Thursday, November 17, 2016

USIKOSE UZINDUZI JUMAPILI HII 20/11/2016

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

VINE SONG LIVE IN TANZANIA

 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Thursday, October 27, 2016

ONYESHA MATUKIO YAKO YOTE LIVE, HARUSI, BIASHARA, RADIO, TV, IBADA, MKUTANO.NK

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Wednesday, October 12, 2016

Je! WEWE ni SUMAKU ya MUNGU?
This is automatic! Ukianza ku-focus kwa Mungu na kuondoa moyo wako kwenye mambo yote yanayomchukiza Mungu, Mungu naye anaanza ku-focus kwako na KUJA karibu yako. Wewe unakuwa kivutio kwa Mungu kama sumaku. Hapo ni bila kuomba chochote wala kumwita Mungu; Atakuja tu.
 
Kwa maana macho ya BWANA hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake” (2 Nyakati 16:9).
 
Na, ukiondoa focus kwa Mungu, na kuhamishia MOYO wako kwa mtu au miungu mjngine; Mungu anaondoka bila kufukuzwa, tena bila kuaga! Hii ndio maana halisi ya wivu; Mungu ni mwenye wivu!
 
BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, Amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake Na moyoni mwake amemwacha BWANA” (Yeremiah 17:5).
 
Kumbuka KANUNI hii, “Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili” (Yakobo 4:8) - WEWE ndio unaanza KUMKARIBIA Mungu ili YEYE akukaribie wewe; Unafanya hivyo kwa KUULEKEZA moyo wako kwake na kufanya mapenzi yake. Hapo UTANASA yale macho ya Mungu yanayo kimbia-kimbia duniani mwote kusaka watu wa namna hii.
 
Chagua leo, unataka UKARIBU na Mungu au na MTU (miungu mingine)? Kisha chukua hatua.

Frank P. Seth
 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

KUFUNGA NI ZAIDI YA KUACHA KULAJE, KILE ULICHOACHA KULA UNAKIFANYEJE?

UNASUBIRI JIONI ILI UPIGE SAHANI 3 KULIPIZA?

Kufunga ni Sacrifice

Mara nyingi wakristo tumekuwa na maombi ya kufunga lakini wakati mwingine kuna kanuni za kufunga huwa hatuzifuati ambazo zinatokana na neno la Mungu


baada ya kumaliza kufunga  unatakiwa kuwatembelea wenye mahitaji mbali mbali kama ilivyoandikwa kwenye Isaya 58.... Na kuwapatia Sacrifices zetu au vitu ambavyo  tumeacha kutumia kwa muda wa siku ambazo ulifunga


KARIBU USOME

Isaya 58:3-14

3 Husema, Mbona tumefunga, lakini huoni? Mbona tumejitaabisha nafsi zetu, lakini huangalii? Fahamuni, siku ya kufunga kwenu mnatafuta anasa zenu wenyewe, na kuwalemea wote watendao kazi kwenu.
 4 Tazama, ninyi mwafunga mpate kushindana na kugombana, na kupiga kwa ngumi ya uovu. Hamfungi siku hii ya leo hata kuisikizisha sauti yenu juu.
 5 Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
 6 Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
 7 Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
 8 Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
 9 Ndipo utaita, na Bwana ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;
 10 na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
 11 Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
 12 Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
 13 Kama ukigeuza mguu wako usihalifu sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya Bwana yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;
 14 ndipo utakapojifurahisha katika Bwana; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha Bwana kimenena hayo.KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

AWAMU TATU za UKRISTO 
1 Siku ile kukatukia adha kuu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemu; wote wakatawanyika katika nchi ya Uyahudi na Samaria, isipokuwa hao mitume. 2Watu watauwa wakamzika Stefano, wakamfanyia maombolezo makuu. 3Sauli akaliharibu kanisa, akiingia kila nyumba, na kuwaburuta wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani. 4Lakini wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno” (Matendo ya Mitume 8:1-4).
 
Kuna awamu tatu muhimu za ukristo ambazo ukiwa dunuani imekupasa kuzipitia na kutoa hesabu yake. Hatua hizi ni: kuzaliwa, kukua na kuzaa.
 
i.                    KUZALIWA
Ukristo unaanza na kuzaliwa kwa mara ya pili, kwa kumpokea Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Kwa tafsiri nyingine, hii inaitwa “kuzaliwa kwa maji na kwa Roho” (Yohana 3:1-6). Hili huwa zoezi rahisi tu kama ukiamua leo, “Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu” (Warumi 10:10).
 
ii.                 KUKUA
Mtoto azaliwapo, hunyeshwa maziwa safi (yasiyoghoshiwa/yasiyotiwa maji) ili aweze kukua vizuri. “Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpatekuukulia wokovu” (1 Petro 2:2). Hii ni hatua ya muhimu sana ya Mkristo ya KUTAMANI kujifunza neno la Mungu ili aweze kukua.
 
Kiwango tofauti cha KUTAMANI maziwa hupelekea watoto wa kiroho kukua kwa KASI tofauti. Ndio maana ndani ya kanisa utakuta watu wawili, mmoja anamiaka kumi kanisani lakini bado analishwa maziwa tu wala hajakua popote. Mwingine ana mwaka mmoja lakini ameshakomaa kiasi cha kuanza kuzaa! Hii yote ni UAMUZI wa mtoto husika, je! Unatamaini MAZIWA?
 
iii.               KUZAA
Kazi ya kondoo ni KUZAA kondoo wengine. Kazi ya mchungaji ni kulisha kondoo ili wakue, tena kwa kusudi maalumu. Kondoo asipozaa huyo huondolewa kundini mapema kwa maana hana faida kwa mchungaji, tena yamkini, huharibu na kondoo wengine.
 
Angalia tena kwa namna hii, kama BWANA Yesu ni mzabibu, na sisi ni matawi; maana yake tuko kwake tayari, yaani tumevuka hatua ya kuzaliwa na tunaendelea kukua, lakini kuna hatua ya kuzaa matunda inakuja hapo. Akiona tawi LISILOZAA, Yeye hulikata! Na lile lizaalo hulisafisha ili liweze kuzaa zaidi (Yohana 15:1, 2). Lengo la kubaki kwenye mzabibu ni kuzaa!
 
Ukiangalia Matendo ya Mitume 8:1-4, utaona jinsi ambavyo kanisa liliongezeka kwa ‘kondoo kuzaa kondoo’ kwa sababu baada ya kufanyika WANAFUNZI wa Yesu (wakristo), chini ya mitume, ilibidi watawanywe kwa nguvu ili wakazae huko waendako. Mitume (wachungaji) wakabaki Yerusalemu, kondoo (waumini) wakaenda kuhubiri injili na kuzaa matunda (waumini wengine) huko walikokwenda.
 
Ni jambo lililozoeleka kwa nyakati hizi kwamba kazi ya kuzaa kondoo ni ya mchungaji (viongozi wetu wa kiroho), kisha kuwatunza na kuhangaika tena kuandaa mikutano na seminia za kiroho ili kuzaa tena na kukuza wachanga. Wakrito (kondoo) wamekaa tu kanisani wanaingia na kutoka jumapili kwa jumapili; hawazai kitu! Hii sio sawa.
 
Kumbuka, “shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya miti; basi kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa motoni” (Mathayo 3:10). Bwana akikutazama anakuombea kwa BABA kwamba upewe mwaka huu tena kama utazaa au la, na anakuwekea mbolea (unapata mafundisho mbalimbali na huduma zingine za kiroho), ili uzae; lakini usipozaa utakatwa tu kwa maana unaiharibu nchi. Tena sio kuzaa tu, unatakiwa kuzaa matunda MAZURI.
 
Angalia jambo hili, mitume walizaa wakristo wengi kwa KUSHUHUDIA habari za Yesu. Walijiita mashahidi. Yaani, WALISEMA yale waliyoona na kusikia kwa Bwana, hayo wanawaambia na wengine ili waamini (Matendo 22:15). Je! Wewe umewashuhudia wangapi?
 
Watu wengi wamejifariji kwamba kutoa SADAKA inatosha. Angalia, kutoa sadaka ni muhimu, lakini je! Wewe ni SHAHIDI wa BWANA? Kama wewe ni kondoo, ni vyema, ila swala ni KUZAA sio kutoa sufi (sadaka) tu, kuzaa ni LAZIMA!
 
Kila mtu anajua kwamba mti unafaida nyingi, kwa mfano: kuni, mbao, kivuli, nk. Lakini mwenye shamba anataka MATUNDA kwanza! Tunajua unavipawa vingi na unatoa sadaka nyingi kanisani kwako, je! Umezaa kondoo? Hili ni swali la kujiuliza na ni changamoto kwa kila mtu. Kumbuka, matunda ni ya kila msimu na yanatakiwa yawe mazuri na ya mengi. Ndio maana tawi lizaalo husafiswa ili lizae ZAIDI. Bwana anataka matunda zaidi; yaani kuongezeka katika kuzaa mwaka hadi mwaka.
 
Jitathmini umri wako wa kiroho. Kila siku unalishwa tu pale kanisani kwako. Je! Hukui tu? Utazaa lini? Je! Unajua una MUDA ambao ukifika ni LAZIMA uzae? Ndio maana ule mti ulipewa MUDA wa kuzaa kabla ya kukatwa. Jitahidi kuweka jambo hili kwenye maombi na matendo kwa maana hukuitwa kupiga pambio, kusikiliza neno na kuandika notsi tu pale kanisani kwako; leta matunda yako kwa mamana UNADAIWA. Au unasubiri ulazimishwa kwa adha kama lile kanisa la mwanzo?
 
Frank P. SethKAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Saturday, July 9, 2016

  HUDUMU KIVYAKOVYAKO (FREE STYLE) “1 Basi palikuwa na mtu mmoja wa Mafarisayo, jina lake Nikodemo, mkuu wa Wayahudi. 2Huyo alimjia usiku, akamwambia, Rabi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezaye kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, isipokuwa Mungu yu pamoja naye. 3Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu” (Yohana 3:1-3).  “3Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele” (Danieli 12:3). Hebu fikiri, Nikodemo, Farisayo na mkuu wa Wayahudi, yaani Mwalimu wao katika mfumo rasmi (ana ajira kule kwenye dhehebu lake); anakuja GIZANI kujifunza kwa ‘Mwalimu wa mtaani’, asiye na ajira wala idara maalumu, BWANA Yesu, ambaye kwa kweli KAZI zake zinatambulika kwa VIWANGO fulani vya BORA wa kipekee; ila hana CHETI! Sasa jiulize: Kwanza, nani alimwambia Nikodemo kwamba Yesu ni Mwalimu (Rabi)? Jibu ni KAZI zake. Yesu hakuwa na cheti cha kuhitimu mafunzo yao ya Kifarisayo! Pili, Nani alimwambia Nikodemo kwamba Yesu anatoka kwa Mungu? Jibu, MATUNDA ya KAZI zake. Tofautisha KAZI na MATUNDA ya kazi. Kila mtu anaweza kufanya KAZI ila kwa MATUNDA yao tunaweza kuwatofautisha kwamba wametoka wapi. Zingatia MATUNDA zaidi kuliko KAZI maana matunda yatakutangulia hukumuni kabla ya KAZI zako. Ukiona mtu anajivuna na KAZI lakini anapuuza MATUNDA, kuna mambo mawili: kwanza sio MTUMWA (hafanyi kwa ajili ya bwana wake – faida za kiroho sio muhimu kuliko faida za mwilini); na Pili, anatafuta KIBALI kwa hao watu wamwonao kwa sababu ya faida za kipato au cheo au sifa au utukufu. Ukitazama hili, chunguza mambo yako ya gizani (ya siri asiyojua mtu); Hayo ni muhimu kujua aina ya MATUNDA yako, na hayo yatakusimamisha kuliko yale uyatendayo nuruni. Kwa habari hii ya Nikodemo, nataka nikwambie jambo moja la muhimu; fanya kazi yako (HUDUMA) uliyoitiwa (WITO) kwa nguvu na kwa bidii kama vile hakuna anayeona wala kulipa. Najua inawezekana hauko kwenye mfumo rasmi; fanya tu. Utakapozidi sana kufanya, na kumtii Mungu na kumpendeza, japo unafanya “kivyakovyako (free style)”, utagundua wapo WAKUU fulani (akina Nikodemo) wataanza kukunyemelea kwa SIRI gizani (wasikoonekana) wakijifunza kwako taratibu. Na kwa sababu wewe hujui, zidi kufanya kama hakuna mtu anaona hadi siku moja utashangaa kugundua kwamba kumbe walikuwa nyuma yako siku zote! Hivi ndivyo wale wazee (Mafarisayo na wenzao) walimfuatilia BWANA kila hatua na kumsikiliza na kujifunza hadi wakajua kwamba ametoka kwa Mungu! Sasa angalia tena, usishangae, kwa mfano; Siku moja wakipangwawachungaji mbele na kondoo zao wakiwa msururu nyuma yao, na ukaona WATUMISHI wengi sana wako nyuma yako wamejipanga (akina Nikodemo na wenzake). Utaanza kujiuliza na kujitetea, “mimi sio mchungaji na wala sina kanisa”. Ndipo BWANA atajibu kwa mfano na kusema, “hata mimi sikuwa na hicho CHEO cha kichungaji wala sikuwa na HEKALU langu, ila nina kondoo wengi ambao wako kwenye mazizi tofauti”. Na, watu wa namna hii watang’aa kama nyota za Mbinguni milele kwa maana walifanya kazi ya kuwaongoza wengi kutenda mema bila kujali mahali, dini zao na vyeo vyao. Kwa waraka huu nakupa shauri, fanya kazi ya huduma kivyakovyako kama uongozwavyo na ROHO. Kaa chini ya mchungaji wako na ujue umuhimu wake; lakini kumbuka mkiwa shambani mwa BWANA wote ni watenda kazi, kila mmoja akiwa nakiserema chake na wote mtatoa hesabu kwa BWANA mmoja.  Angalizo, usisubiri kupigiwa makofi, kutiwa moyo wala kusifiwa na mtu. Jinsi utakavyozidi kufanya vizuri tarajia vita kuliko shangwe. Na wengi walio hirimu (wakuu waliokutangulia) zako watakutenga kwa sababu ya ubora wako na si kwa udhaifu wako. Kuwa makini. Usikate tamaa. Mungu anakuheshimu kwa sababu unamtumikia, heshima ya wanadamu haitakusaidia sana japo ni LAZIMA uwaeshimu na kuwapenda.    Frank P. Seth  

Saturday, April 9, 2016

UNAFANYA NINI UNAPOFANIKIWA? (Sehemu ya I)Swali “UNAFANYA nini UNAPOFANIKIWA?” sio la kupuuza hata kidogo. Mara nyingi nimesikia watu wakisema, “ukitaka kujua tabia ya mtu, mpe pesa nyingi au cheo kikubwa” Nimetathmini sana maisha yangu binafsi, na nikatazama maisha ya wetu wengine na kuona jambo hili, “maisha baada ya mafanikio yanaweza kuwa baraka itakayokuinua kwenye baraka zingine, au laana itakayokuangamiza wewe mwenyewe”.

Kama hukujua, mafanikio yanaweza kuwa uangamivu, angalia hapa, “32Maana kurudi nyuma kwao wajinga kutawaua, Na kufanikiwa kwao wapumbavu kutawaangamiza” (Mithali 1:32).

Ukiangalia wakati wana wa Isarael wanatoka UTUMWANI kwenye nchi Misri kwenda nchi ya ahadi, iliyojaa MAZIWA na ASALI, utaona onyo ambalo Musa aliwapa, akisema,  “11 Jihadhari, usije ukamsahau BWANA, Mungu wako, kwa kutozishika amri zake, na hukumu zake, na sheria zake, ninazokuamuru leo. 12Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; 13na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka; 14basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa; 15aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu, 16aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako. 17Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo. 18Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo” (Kumbukumbu la Torati 8:11-18).

 Unafanya nini unapuvuka ngazi fulani ya maisha, na kuingia ya juu zaidi, unapofika mahali ambapo “umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake; 13na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka”, (Kumb. 8:12b-13), Unafanya nini? Angalia tabia yako ya sasa na ya zamani, kisha jiulize, wewe ni yule yule au ni mwingine? Je! Hofu yako kwa Mungu ni ile ile au imebadilika? Jitihada zako katika mambo ya Mungu imeathiriwa vipi na mafanikio yako? Unapojiuliza maswali haya na kujijibu mwenyewe angalia usijipandelee wala kujihesabia haki kupita kiasi. Ni muhimu kijiuliza na kujijibu na kuchukua hatua, wewe mwenyewe.

Sasa angalia tena jambo hili, unajua kwamba mafanikio yako hayakuja kwa nguvu zako mwenyewe tu; unajua ulipomlilia Mungu wakati wa mateso na vita vyako na Akakuvusha, Yeye ndiye aliyekupa “nguvu za kupata utajiri” (Kumb. 8:18). Mbona leo umesahau?

Ukitaka kujua kwamba umemsahau Mungu, kumbuka wakati “ule” Alipokuwa Ngao na Kigao kwako. Kila ulipokuta magumu ulimgeukia kwa KUFUNGA na KUOMBA, sasa umepata pesa na mafanikio, hayo ndio sasa yamekuwa ngao na kigao kwako. Unakinga KIFUA kwa sababu  unajua unakazi nzuri, biashara nzuri, watu wanakujua, unajina kubwa mjini, nk. Wala hukumbuki kumshirikisha tena Mungu mipango yako! Je! Hukumsahau Bwana Mungu wako wewe? Mbona humgeukii tena katika MAHITAJI yako ila unatafuta faraja na msaada kwa miungu mingine?

Frank P. Seth.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Tuesday, April 5, 2016

UNAFANYA NINI UNAPOFANIKIWA? (Sehemu ya 2)

 


Kwanini Mzabibu? Kwani Bwana alishindwa kuchagua miti mingine mizuri na ya gharama zaidi porini, akachagua kujiita Mzabibu? Haya ni mwaswali ambayo nilijiuliza. Maana Yesu ni Mzabibu na sisi ni matawi, na Baba yake ni Mkulima (Yohana 15:1, 5).
Nimeona mambo kadhaa:
1. Mungu amekuchagua sio kwa UBORA wako, ila kwa sababu amekupenda.
"1Neno la BWANA likanijia, kusema, 2Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni? 3Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yo yote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo cho chote? 4Tazama, watupwa motoni kwa kuni moto umeziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yo yote? 5Tazama, ulipo kuwa mzima, haukufaa kwa kazi yo yote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yo yote?" (Ezekieli 15:1-5).
 
2. Kwa kuitwa MZABIBU au TAWI la mzabibu, maana yake, Mungu anajua MWANZO wako na udhaifu wako (kwamba huwezi neno lolote pasipo yeye), na ambavyo hukufaa kwa chochote; ila amekuchagua kwa KUSUDI lake na kwa AJILI yake, na anategemea MATUNDA kutoka kwako.
Ndo maana BWANA anasema, "Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni" (Yohana 15:16) Hatuna haki yetu wenyewe iliyotustahilisha kuitwa wana wa Mungu; sisi tumechaguliwa tu. Hii ni maana halisi ya Neema.
 
3. Kuna GHARAMA imelipwa kukufikisha hapo ulipo sasa.
Ukisoma Ezekieli 16: 1-63, Utaona jinsi ambavyo BWANA ameGHAMIKIA watu wake, na sasa WAMEFANIKIWA na WAMEMWACHA!
Angalia, mambo machache katika mlango huu:
[i]. Ulikotoka/Asili yako - umetoka kati ya mataifa
"Asili yako na kuzaliwa kwako kwatoka katika nchi ya Mkanaani; Mwamori alikuwa baba yako, na mama yako alikuwa Mhiti" (.
Eze. 16:3b)
[ii]. Kuzaliwa kwako - Hakuna aliyekijali, ulikuwa masikini tu aliyestahili kufa kwa sababu uliachwa. Hukupendwa, hakuna aliyekujali, huna jina.
"4Na katika habari za kuzaliwa kwako, siku ile uliyozaliwa, kitovu chako hakikukatwa, wala hukuoshwa kwa maji usafishwe; hukutiwa chumvi hata kidogo, wala hukutiwa katika nguo kabisa. 5Hapana jicho lililokuhurumia, ili kukutendea lo lote la mambo hayo kwa kukuhurumia; lakini ulitupwa nje uwandani, kwa kuwa nafsi yako ilichukiwa, katika siku ile uliyozaliwa" (Eze. 16:4, 5).
 
[iii]. Mungu akakufuata katika hali yako mbaya na KUKUOKOA, ukapewa UZIMA bure.
" 6Nami nilipopita karibu nawe, nikakuona ukigaagaa katika damu yako, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai; naam, nalikuambia, Ujapokuwa katika damu yako, uwe hai" (Eze. 16:6).
[iv]. Mungu AKAKUBARIKI na KUKUONGEZA
"7Nalikufanya kuwa maelfu-elfu, kama mimea ya mashamba, ukaongezeka, na kuzidi kuwa mkubwa, ukapata kuwa na uzuri mno; matiti yako yakaumbwa, nywele zako zikawa zimeota; lakini ulikuwa uchi, huna nguo" (Eze. 16:7)
 
[v]. Mungu akakuFUNIKA aibu yako. Sasa unaHESHIMA na JINA mjini
"8Basi, nilipopita karibu nawe, nikakutazama; tazama, wakati wako ulikuwa wakati wa upendo; nikatandika upindo wa vazi langu juu yako, nikakufunika uchi wako; naam, nalikuapia, nikafanya agano nawe, asema Bwana MUNGU, ukawa wangu" (Eze. 16:8).
[vi]. Ukapewa kusafiwa kwa Neno na kujazwa Roho na VIPAWA, ambavyo vimekufanyia NAFASI ya KUKETI na wakuu wa nchi
 
"9Kisha nikakuosha kwa maji; naam, nalikuosha kabisa damu yako, nikakupaka mafuta" (Eze. 16:9)
[vii]. UTUKUFU wa Mungu ukadhihirika maishani mwako kwa ile NEEMA uliyopewa; Mkono wa Mungu ulidhihirika sana juu yako, naam, ukavikwa UTAYARI kwa ajili ya HUDUMA.
"10nikakuvika nguo ya taraza, nikakupa viatu vya ngozi ya pomboo, nikakufunga nguo ya kitani safi kiunoni mwako, nikakufunika kwa hariri. 11Nikakupamba kwa mapambo pia, nikatia vikuku mikononi mwako, na mkufu shingoni mwako. 12Nikatia hazama puani mwako, na pete masikioni mwako, na taji nzuri juu ya kichwa chako. 13Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikilia hali ya kifalme" (Eze. 16:10-13).
[viii]. JINA lako likawa MAARUFU kwa sababu ya ile NEEMA juu yako, na KUFANIKIWA sana juu ya nchi.
"14Sifa zako zikaenea kati ya mataifa kwa sababu ya uzuri wako; kwa maana ulikuwa mkamilifu, kwa sababu ya utukufu wangu niliokutia, asema Bwana MUNGU" (Eze:16:14).
4. Baada ya KUFANIKIWA umefanya nini? Je! Umemkumbuka BWANA na kuendelea KUMTAFUTA na KUMFUATA kwa BIDII?
[i]. Wapo walioABUDU mafanikio yao badala ya Mungu! Na kufanya MACHUKIZO yale ya MATAIFA walikotwaliwa.
 
"15 Lakini uliutumainia uzuri wako, ukafanya mambo ya kikahaba kwa sababu ya sifa zako, ukamwaga mambo yako ya kikahaba juu ya kila mtu aliyepita; ulikuwa wake" (Eze. 16:15).
[ii]. Je! Umekumbuka ULIKOTOLEWA na Mungu? Pale ulipokuwa sio kitu chochote, wala huna jina? Sasa, badala ya kuwapeleka wengine kwa BWANA unawapoteza na wale walio wadogo; Umewapotosha!
"21hata ukawaua watoto wangu, na kuwatoa kwa kuwapitisha motoni kwa hao? 22Na katika machukizo yako yote, na mambo yako ya kikahaba, hukuzikumbuka siku za ujana wako, ulipokuwa uchi, huna nguo, ukawa ukigaagaa katika damu yako" (Eze. 16:21, 22)
 
[iii]. Sasa unajijengea UFALME wako, na JINA lako na wala humwinui Mtakatifu wa Israel! Unajifanyia mambo yako kwa faida zako kwa kuzidisha machukizo yako.
"25Umejenga mahali pako palipoinuka penye kichwa cha kila njia, ukaufanya uzuri wako kuwa chukizo, ukatanua miguu yako kwa kila mtu aliyepita karibu, ukaongeza mambo yako ya kikahaba" (Eze. 25).
[iv]. Kwa ajili ya FAIDA yako unafanya KAMA wafanyavyo mataifa, na Jina la BWANA linatukanwa juu ya nchi. Wanasema, "hivi na huyu ni mtu wa Mungu, mbona anafanya hivi?"
"26Tena umezini na Wamisri, jirani zako, wakuu wa mwili; ukaongeza mambo yako ya kikahaba, ili kunikasirisha....28Pia umefanya mambo ya kikahaba pamoja na Waashuri, kwa sababu ulikuwa huwezi kushibishwa; naam, umefanya mambo ya kikahaba pamoja nao, wala hujashiba bado. 29Pamoja na hayo umeongeza mambo yako ya kikahaba katika nchi ya Kanaani, mpaka Ukaldayo, wala hujashibishwa kwa hayo" (Eze. 26, 28-29).
 
[v]. Je! Hukukaza mkono wako KUTAWALA na KUTUMIKISHA wengine kwa FAIDA yako tu?
"30Jinsi moyo wako ulivyokuwa dhaifu, asema Bwana MUNGU, ikiwa unafanya mambo hayo yote, kazi ya mwanamke mzinzi, 31apendaye kutawala watu; kwa kuwa wajijengea mahali pako pakuu penye kichwa cha kila njia, na kufanya mahali pako palipoinuka katika kila njia kuu; lakini hukuwa kama kahaba, kwa maana ulidharau kupokea ujira. 32Mke wa mtu, aziniye! Akaribishaye wageni badala ya mumewe!" (Eze. 16:30-32)
 
[vi]. Umevifanyia nini VIPAWA vya Mungu? Fedha na utajiri, na Neema? Je! Hivyo havikuwa uharibifu kwa wengine na kubomoa Zaidi kuliko kujenga?
"17Pia ulivitwaa vyombo vyako vya uzuri, vya dhahabu yangu na vya fedha yangu, nilivyokupa, ukajifanyia sanamu za wanaume, ukafanya mambo ya kikahaba pamoja nazo" (Eze. 16:17)
5. Kuna jambo Mungu alitarajia kukona baada ya kukuinua kwa kiasi hicho. Je! Umerudi nyuma hata ukamsikitisha Mungu? Mafanikio yako yanamtukuza Mungu au yanamtukana?
Kumbuka hali yako ya mwanzo ulipokuwa si kitu, kama mti wa mzabibu usio faa kwa chochote, sasa uko juu sana kwa kuwa BWANA amekuinua.
Haya maneno yamesema na mimi kwa nguvu kubwa, na nimeona nilivyopungua. Nimeweka hapa, sio kukuhukumu ila kama mimi Frank nilivyopata changamoto na kujitathminina, nimeweka hapa ili uone kama kuna mahali pa kurekebisha, rekebisha; ILI kwa mara hii tena MAFANIKIO yako yawe Baraka si kwa watu tu ila na kwa Mungu pia.

Frank P. Seth
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

SIRI ZA JANGWANI SEHEMU YA KWANZA BY Frank P. Seth

 
 
Kama wewe ni msomaji wa biblia, utagundua kwamba katika hadithi maarufu za biblia, na ambazo mahubiri mengi sana yametaja, tangu zama za manabii na mitume wa zamani hata sasa, ni safari ya wana wa Israel Jangwani.
Pamoja na mambo MAGUMU mengi ya jangwani, hapo ndipo Mungu ALISEMA uso kwa uso na Musa, na hata wana wa Israel walisikia sauti ya Mungu kwa masikio ya damu na nyama.
 
Ni katika kipindi hiki cha kupita Jangwani, ambapo Mungu amesema na Musa kule mlimani, na kumpa amri 10. Ni kule jangwani ambapo vitabu vya Torati, ambavyo ni mwongozo wa taifa la Israel hadi leo viliandikiwa kutokana na mambo ambayo Mungu alizungumza. Kwenye safari za maisha kuna sehemu nyingi za kujifunza, lakini usikose darasa lako upitapo jangwani.
 
Je! Umegundua kwamba katika maisha yetu kuna vipindi vya kupita jangwani? Nyakati ambazo unaona kabisa mambo hayaendi (kifamilia, kazini, kwenye ndoa, shuleni, nk). Jangwani ni mahali pa kupungukiwa na kiu; Ni mahali pa kero na misukosuko mingi, lakini, hapo ndipo kuna DARASA zuri la maisha yako. Hapo jangwani ndipo Mungu atasema na wewe kwa habari ya hatma yako. KOSA la kuondoka JANGWANI isivyosahihi litakugharimu HATMA ya maisha yako.
 
Sasa angalia jambo hili. Bwana Yesu alipopelekwa kujaribiwa, Roho alichagua kumpekeka NYIKANI pia. BWANA Alikaa siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa, hapo ni jangwani. Zingatia jambo hili, ukiwa jangwani, ni mahali ambapo pia utaisikia sauti ya Ibilisi kwa DHAHIRI sana. Kila mara sauti hii itakuwa ikikutaka KUONDOKA jangwani (to find a comfort zone) kwa namna ya KUMKOSEA Mungu. Ndio maana Ibilisi alikuja na vitu vingi vya kuvutia, ili kuondoa USIKIVU wa Yesu kwa Mungu wake (Neno). Kila adui alipotaka kumhamisha katika KUSUDI la Mungu, Yesu alisema, "imeandikwa" kisha Alikataa vishawishi vya Adui.
 
Kukaa katika Neno la Mungu, ndio siri ya ushindi wako upitapo jangwani. Kumbuka siku zote, jangwa halitadumu siku zote, ni njiani tu, lakini hapo ndipo utasikia suati ya Mungu pia, Akikwambia mambo mengi ya hatma ya maisha yako. Hapo ndipo utajifunza mambo na kumsikia Mungu akijibu yale maombi yako ya siku nyingi. Kaa hapo jangwani usiondoke. Zidi kumkaribia Mungu kwa KUFUNGA na KUOMBA, kaa jangwani kwa saburi na utulivu kabisa, naam, bila KUNUNG'UNIKA. Ushindi wako ni mkubwa ukivuka hapo.
 
Usishangae wakati ukiuwa PEKEYAKO jangwani, ndipo ADUI hukujia na kukuonesha UZURI wa TUNDA, kama alivyofanya kwa mama yetu Hawa pale kwenye bustani ya Eden (alipokuwa peke yake). Zingatia jambo hili, kweli tunda lafaa kwa chakula, kweli tunda linapendeza macho, kweli tunda linavutia sana; lakini kumbuka hapo unashughulika na HATMA yako. Kweli unaweza KUEPUKA jangwa lako kwa kufanya mambo mengi ya kukupa AHUENI (kivuli kidogo), lakini jiulize, Je! Ndivyo Neno la Mungu limekuagiza hivyo? Kama jibu ni HAPANA, jua Adui anataka KUKATILIA MBALI hatma yako kama alivyofanya kwa mama yetu Hawa.
 
Utulivu wako JANGWANi utakusaidia kusikia SAUTI ya Mungu kwa namna ambavyo hujawahi kusikia ukiwa katika madarasa mengine. Darasa la jangwani ni la muhimu; tulia hapo usiondoke hadi utakapopita, maana, hapo sio mahali pa kudumu sana japo kuna maumivu mengi. Vumilia tena kidogo.
 
Frank P. SethKAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

SIRI ZA JANGWANI SEHEMU YA PILI BY Frank P. Seth

  
Kuna mambo kadhaa ya kukumbuka UPITAPO jangwani:

1.      Ni marufuku kuchoka/kukata tamaa/ kuzimia roho. Kuchoka ni kikwazo cha mavuno yako.
9 Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho” (Wagalatia 6:9). 
Nikiangalia katika Wagalatia 6:9, naona kwamba kuna uwezekano wa kupanda mbegu, yamkini na kupalilia, hata kunyeshea, lakini KUSUBIRI kwa muda mrefu, katika hali ngumu (jangwani), inaweza kuleta hali ya KUKATA TAMAA/KUCHOKA/KUZIMIA MOYO, ambayo hali hii inazimisha UWEZO wako wa kuvuna (kupata majibu ya maombi yako au kupata matarajio yako kule ng’ambo ya jagwa).
 
2.      Manun’guniko ni kivutio cha adhabu badala ya msaada.
 
5Watu wakamnung’unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. 6BWANA akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. 7Watu wakamwendea Musa, wakasema, Tumefanya dhambi kwa sababu tumemnung’unikia Mungu, na wewe; utuombee kwa BWANA, atuondolee nyoka hawa. Basi Musa akawaombea watu” (Hesabu 21:5-7)

Angalia maneno yako unapopita jangwani. Mara nyingi ni rahisi kunung’unika kwa sababu ya adha mbaliambalia unazopitia. Utakuta mtu anaanza tu kusema, “kwa hali hii, mi naona maisha ya wokovu ni magumu sana”, “aheri hata ndoa za wamataifa, naona yangu ni mateso tu”, “yaani pamoja na kumtumikia Mungu bado nateseka kuliko watenda dhambi”, “sasa unafikiri mtu ataishije namna hii?”, “hata Mungu anaona kwamba nimevumilia muda mrefu”, n.k. Haya ni maneno ya mtu aliyechoka na yamkini sasa anajifariji wakati anatafuta namna ya “kuchepuka” apitapo jangwani.
 
3.      Kanuni za kula manna; kila chakula (Neno) huja kwa wakati na kusudi maalumu kukufundisha. Elimu ya jangwani ni muhimu kwa maisha ya Kaanani.

35 Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arobaini, hata walipofikilia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikilia mipakani mwa nchi ya Kanaani” (Kutoka 16:35).

Ukiwa jangwani, bado Mungu atakuletea “chakula cha siku”, hadi uvuke hapo. Kumbuka, manna ilikuwa “chakula cha kuokota”, wana wa Israel hawakutafuta, kazi yao ilikuwa ni kuokota tu, tena kwa KANUNI maalumu. Kila siku ilimpasa mtu kukusanya chakula cha siku moja, na siku ya 6 walikusanya chakula cha siku mbili, kwa sababu siku ya Sabato hawakutakiwa kufanya chochote ila kupumzika.

Kumbuka, siku 6 walikusanya chakula cha siku moja (hapakuwa na kiporo), na aliyekusanya zaidi, ile manna iliharibika! Angalia jambo hili, siku ya Sabato manna hiyo hiyo iliweza kudumu siku 2 bila kuharibika! Na, kwenye Sanduku la Agano ipo manna nyingine hata leo haijaharibika, imefichwa hadi kwenye ufalme ujao; watakaoshinda watapewa huko Mbinguni (Ufunuo 2:17).

Uwe makini na chakula (NENO) Mungu analosema nawe ukiwa jangwani. Huja kwa wakati maalumu na kwa kusudi maalumu, hilo Neno ndilo litakuvusha kwenye jangwa lako salama. Hilo Neno haliji holela, linakuja kwa namna maalumu kwa ajili yako. Omba sikio la “kusikilia” ili usikie litamkwapo.
 
4.      Ukimwangalia nyoka wa shaba utapona; Msaada wako unatoka katika Bwana. Yeye aliyakupitisha hapo jangwani anaDAWA ya kila shida yako.
 
8Bwana akamwambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo ataishi. 9Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi” (Hesabu 21:8,9).

Pamoja na majanga yote ya jagwani, Mungu hufanya “njia ya kutokea”, na msaada ambao imekupasa KUUJUA na KUTII ili weze KUPONA. Watu wengi waliofia jangwani ni kwa sababu ya kukosa UTII. Kumbuka siku zote, kama yuko NYOKA WA SHABA, kuumwa na NYOKA sio tatizo, dawa ipo. Watu wengi wamekatishwa tamaa kwa sababu katika kupita kwao jagwani wamemkosea Mungu (wakaumwa na nyoka za moto), na wemehukumiwa na wanadamu kwamba kwasababu wamemkosea Mungu wataangabia bila shaka! Hivyo, hawakuona sababu tena ya kuinua macho yao na kumwangalia ‘nyoka wa shaba’ ili wapone. Sikiliza, Inua macho yako sasa, angalia juu, Kristo anakuona ulipo, liitie jina lake UTAOKOKA na KUPONYWA kwa maana “kila aliitiaye jina la BWANA ataokoka”.

Yesu hatishwi na dhambi zako, wala hakuchukii wewe kwa sababu ya hayo makosa yako unayohukumiwa nayo; Amekuja kwa ajili ya mtu kama wewe, yaani “amekuja kwa walioDHAIFU wanaohitaji TABIBU”.
 
5.      Urefu wa jangwa unakutegemea wewe na sio Mungu. Kadri UNAVYOJIFUNZA mapema na KUTII ndivyo utafupisha urefu wa njia yako jangwani.

Wakati wana wa Israel walipotoka Misri, kulikuwa na njia fupi ya kufika Kaanani, ila kulikuwa na maadui, hivyo Mungu akawaepusha na vita kwa kuwapitisha MBALI. Sasa ona mambo mawili: Kwanza, Iliwapasa wazunguke umbali mrefu kwa sababu ya HALI yao wenyewe, kwa maana wangepitia VITA mapema, wengi wangekatishwa tamaa kwa sababu aidha HAWAJUI kupigana vita (maana kule Misri hawakujifunza vita ila kazi za ujenzi, na utumishi) au HAWAKUWA tayari kupigana; Njia yao ikawa ndefu. Pili, Baada ya kumkasirisha Mungu, wakiwa karibu kabisa na kuvuka Yordan, waliambiwa “wageuke” kurudi tena nyuma kuelekea jangwani. Hawakuwa tayari kuvukia ile AHADI kwa sababu ya uhaba wa IMANI yao, baada ya Mungu kusema nao kwa namna nyingi [Soma Hesabu mlango wa 13 na 14]. Hapa tena ni wao wenyewe!

Angalia hapa, “24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki. 25Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu” (Hesabu 14:24). Hawa watu walifika karibu kabisa na nchi ya ahadi, pale ambapo Musa alimtuma Kaleb na wale wengine 11 ili kuipeleleza nchi, na walitumia siku 40 tu kwenda Kaanani na kurudi. Inamaana baada ya miaka 40 jangwani, walibakiza siku hata hazifiki 40 ili kumaliza safari yao, na kuirithi ile AHADI, wakamkorofisha tena Mungu. Wakageukia jangwa kwa upya! Kwa sababu IMANI yao ilitindika, na kuna MAADUI bado! Ila walibakiza kidogo tu wamalize jangwa. Wakashindwa mahali pa kumalizia!

Angalia vita uliyonayo sasa, umepigana vingi, usichoke sasa, hata hii nayo utashinda tu. Simama, utamwona Mungu, jangwa sio la milele, ni njia tu, utavuka.

6.      Nguvu za kuvuka Yordan zinatoka kwa Mungu pia; Usikorofishane na Mungu, hutafika Kaanani, kwa maana bila yeye huna nguvu za kuvuka Yordan.
 
Kumbuka, Kutoka Misri palihitajika MUUJIZA wa kuvuka bahari ya SHAMU, na baada ya jangwa, palihitajika muujiza mwingine wa kuvuka YORDAN ili kuingia Kaanan. Ukikorofishana na Mungu, hata ukikimbilia kwa njia zako hadi ukingoni (ufukweni) mwa Yordan, utavukaje mto? Bado utagundua kwamba unamhitaji tena Mungu. Kuwa mtulivu jangwani. Mwombe Mungu akupe neema ya kutulia kabisa na kuchukua shule zake zote na KUKUA kiIMANI ili ukivuka hapo uingie hatua zingine za Baraka na kufanikiwa.
 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Sunday, February 28, 2016

COUNSELING TRAINING - MWENGE! AINA TATU ZA MTOTO KUJIFUNZA VITUWatafiti wamefanya utafiti na kugundua kuwa kuna aina tatu ya jinsi ambavyo mwanadamu (watoto) huweza kujifunza mambo.

1. Kujifunza Kwa Njia ya Kuhusianisha Mambo (Classical conditioning)
Kujifunza kwa kuhusianisha mambo kujilikanako kama (classical Conditioning) ni aina ya kujifunza ambapo mtoto anajifunza jambo kwa kuhusianisha na kitu fulani.
Kwa mfano kama unasafiri na kila ukisafiri unaporudi unarudi na zawadi kwa mtoto basi mtoto atahusianisha safari na zawadi kwamba ukiona baba au mama amesafiri basi ujue anaporudi lazima atakuja na zawadi.
Mgunduzi wa aina hii ya kujifunza kwa njia ya kuhusianisha (Classical Conditioning - Learning Through Association) Bwana Pavlov alifanya utafiti kwa kutumia mbwa. Kila mara alipokuwa anataka kumpa chakula alianza kwa kugonga kengere kwanza na mbwa akazoea kwamba ukisikia mlio wa kengere ujue chakula kimekuja.

Kuna wakati alikuwa anakwenda na kengere bila chakula, lakini mbwa mara zote aliposikia mlio wa kengere alikuwa akitarajia kupata chakula kwasababu alikuwa akiusianisha kengere na chakula.
2. Kujifunza kwa Njia ya Pongezi au Zawadi (Oparent Conditioning -Learning through Rewards)
Njia ya pili ya kujifunza mambo inaitwa kujifunza kwa njia ya pongezi au zawadi yaani (Oparent Conditioning - Learning through Rewards) iligunduliwa na mtafiti Edward L. Thondike na B.F Skiner.
Katika njia hii mtoto anapata kujifunza kwa kupitia kuwepo au kuondolewa kwa pongezi na zawadi.
Kuna aina mbili za mtoto kujifunza kwa njia ya ongezi au zawadi.
• Kupokea pongezi na zawadi anapofanya vizuri (Positive reinforcements)
Hii humaanisha kwamba mtoto anapokuwa amefanya jambo zuri anapokea pongezi au zawadi fulani kupitia pongezi au zawadi hizo mtoto anajifunza kwamba endapo atafanya jambo zuri basi anatarajio la kupokea pongezi au zawadi.
Mfano wa Baba yangu aliniahidi kuwa nikifanya vizuri kimasomo na nikajua kingereza atanipeleka nairobi kuishi huko

Wakati huo nairobi ilikuwa inaonekana kama Marekani ya Watanzania.
• Kupoteza Nafasi ya Kupokea pongezi na zawadi anapofanya vibaya (Negative reinforcements)
Hii humaanisha kwamba mtoto anapokuwa amefanya jambo baya au hajafanya kile alichokuwa anatarajiwa kukifanya, basi ile pongezi au zawadi ambayo ilikuwa aipate kwa sasabu ya kutokufanya vizuri basi ile zawadi au pongezi inaondolewa anakuwa haipati tena.
Hiyo inamfundisha kwamba kumbe kama akifanya kinyume ana anachotarajiwa kukufanya basi atakosa zawadi au pongezi fulani fulani.
Mfano wa Kijana wangu
Kuna mwaka sikumfanyia Birthday maana akikosea adhabu yake ikawa mwaka huu hakuna birthday party alimumia sana kwa kukosa sherehe hizo.

3. Kujifunza Kwajia ya Kuchunguza au Kutazama Bila Mhusika Kujua. (Observational Learning)
Aina hii ya tatu ya kujifunza kwanjia ya kuchunguza au kutazama bila mhusika kujua, iligunduliwa na mtafiti Albert Bandura ambaye aligundua kwamba, mtu anaweza kujifunza mambo yanayo fanyika kwa kuangalia tu mifano na tabia za watu wengine wanapokuwa wakifanya jambo.
Watoto walioona wazazi wao wakihusiana usiku na walipokuwa wakicheza kasichana na kavulana wakavua nguo wakaanza kuona yale waliyo yaona yakitendwa na wazazi wao.
Most is Caught than Taught
Kulingana na mtafiti Albert Bandora, kujifunza kwa kuchunguza kuna husisha hatua nne muhimu:
• Kuweka Umakini - Attention
Kuweka umakini kwa mtu au kwa tabia zake anavyofanya.
• Kukumbuka kile kilichofanywa na yule mtu mhusika - Retention
Anayejifunza lazima akumbuke kile alichokiona na kujifunza.
• Kufanya kile alichokiona kikifanywa na mhusika - Reproduction
• Motisha - Motivation
Watu wanatabia ya kupenda kuigiza kitu ambacho kinamfurahisha kuliko kile ambacho hakimfurahishi

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

COUNSELING TRAINING - MWENGE! WATOTO WANAZALIWA WAKIWA NA DHAMBI DHAMBI YA ASILI KWA WATOTO!


1. Ukimuwekea mtoto Mungu na Shetani halafu ukampa uhuru wa kuchagua amfuate nani, wengi tunadhani kwamba mtoto atamchagua Mungu lakini ukweli ni kwamba mtoto atachagua kumfuata shetani badala ya Mungu.

2. Watoto hawawezi kuchagua kwa hiari yao kutenda mema kwasababu ya ile nguvu ya dhambi ya asili itendayo kazi ndani ya mwanadamu..
3. Ni jukumu la wazazi kuhakikisha wanaweka mkakati wa makusudi kwa mtoto/watoto tokea wanapokuwa tumboni, kabla ya kuzaliwa kuzaliwa kwao mpaka makuzi yao mpaka watakapokuja kuwa watu wazima.

4. Ni wakati gani wa kuanza kuzungumza na mtoto wako? Jibu ni kwamba ni wakati akiwa mimba. Mtoto anauwezo wa kusikia tokea akiwa mimba hata kabla hajazaliwa.
5. Wazazi wasiwatarajie watoto kuwa wema wao wenyewe bila kuhakikisha wanawawekea njia madhubuti za kimungu na kuwasisitiza watoto wao kuzifuata na kuzikataa njia za shetani.
6. Watoto wetu wameuzwa kwa shetani ili kuwarudisha lazima kuwafundisha njia za kimungu na kuwawekea mikakati ya kumjua Mungu na kumfuata vinginevyo watamezwa na dunia na kamwe Mungu hawatamtaka.
Warumi 7:14 - 20

14 Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. 15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. 16 Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema.17 Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu 18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. 19 Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. 20 Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com