Jumamosi, 26 Aprili 2014

JESCER MICHAEL NI CHIPUKIZI WA NYIMBO ZA INJILI, MWENYE KIPAJI CHA KUTUNGA NA KUIMBA, MALENGO YAKE NI KUUFIKIA ULIMWENGU KWA UIMBAJI.

Mkoa wa Dodoma ni kati ya mikoa ambayo kuna waimbaji maarufu wa injili hapa Tanzania vile vile iko mikoa kama Mbeya, Kigoma, Arusha, Dar na kwingineko. ukitaja jina kama Rose Mhando ni jina linalojulikana sana na ni malkia wa nyimbo za injili hapa Tanzania na hata kuweza kuweka mkataba na kampuni kubwa la mziki hapa Africa.

 lakini katika mkoa huu wa Dodoma kuna waimbaji wengi sana ni under Ground na wengine ndo wana chipukia. Blog hii ilipata nafasi ya kuonana na baadhi ya waimbaji hao mjini Dodoma na kufanya nao mahojiano kujua machache katika huduma zao. kama mnavyojua na ni ukweli usio pingika kuwa kwa sasa mziki wa injili Tanzania umeshika hatamu kuliko miziki wowote. na hii ni kutokana na umahili na kazi nzuri zinazofanywa na watu wote katika muziki huu wa Gospel hii ni pamoja na waimbaji, wapigaji ala za muziki, maproduza wa audio na Video pamoja na wasambaji wa kazi hizi wamekuwa na mchango mkubwa, hii imeleta kutokea kwa uamusho na kuwa na waimbaji wengi wanaochipukia na ambao wana fanya vizuri katika tasnia hii na kuleta changangamoto kwa waimbaji wakongwe.

 Jescer Michael ni mmoja ambaye tuliweza kufanya mahojiano mafupi kujua kwa ufupi amejipanga vip. ni kati ya waimbaji chipukizi wenye kipawa cha uimbaji, na sauti yenye mvuto ambayo haichoshi kusikiliza. sikiliza hahojiano hapo chini

sikiliza wimbo wake hapa chini unaitwa Hakuna kama Yesu



Jescer  anahitaji watu watakao msaidia kukamilisha albamu yake ambayo bado anarekodi amekwama fedha za kumalizia basi kama utaguswa unaweza kuwasiliana nae kwa simu. 0788009030 na 0716584777
au unaweza kumpata facebook https://www.facebook.com/jescer.michael?fref=ts

au unawe kuwasiliana nasi

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: