Hii Group hapa ilikuwa si Mchezo kwa Mwendo wa Kusebeneka
Blogger akienda sawa na Mwanamuziki Kutoka Uingereza siku ya Jana
 Mwanamuziki Nguli kutoka Africa Ya Kusini Keke akiwa Jukwaani
 Keke akiwa Kikazi zaidi
 Backers Vocalists wakiwa wanaenda sawa
 Keke Kikazi Zaidi
 Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anaenda sawa
Drummer Boy
 kwa hisani ya Sam Sasali

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Alhamisi, 25 Aprili 2013

WAIMBAJI WA TANZANIA KUSHIRIKI TAMASHA LA KIMATAIFA MAREKANI


Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania Christina Shusho anatarajia kushiriki Tamasha la The International Gospel Music festival kwa Mwaka 2013, lililoandaliwa na Kanisa la All Nation Break Through lililoko lililoko Columbus, Ohio, USA chini ya Watumishi wa Mungu Pastor Donnis & Nnunu Nkone.

Waimbaji wengine watakaoshiriki ni pamoja na Upendo Nkone, Pastor Daniel Kiza na Wengine wengi watakaoendelea kutangazwa siku chache zijazo. Taarifa zaidi kuhusu Muda na Sehemu zitatolewa hivi karibuni.

 KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela