Jumamosi, 19 Aprili 2014

PICHA ZA HARUSI ZA AMOSI. YESU NI MWANAUME ANABADILISHA. HUYU NI MUISLAM ALIYEOKOKA ALIKUWA SHOGA, JINA AUNT ASU, KAKUTANA NA MWANAUME WA WANAUME YESU KAMBADILISHA SASA ANAMTUMIKIA MUNGU, AMESHAREKODI CD YAKE.


Amosi akiwa na mkewe baada ya kufunga harusi.

 Yesu anaendelea kuonyesha uwezo wake wa kubadilisha maisha ya wanadamu, zaidi upendo wake kwa wanadamu kuonyesha kuwa hana upendeleo hata kama mtu ni mwovu namna gani basi yeye bado yeye anampenda tu, kwani yeye hakuja kwa waliowazima maana hawahitaji dakitari bali wale waliopotea, walio kwenye vifungo vya shetani na kuwahamishia katika pendo lake na kuwapa maisha ya heshima yenye furaha na upendo. hii inamhusu sana aunt Asu ambaye hapo mwazo alikuwa shoga wa kutupwa ameshaolewa mara nyingi na kuachwa, na si hivyo tu bali aliishi maisha ya kudhalilika ya kuvyaa mavazi ya kike na kujipodoa. lakini upendo wake Mungu na neema ya kristo ikamwangazia na kupata neema hii ya wokovu na kuamua kuokoka.

ni heshima ya namna gani ya harusi ya heshima kama hii mbele za madhabahu ya Bwana

Mtumishi wa Mungu Amosi akiimba moja ya nyimbo zake.
 Kwa kweli Yesu anabadilisha kabisa na kumfanya mtu kuwa kiumbe kipya huyu sasa tena siyo Aunt Asu kama wengi walivyozoea kumwona sasa ni Mtumishi wa Mungu ambaye kwa sasa amejikita katika kumtumikia Mungu kwa sasa amesharekodi albamu yake ya nyimbo za injili, na amesha anza kurekodi na dvd muda si mrefu itaingia katika soko la muziki wa injili, kati ya nyimbo ameimba kuna unaoelezea maisha yake wakati anatumikishwa na shetani lakini sasa kabadilika.
 hili tukio la kihistoria lilifanyika katika kanisa la TAG Magomeni tar 13-04-2014 Amosi alipofunga pingu za maisha na kudhihilishia uma kuwa sasa yeye kabadilishwa na yesu na sasa ana maisha mapya.

wakiingia ukumbini

Akiimba nyimbo






hicho ni cheti kuonyesha ndoa hii ni halali



Msajili wa ndoa hiyo mch D. Kanemba na mapaparazi nao walikuwepo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: