Ijumaa, 12 Juni 2015

WAIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI WAGEUKIA NYIMBO ZA KISIASA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida kutokea katika chaguzi za miaka ya nyuma kwa waimbaji wa nyimbo za injili kujitosa na kuamua kuimba nyimbo zinazowahusu wana siasa hapa inchini. Hadi sasa waimbaji wengi wameshatoa nyimbo zao zinazowahusu wale wanaowaona kuwa wanafaa, mwimbaji Bahati Bukuku ametoa wimbo unaomhusu Lowasa na pia mwimbaji chipukizi Abu lev nae kaimba wimbo unaomhusu Lowasa, mwingine na Flora Mbasha ambaye nae ametoa wimbo unao mhusu Halima Mdee na ametangazwa kuwa pamoja na chama cha chadema katika kampeni zinazokuja. Na waimbaji wengine ambao ni Rose Mhando, Bonny Mwaitege, Martha Mwaipaja, Upendo Nkone wametoa wimbo unaomhusu Mwigulu Chemba na nyimbo hizo zote zinzpatikana katika mitandao ya kijamii.

Baadhi ya watu waliozisikiliza nyimbo hizo wamekuwa na hisia za tofauti hasa kwa kundi kubwa kujitosa katika kuwaimbia wanasiasa, na hata wengine wamediliki kusema yamkini pesa ndizo zinawafanya wakubali kuimba nyimbo hizo, lakini huo ni upande mmoja wa shilingi na wengine wamesema wagombea wengi wa chama tawala kuwakimbilia waimbaji wa injili hii imetokana na pengo liliachwa na mwimbaji maarufu marehemu captain Komba sasa kila mtu anatafuta angalau wa kujaribu kuziba pengo hilo. Vuguvugu la mchakato wa uchaguzi mkuu unaendelea inchini ambapo vya vyote vya siasa vinajipanga vyema katika uchaguzi utakao fanyika mwezi wa kumi.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni