Baada ya kutokuonekana kwa muda sasa katika matamasha
hatimaye Mwimbaji Flora Mbasha tar 14/06/2015 atazindua DVD yake mpya
inayokwenda kwa jina la nipe nguvu ya kushida. DVD hiyo ina nyimbo 10. Flora amesema DVD hiyo
imetengenezwa chini ya studio yake inayoitwa flem record, amesema pia tamasha
la kipindi hichi atalifanya kwa namna ya tofauti ambapo nyimbo zote atakazoimba
zitaimbwa live na hata sasa yuko kwenye maandalizi makubwa pamoja na mazoezi
ili kuwapa radha adimu wote watakaohudhulia siku hiyo. alipoulizwa kwanini
ataimba live tofauti na ilivyozoeleka kutumia cd, alisema Nitaimba live maana
huo ndiyo mziki wenyewe radha watu wameshasikiliza sana cd nyumbanikwake, Hivyo
mtu anapokuja ategemee kupata Vitu vizuri zaidi vyenye upako zaidi.
alipoulizwa
kuwa watu hawajakuona kwenye matamasha kwa muda sasa wategemee nini kuona
kutoka kwako alijibu Watu wategemee kazi nzuri na nyimbo zenye nguvu ya kubwa
Mungu Kwani Lengo langu ni kumtangaza YESU kwa dunia nzima wajue na wamsifu na
kumtumaini yeye peke yake. mpaka sasa mgeni rasmi katika uzinduzi huo
hajajulikana ijapo alisema atajulikana muda si mrefu. swali la mwisho kwa Flora
lilikuwa nini kitafua baada ya uzinduzi
wake nae alisema Baada ya kuzindua hapa Dar inategemea kwenda Mwanza na Arusha
na baada ya hapo atatangaza ratiba nyingine na alimaliza kuwaomba watu
kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha lake kwani watu watamwona Mungu lakini pia
watapata kununua DVD yake hiyo mpya ambayo itapatikana siku hiyo kwenye
uzinduzi waimbaji wengine wataosindikiza uzinduzi huo ni pamoja na Edson Mwasabwitwe, Christopher Muhagila, Neema Gasper, Madam Ruti, Tumaini Njole pamoja na Mahanaimu bendi
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni