Alhamisi, 28 Mei 2015

JOHN LISU AANDA TAMASHA LA KUKATA KIU YAKO TAR 14/06/2015



Mwimaji John Lisu ameandaa tamasha la KIU, mwimbaji huyo ambaye huwa anafanya matamasha ya kuimba live, amesema kutokana na kutokufanya tamasha lolote ndani ya jiji la Dar es Salaam, watu wengi wamemtaka kufanya tamasha ili wakate kiu yao, kwa kuona kiu hiyo ya washabiki wangu nimeamua kuliita tamasha hilo KIU, nawakaribisha watu wote katika jiji la Dar waje wakate kiu yao siku hiyo na watakutana na nguvu za Mungu na kusababisha kiu yao yote kuisha. Tamasha hilo litafanyika Tarehe 14/06/2015 katika kanisa la VCC Mbezi kuanzia saa 3:00PM, katika tamasha hilo atatambulisha nyimbo zake mpya ambazo ataziimba kwa mara ya kwanza katika tamasha hilo. amesema waimabaji wengine watakao msindikiza katika tamasha hilo ni pamoja na Pastor Safari, mpuliza mdomo wa bata maarufu Mise, Angel Magotti, na the Voice. John Lisu amemalizia kwa kusema kuwa watu wanaruhusiwa kuchagua nyimbo ambazo wanataka aimbe katika tamasha hilo ili kukata kitu yao wasiliana nae kama una wimbo unataka aimbe.
 

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: