Jumatatu, 21 Aprili 2014

TAMASHA LA PASAKA HIVI NDIVYO KEKE ALIVYOTOKELEZEA


Tamasha la Muziki wa Injili la Pasaka limefanyika  katika Mkoa wa Dar-es-Salaam na maelfu ya Watanzania walijitokeza  kushuhudia wanamuziki wa Injili kutoka nchi mbalimbali kama Tanzania, Kenya, UK, Zambia na Afrika Ya Kusini.
 
Tamasha la Pasaka ambalo huandaliwa na Msama Promotion hufanyika kila wakati wa Pasaka na Christmas hapa nchini ili kutoa fursa kwa Wakristo kutoka madhehebu mbalimbali.kuweza kukusanyika kwa pamoja na kumtukuza Mungu wao.

Katika Siku ya jana Mgeni rasmi wa Tamasha hilo alikuwa Mhe. Bernard Membe aliyemwakilisha Rais Jakaya Kikwete ambaye kwa sasa yupo nje Kikazi.
 
Baadhi ya Wanamuizi wa injili waliohudumu ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Sara K kutoka Kenya, Glorious Worship Team, John Lisu, Mwanamuziki kutoka UK na Keke Kutoka South Africa. Malkia wa Muziki wa injili Rose Muhando alipanda Jukwaani Saa 2 Usiku ili kuwahudumia watu.
Mhe. Benard Membe akisikiliza risala kutoka kwa Mchungaji Mwasota ambaye ni Mwenyekiti wa Makanisa ya Pentekoste Ukanda wa Dar-es-Salaam
Keke mwanamuziki kutoka Africa Ya Kusini akihudumu katika Uwanja wa Taifa
Sehemu ya Umati ukiwa unafatilia matukio uwajani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe akiongea  kuhusu Mchakato wa Katiba Mpya
 Laura Msama Mke wa Msama akiwa amekunja goti wakati akisalimiana na Mhe. Membe
 Mhe. Membe akiwa anasalimiana na Keke
Mwanamuziki kutoka Zambia Ephrahim Sekeleti akiwa anapasha pamoja na Backers Vocalists wake.
 Upendo Kilahiro akiwa anaenda sawa katika Uwanja wa Taifa
 Mise Anaeli akuwa anapuliza tarumbeta Uwanjani
 Sarah K Mwanamuziki Kutoka Kenya akiwa anaimba Wimbo Wake "Liseme"
"Kwani Ni Jambo Lipi hilo, Yeye asiloliweza"
Baadhi ya Waimbaji Wa Glorious Worship Team wakiwa Jukwaani wakienda sawa
Hii Group hapa ilikuwa si Mchezo kwa Mwendo wa Kusebeneka
Blogger akienda sawa na Mwanamuziki Kutoka Uingereza siku ya Jana
 Mwanamuziki Nguli kutoka Africa Ya Kusini Keke akiwa Jukwaani
 Keke akiwa Kikazi zaidi
 Backers Vocalists wakiwa wanaenda sawa
 Keke Kikazi Zaidi
 Mpiga drums nambari moja wa Keke akiwa anaenda sawa
Drummer Boy
 kwa hisani ya Sam Sasali

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: