Ijumaa, 26 Oktoba 2012

ZAKAYO MAGULU CAMERA MAN NO 1 TANZANIA KUANDAA TAMASHA LA KUREKODI DVD LIVE DEC 23 MWISHO WA MWAKA HUU

Mr&Mrs Magulu siku ya harusi yao wakiwa na malehemu Kanumba the Great
 Jina la zakayo Magulu si geni hasa wale waangaliaji wa kwaya na movie za Marehemu kanumba. mimi nilimfahamu alipoturekodi mkanda wa kwaya yetu ya Revival Magomeni kipindi hicho akiwa na Mtitu Game na akawa ana record movie na baadae akawa anafaya kazi ya kurekodi filamu za marehemu Kanumba. na katika blog ya kanumba the great aliwahi kusema kuwa Zakayo he the best camera man in Tanzania. nami naamini kutokana na kazi nyingi ambazo amezifanya na anaendelea kuzifanya. na hata DVD ya sifa zivume ya John Lisu ni moja ya camera man waliorekodi. sasa mwaka huu anakuja kivingine kabisa kwani yeye mwenyewe sasa ana andaa tamasha kubwa la kisasa kwani vitatumika technolojia mpya katika kuboresha DVD hiyo iwe kwenye viwango vya kimataifa. katika ukurasa wake wa fb ameandika hivi
MY BROTHERS $ SISTERS NINAPENDA KUWAJULISHA KUWA TAREHE 23 DEC 2012 NATEGEMEA KUFANYA LIVE CONSERT RECORDING...UKUMBI NI MAKUMBUSHO YA TAIFA POSTA MKABALA NA IFM.CONSERT ITAANZA SAA 9 ALASILI MPAKA SAA 1 JIONI, TEGEMEA KUKUTANA NA BWANA....LAKINI PIA KUWAONA NA KUSALIMIANA NA WATU AMBAO SI RAHISI KWA MBANANO WA MAJUKUMU KUKUTANA NAO.....TUNATEGEMEA KUANZA MATANGAZO MAPEMA HIVYO BADO TUNAKARIBISHA WADHAMINI ILI WAWEPO KATIKA MATANGAZO YETU....KWA MAMBO YANAYOHUSIANA NA TAMASHA NA SI KUIGIZA NIPIGIE KWA NAMBA 0757871916.
 na hakuishia hapo akafunguka tena na kusema
Zakayo Magulu Usijali itatoka haraka na kwa sababu nitaiedit mwenyewe katka ofisi zetu naamini itakuwa katika viwango vya kimataifa.....kwa sasa tumeagiza software za Mac zinazodeal na colour collection ili kupata best picture colour na namshukuru Mungu kwamba kwa upande wa sauti recording tumepata mafundi wazuri na vifaa vya kisasa,na ndugu yetu keppy yuko sawa sawa huko ukumbini kwa hiyo tegemea the best DVD
Zakayo akiwa location kikazi zaidi sasa nguvu hiyo na utalamu wote utahamia kwenye maandalizi ya hiyo DVD mpya itakayo rekodiwa december don't plan to miss it
 
 
jiandae kuwa mmoja wa washiriki katika tamasha hilo kwa kuombea kuwaambia wengine na kufika kwenye kamasha hilo.  blog hii imefanya mazungumuzo mafupi na kuambiwa kuwa kila kitu kinaendelea vizuri anaomba maombiya wapendwa ili kazi ya Mungu isonge mbele. tutaendelea kuwaletea maandalizi yanavyoendelea kadri tutakavyopata habari.

 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Alhamisi, 25 Oktoba 2012

TAMASHA LA PENUEL TAG KIGOGO MBUYUNI LAFANA

Kanisa la Penuel Tag lilianda tamasha kubwa la kusifu na kuabudu. kanisa hilo lililoko kigogo mbuyuni linaloongozwa na Mch Linde lilijaa watu hata kukawa hakuna sehemu ya kukaa. kwaya mbalimbali ziliimba katika tamasha hilo. kwaya hizo ni kama Revival Magomeni, Kwaya ya watoto Magomeni, Kwaya ya diodoxer ya Magomeni Christ Boyz band ya Magomeni TAG na kulikuwepo na kwaya ya wenyeji  kwaya kutoka Msasani TAG, kwaya ya EAGT Kigogo kwaya ya TAG Tandale kwa Mch Mshama, na waimbaji binafsi kadha wa kadha.



Mgeni rasmi akiingia kanisani


Mc wa Tamasha hilo ndugu Tony akicheza



Mr& Mrs Mwakibuti ambaye alikuwa mgeni rasmi mchungaji Linde 


watu wakiwa wamejaa mpaka nje ya kanisa

katika Tamasha hilo mgeni lasmi alikuwa ni Makamu mkurugezi CA's jimbo la mashariki Ndugu Joseph Mwakibuti. ambapo lengokubwa ilikuwa ni kuchangia ununuzi wa viti vya kanisa hilo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

KAMA KAWAIDA SIKUKUU YA VIJANA TAG MAGOMENI S YAFANA , WAANZA KUNUNUA VYOMBO VYA INJILI, MSINDI WA KUSOMA BIBLIA AJINYAKULIA KITITA CHA SH 600,000

Si mfano wa pesa bali ni pesa halisi na si bahati na sibu no ni washindi wa kwanza na wa pili wa shindano la kusoma biblia lililoandaliwa na chama cha vijana mshindi wa kwanza ni chesco kushote aliyejitwalia sh 600,000 na mshindi wa pili ni aliyejitwalia sh 400,000 shindano hilo lilidhaminiwa na Mr&mrs Lumelezi
Kila mwaka mwezi ya kumi huwa ni sikukuu ya vijana na Magomeni TAG huwa wanafanya sikukuu hizo bila kukosa kila mwaka huwa na mambo mapya na kuzutia ili mradi kuonesha tofauti ya miaka iliyopita. katika mwaka huu, vijana walijikita katika kuchangisha hela ili kununua vyombo vya kuhubilia injili, na hilo wameonyesha kwa vitendo baada ya kununua kinanda chenye thamani ya sh 3500,000. ukiacha taratibu zao za kila wiki kulikuwa na shindano la kusoma Biblia ambalo lildhaminiwa na Mr Lumelezi na washindi walikabidhiwa hela cash kama mnavyoona hapo juu. mwaka huu kuna nini jipya tujipange tusubili tuone yale watakayo yafanya blog hii inawapongeza kwa hatua waliyofikia.
Mwenyekiti wa vijana akiongea jambo kwenye sikukuu hiyo

Kwaya ya vijana wakiimba


washiriki wa shindano la biblia 10 walioingia fainali

Kwaya ya vijana

vijana wakiwa wamebeba keybord Yamaha pss910 yenye thamani ya sh 3500,000 ikiwa ni mikakati ya kununua vyombo vya injili

Vijana wakiwa na keybord yao

Kamati mpya inayohusika na wasomi na watu wenye taaluma zaokatika chama cha vijana

Mama mwenyekiti

Mwenyekiti katibu na Mwinj Kazimoto


Flora

John

Mdhamini w shindani la kusoma Biblia Ndugu Lumelezi

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Jumatatu, 22 Oktoba 2012

MALI ZA MTUME MWINGIRA WA EFATHA ZACHOMWA MOTO

Mtume mwingira

WANANCHI wenye hasira ambao wanadaiwa kuwa wakazi wa kijiji cha Sikaunga wilayani hapa, wamevamia kambi kwenye shamba lililonunuliwa na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha Tanzania na kusababisha hasara ya zaidi ya Sh milioni 228.

Wakazi hao walifanya uharibifu mkubwa ambapo inadaiwa kuwa wameteketeza kwa moto matrekta mawili makubwa aina ya New Holland, nyumba kadhaa kubomolewa na shehena ya mahindi kuchomwa moto wakimtaka mwekezaji huyo kuwaachia ardhi yao ambayo wanadai amewapora.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda amekiri kutokea kwa tukio hilo hivi karibuni ambapo watu 11 wanaotuhumiwa kuongoza wenzao kufanya uvamizi huo wamekamatwa na juzi walifikishwa mahakamani.

Inadaiwa kuwa, tangu Nabii Mwingira auziwe shamba hilo lililokuwa la taifa la mifugo la DAFCO–Malonje lenye ukubwa wa ekari 10,000 na uongozi wa Halmashauri ya Manispaa miaka zaidi ya mitano iliyopita kwa bei ya Sh milioni 600 huku mwekezaji wake akituhumiwa kukiuka mkataba wa mauziano.

Hivyo, Serikali baada ya kupokea taarifa kuwa mwekezaji huyo ameanza kulima mazao mbalimbali tofauti na mkataba unaomtaka kufuga, iliuagiza uongozi wa mkoa wa Rukwa kuupitia upya mkataba.

Licha ya kukiukwa kwa mkataba huo, lakini pia watumishi wa shamba hilo wamekuwa wakituhumiwa kukamata na kutesa wananchi wanaoishi pembeni mwa shamba, ikiwa pamoja na baadhi yao kudai kukatwa masikio na wanawake kubakwa, hali iliyoibua uhasama baina ya watumishi wa shamba hilo na wakazi wa vijiji jirani.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi kijijini humo, wamedai kuwa wamevumilia kiasi cha kutosha, ndiyo maana wameamua kuchukua sheria mkononi, ikiwa ni jitihada za kumlazimisha mwekezaji huyo kuwaachia ardhi wanayodai ni mali yao.

Akizungumzia sakata hilo la uvamizi uliofanywa katika kambi hiyo ya Sikaunga, Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa hilo la Efatha mkoani Rukwa alikiri kuwa mmiliki wa shamba hilo amepata hasara ya zaidi ya Sh milioni 228 kutokana na uharibifu uliofanywa na wananchi hao.

Akifafanua, alisema uvamizi huo ulitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela, Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadhara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.

Hata hivyo, alikiri kuwa katika risala yao iliyoandaliwa na Mtendaji wa kijiji cha Sikaunga, R. Mkangwa kwa niaba ya Serikali ya kijiji hicho na kusomwa mbele yake pamoja kueleza changamoto kadhaa zinazowakabili, lakini pia wakazi wa kijiji hicho walitaka kujua hatima ya shamba hilo kama watarudishiwa.

Hata hivyo Mbunge Malocha amekanusha kuhusika na suala hilo, akisema taarifa hizo zimepikwa ili kumchafulia jina, akisisitiza hazina msingi wowote na kuongeza alikwenda hapo kufanya mikutano ya kuwahamasisha wananchi kujitokeza kutoa maoni ya Katiba mpya mbele ya tume ya kuratibu maoni hayo.

Hata hivyo Kamanda Mwaruanda alikanusha na kueleza kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwa mbunge huyo alihamasisha matumizi ya nguvu ya umma kuyakomboa mashamba hayo. Juhudi za kumpata Nabii Mwingira hazikufanikiwa.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Jumamosi, 20 Oktoba 2012

MATUKIO YA JANA YA MAANDAMANO


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Ijumaa, 19 Oktoba 2012

KWA MABINTI WOTE HII INAWAHUSU


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

MAASKOFU WA KKKT WATOA TAMKO KWA WATANZANIA WOTE KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUCHOMA MOTO MAKANISA YA KIKRISTO ENEO LA MBAGALA – DSM

 
Askofu Mkuu wa KKKT, Askofu Dk. Alex G. Malasusa(kushoto)
 


Wapendwa Katika Bwana,
Waumini wa KKKT, Wakristo Wote na Watanzania kwa Ujumla.Neema na Iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba na Bwana wetu Yesu Kristo, Amina.

Sisi maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), tumepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za matukio ya uchomaji wa makanisa katika eneo hili la Mbagala. Tumekuwa katika mkutano wetu wa Mwaka wa Lutheran Mission Cooperation (LMC) huko Moshi pamoja na vyama vyote vya Kimissioni vya Ulaya na Marekani. Tumelazimika kukatisha mkutano huo ili kufika hapa Mbagala. Tumekuja kwa madhumuni makubwa matatu:
Tumekuja kuwapa pole na kusimama pamoja nanyi katika uchungu mkubwa mlio nao. Machozi yenu ni machozi yetu. Machozi yetu ni machozi ya Kristo mwenyewe aliye Bwana wa kanisa linaloteswa. Jipeni moyo kwa kuwa yeye aliushinda ulimwengu (Yohana 16:33).
      Tumekuja kuonyesha majonzi yetu makubwa kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kuporomoka kwa umoja na mshikamano wa watanzania. Huu ni msiba mkubwa, na wenye msiba ni watanzania wote, wenye dini na wasio na dini.

Tumekuja kushiriki pamoja nanyi kupokea matumaini ya Tanzania mpya.
Katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa madhabahu ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa. Majivu haya na machozi yenu ni rutuba ya Tanzania mpya itakayojali upendo, uvumilivu, ustahimilivu, umoja, mshikamano, uhuru wa kuabudu na dola isiyo na dini.

Katika ujio huu wa maaskofu hapa Mbagala, hatukuja hapa kufanya haya yafuatayo:

      Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaokashifu dini za wenzao, wawe na ruhusa kutoka mamlaka zilizo juu au kama wanajituma wenyewe.

Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaodhalilisha misahafu ya dini; wawe wametumwa, kutegeshewa na mamlaka zozote au kwa misukumo ya utashi wao binafsi ili kupata kisingizo cha kugombanisha madhehebu ya dini.

       Hatukuja kuwahukumu hata kama hatukubaliani na wanaochoma makanisa na kuiba mali za makanisa kwa kisingizio cha kumtetea Mungu. Kisasi cha dhambi hiyo tunamwachia Mungu mwenyewe aliyedhihakiwa na walionajisi madhabahu yake.


Wapendwa wana KKKT na watukuka sana, wana na mabinti wa Tanzania ya Julius Kambarage Nyerere; kilichotokea Mbagala katika wiki ya kuadhimisha siku ya Baba wa Taifa, ni kebehi si kwa Baba wa Taifa bali ni kebehi kwetu sisi wenyewe tunaokalia kiti alichokalia Baba wa Taifa. Yeye amelala baada ya kazi njema. Apumzike kwa amani na tunu zake zifufuke katika majivu haya yaliyotokana na kuchomwa kwa amani na mshikamano wa Tanzania aliyoijenga.Kilichotokea Mbagala ni mateso ya kimbari, yaani mateso ya Kanisa (Persecution). Mateso haya ni matokeo ya mbegu ya magugu iliyopandwa katika bustani njema na sasa magugu hayo yanazaa matunda machungu. Dalili za mateso ya kimbari kama ilivyo kwa mateso ya kanisa; zilianza kitambo na hazikushughulikiwa na waliomrithi Baba wa Taifa. Dalili hizo ni kama hizi zifuatazo:

      Uchochezi wa wazi kuwa taifa hili linaendeshwa na unaoitwa “mfumo Kristo”, na kuwa Baba wa Taifa alaaniwe kwa yote aliyolitendea taifa hili.

Ubishi usio na tija juu ya idadi ya waumini wa dini mbalimbali hapa nchini na hata kudiriki kushawishi na kugomea zoezi la sensa ya watanzania. Lengo la ubishi huu ni mbegu inayoweza kuratibisha na kurasmisha mateso ya kimbari na mateso ya kanisa.

      Matumizi mabaya ya baadhi vyombo vya habari, vyenye lengo la kujenga hofu ya kudumu na migawanyiko ya kidini miongoni mwa watanzania

Ukimya wa vyombo vya dola juu ya vitendo vya uvunjaji wa sheria ya matumizi ya vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile, uvumilivu wa dola hauna maslahi mapana kwa mustakabali wa taifa letu na ni mateso ya kimbari, mateso kwa kanisa, na kwa wantanzania wote; wawe wengi dhidi ya wachache au wachache dhidi ya wengi.

      Madai yasiyo ya kawaida na ya mara kwa mara kwa serikali inayodaiwa kutokuwa na dini. Madai hayo ni kama:

 
      Kulazimisha uvaaji wa alama za kidini katika taasisi za umma ili kurahisisha na kuratibisha tofauti za watanzania. Tunajiuliza: Likitokea la Mbagala katika mashule yetu na vyuo vya umma, watachomwa wangapi na kuuawa wangapi?

Madai yanayojirudiarudia kutaka balozi za nchi fulani kufungwa hapa nchini. Madai haya yanaashiria kutaka balozi za nchi fulani tu ndiyo ziwe hapa nchini.


Madai na mashinikizo ya Uanzishwaji wa mahakama za kidini hapa nchini

  Mashinikizo ya kidini yanayoingilia mifumo ya kitaaluma na kisheria.
       Mashinikizo ya kidini juu ya mfumo wa uteuzi wa watendaji wa serikali na katika ofisi za umma,

      Kuhoji na kupotosha juu ya ushirikiano wa serikali na mashirika ya dini katika utoaji wa huduma za kijamii hususan afya na elimu hapa nchini


Wapendwa wana KKKT na Wapendwa watanzania wote. Hata kama wanaofanya mambo haya ya kusikitisha wametunukiwa hadhi ya kuitwa kuwa ni “wana harakati”, tofauti na wanaharakati wanaotambuliwa na watanzania walio wengi, tunawiwa kuonya kwa uvumilivu wote kuwa uana harakati wao usitumike kuvunja nchi na sheria za nchi. Tanzania yenye amani na mshikamano ni tunda la dini zote, makabila yote, itikadi zote za vyama, rangi zote na hali zote za kiuchumi. Hata wasio na dini wanachangia amani ya nchi hii.

Kwa macho na masikio yetu, tumeendelea kushuhudia vitendo vya uchomaji makanisa huko Zanzibar, Mwanza, Mdaula, Mto wa Mbu, Tunduru, Rufiji, Kigoma na sasa Mbagala. Wakati wote uvumilivu wa wakristo huenda umetafsiriwa kuwa ni unyonge na woga. Ikumbukwe kuwa hata wanyonge na waoga, hufika wakati wakasema “sasa basi” pale wanapodhalilishwa kupita kiasi. Hatuombei wakristo wafikishwe hapo.

Tumeshuhudia wizara zetu zikivamiwa mchana kweupe na kushinikiza kuachiwa kwa watuhumiwa wa uhalifu; tumeshuhudia vituo vya polisi vikichomwa moto; mahakama zikilazimishwa kufunga shughuli zake, misikiti ikitekwa, uhai wa viongozi wa dini ukitishiwa hadharani na viongozi wastaafu wakizabwa vibao hadharani kwa sababu ya zinazoitwa harakati za kidini. Tumefikia kuhoji, watu hawa wavamie nini ndipo hatua zichukuliwe? Wachome nini ndipo viongozi wenye dhamana ya kulinda mali na uhai washtuke? Wamwue nani ndipo iaminike kuwa watu hawa ni tishio kwa usalama wa taifa letu?

Sisi tulioitwa kwa njia ya nadhiri na viapo vitakatifu, tunawasihi sana waumini wa dini zetu na watanzania kwa ujumla, wenye wajibu wa kututii na wasiolazimika kututii, kuzingatia kuwa Mwenyezi Mungu analipenda taifa hili na watu wake. Kamwe hawezi kuliacha liangamie.

Kwa Wakristo wote, huu ni wakati wa kuendelea kufunga na kuomba kwa ajili ya amani ya taifa hili. Mkristo wa kweli ni yule aliye tayari kuteswa kwa ajili ya Kristo na kanisa. Wakristo hatuko tayari kuua, kutesa, kulipiza kisasi ili kumtetea Kristo. Mungu wetu hatetewi kwa kuua wengine na kuchoma madhabahu ya dini nyingine.

Katika mateso haya, kanisa litaimarika zaidi; na katika majivu haya ya Mbagala, Tanzania mpya itazaliwa na ukombozi wa kweli utapatikana. Tunawataka wakiristo wote kusamehe na kuendelea kuwa raia wema. Kushiriki kikamilifu katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa kupitia njia sahihi zilizowekwa. Wakati wengine wanaweka mikakati ya kuchoma madhabahu, wakiristo tuweke mikakati ya kuomba na kushiriki vema katika haki zetu za uraia. Pamoja na kuwa wapole kama njiwa, imetupasa pia kuwa na busara kama nyoka (Mathayo 10:16).

Daima tukumbuke kuwa, “KUSHINDANA KWETU SISI SI JUU YA DAMU NA NYAMA BALI NI JUU YA FALME NA MAMLAKA, JUU YA WAKUU WA GIZA HILI, JUU YA MAJESHI YA PEPO WABAYA KATIKA ULIMWENGU WA ROHO” (Waefeso 6: 12).Ni sisi Maaskofu wenu kwa Neema ya Mungu,

     Askofu Dr. Alex G. Malasusa – Mkuu, KKKT na D/Mashariki na Pwani

     Askofu Dr. Stephen Munga –Mkuu, D/Kaskazini Mashariki
     Askofu Dr. Martin Shao – Mkuu, D/Kaskazini

     Askofu Dr. Thomas Laizer – Mkuu- D/Kaskazini Kati

     Askofu Dr. Benson Bagonza- Mkuu, D/Karagwe

     Askofu Isaya J. Mengele – Mkuu, D/Kusini

    Askofu Levis Sanga – Mkuu- D/Kusini Kati

   Askofu Elisa Buberwa – Mkuu –D/Kaskazini Magharibi

   Askofu Andrew Gulle – Mkuu, D/Mashariki ya Ziwa Victoria

   Askofu Michael Adam –Mkuu, D/Mkoani Mara

   Askofu Renard Mtenji – Mkuu, D/Ulanga-Kilombero

   Askofu Dr. Israel-Peter Mwakyolile – Mkuu, D/Konde

   Askofu Job Mbwilo – Mkuu, D/Kusini Magharibi
   
  Askofu Dr. Owdenburg Mdegella- Mkuu, D/Iringa

   Askofu Jacob Ole Mameo- Mkuu, D/Morogoro

   Askofu Zebedayo Daudi – Mkuu, D/Mbulu

   Askofu Paulo Akyoo – Mkuu, D/Meru

   Askofu Charles Mjema – Mkuu, D/Pare

   Askofu Mteule Amon Kinyunyu- Mkuu, D/Dodoma

   Askofu Mteule Dr. Alex Mkumbo- Mkuu, D/Kati


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Alhamisi, 18 Oktoba 2012

VURUGU ZAZUKA KUTOKANA NA KUKAMATWA KWA PONDA NA KIONGOZI WA UAMSHO ZNZ


 

POLISI mkoani Dar es Salaam na wale wa Kisiwani Zanzibar, jana walitumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha kusambaratisha makundi ya watu wanaodaiwa kuwa waumini wa Dini ya Kiislamu, waliopanga maandamano kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao.

Kisiwani Zanzibar vurugu kubwa ziliibuka baada ya kusambaa taarifa kuwa Kiongozi wa Kundi la Uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed alitekwa nyara juzi saa 3 usiku akiwa kwenye gari lake na dereva wake.

Vurugu hizo zilisababisha uharibifu wa mali kadhaa ikiwamo Maskani Kaka ya Kisonge inayomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambayo ilichomwa moto na waandamanaji.


Waandamanaji hao pia walichoma moto baa za Darajani na Mbawala eneo la Mikunguni na baadhi ya nyumba za kulala wageni, kabla Vikosi vya Kutuliza Ghasia (FFU) na Kikosi cha Zima Moto kudhibiti vurugu hizo kwa mabomu ya kutoa machozi.

Pia magari kadhaa yalichomwa moto na kuharibiwa vibaya yakiwa yameegeshwa katika maeneo mbalimbali, huku mipira na matairi vikichomwa katika barabara kadhaa.

Katika maeneo ya Mjini baadhi ya njia zilifungwa na watu waliokuwa wakitoka kazini walishindwa kwenda nyumbani. Maeneo yaliyoathirika zaidi ni yale ya Malindi, Darajani hadi Michenzani ambako njia zilifungwa na mabomu yalisikika yakipigwa mfululizo.

Katibu wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), Sheik Abdallah Said alisema,
“Taarifa tulizonazo ni kwamba Sheikh Farid ametoweka katika mazingira ya kutatanisha…Alitoka kwake Mbuyuni katika gari yeye na kijana wake wa hapo nyumbani, lakini baadaye kuna gari ikamfuata na kusimama na ndipo alipoingia katika hilo gari jingine na hakuonekana tena. Hatujui ni kina nani waliomchukua na hatujui ilikuwaje akaingia katika hilo gari ...”

Polisi waliimarisha ulinzi katika baadhi ya maeneo hasa Msikiti wa Mbuyuni ambao uko jirani na makazi ya Sheikh Farid. Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema polisi halihusiki na kukamatwa kwa Farid, lakini wao wanaamini kwamba ‘amejipoteza’ mwenyewe na kujificha.

Kamishna Mussa alisema polisi watawasaka wote waliosababisha vurugu hizo, na kwamba hadi sasa hawafahamu chanzo chake bado.

“Tunafanya uchunguzi zaidi kujua chanzo cha fujo hizo ingawa mimi sijui habari za kutekwa Farid, sasa tunasema tunachunguza chanzo cha vurugu hizo na tukishapata uthibitisho na waliosababisha tutawafikisha mahakamani kujibu mashtaka,” alisema kamishna huyo.

Ilivyokuwa Zanzibar
Vurugu hizo zilianza katika maeneo mbalimbali muda mfupi baada ya vijana kadhaa kukusanyika katika eneo la Darajani kando ya Soko Kuu majira ya asubuhi, kutokana na kuzagaa kwa taarifa kwamba Sheikh Farid alikuwa haonekani.

Idadi ya vijana hao ilikuwa ikiongezeka kadiri muda ulivyosonga, huku wengi wao wakiwa na silaha za aina mbalimbali zikiwamo magongo na mawe, hali iliyoibua hofu kwa wafanyabiashara wa eneo hilo, hivyo baadhi yao waliamua kufunga maduka.

Maeneo yalioharibiwa ni pamoja na baadhi ya nyumba za kulala wageni ambazo zimechomwa moto katika eneo la Amani, huku baadhi ya vijana wakionekana wakikimbia na kreti za pombe.

Katika eneo la Darajani, vijana kadhaa wakishirikiana na Wamachinga, walionekana wakivunja kisha kuingia katika moja ya maghala ya kuhifadhia bia, ambako walipora bidhaa zote zikiwamo kreti kadhaa za bia zilizokuwa zimehifadhiwa humo.

Baadhi ya wenye maduka walifunga na kutoweka, lakini waporaji waliiba baadhi ya bidhaa vikiwamo vyakula, kisha  kutokomea navyo kusikojulikana.

Katika maeneo ya Ng’ambo ambayo ni Amani, Mikunguni, Kwerekwe na Daraja Bovu vijana walioonekana kuwa na hamasa, waliingia kwenye makazi ya watu na kuiba vitu kadhaa, na kila mabomu yalipopigwa walikimbilia vichochoroni na baada ya muda walirejea tena.

Maeneo ya Malindi, Michenzani na  Rahaleo, kulikuwa na vurugu za urushaji mawe na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu katika maeneo hayo.

Matawi ya miti ilikatwa na kuunganishwa na magari mabovu kuwekwa barabarani kisha kuchomwa moto. Hali hiyo ilisabababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya barabara, na katika fujo hizo baadhi ya vijana walikamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohammed alithibitisha kutokea kwa fujo hizo na kusema Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo chake na taarifa kamili zitatolewa baada ya kukamilika uchunguzi huo.

Ponda Dar
Jijini Dar es Salaam, baadhi ya watu walipanga kufanya maandamano hadi Makao Makuu ya Polisi, kupinga kukamatwa kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa juzi usiku na kushikiliwa kutwa nzima ya jana katika Kituo Kikuu cha Polisi.

Ponda alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuchochea vurugu na uvunjifu wa amani jijini Dar es Salaam, na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisisitiza kuwa polisi wamechoka kuvumilia harakati zake za kutaka “nchi isitawalike”.

“Kuanzia leo uvumilivu kwa Jeshi la Polisi dhidi ya watu wasiofuata sheria za nchi umekwisha. Kwa kuwa Ponda ni mtu anayepotosha watu waliopo chini yake wanaotaka kuandamana bila utaratibu wasitulaumu kwa lolote lile litakalotokea,” alisema Kova.

Kova alisema hadi jana Ponda alikuwa bado anahojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Mkoa wa Dar es Salaam na kwamba ushahidi ukijitosheleza, atafikishwa mahakamani wakati wowote.

Alisema taasisi anayoingoza Sheikh Ponda haijasajiliwa kwa mujibu wa sheria kufanya shughuli za dini. Hivyo basi shughuli zote zinazoendesha na taasisi hiyo si halali.

"Natoa wito pia kwa wafuasi wa kiongozi huyo, walioshiriki katika vurugu mbalimbali za hivi karibuni, wajisalimishe haraka kwa kuwa sasa tupo katika mchakato wa kuwasaka, kuwakamata na baadaye kuwafikisha mbele ya sheria," alisema.

Tuhuma za Ponda
Kamanda Kova alidai kuwa Sheikh Ponda amekuwa akichochea vurugu na kuwashawishi wafuasi wake kuidharau Serikali na vyombo vya usalama.

“Ponda amekuwa ni mtu ambaye amefanya nchi hii, hasa katika Jiji la Dar es Salaam kukaa katika hali ya wasiwasi. Ijumaa imekuwa siku ya fujo badala ya kuwa siku ya amani,” alisema Kova.

Alisema vurugu hizo zinazoongozwa na Sheikh Ponda zimekuwa zikisababisha baadhi ya watu kushindwa kwenda kazini siku za Ijumaa na hali hiyo haivumiliki tena.

Kamanda Kova alitaja tuhuma nyingine dhidi ya Sheikh Ponda kuwa ni kuongoza kundi la watu kwenda kuvamia kiwanja namba 311/3/4 eneo la Chang’ombe ambacho kinamilikiwa  na kampuni Agritanza.

"Kiwanja alichokwenda kukivamia kilikuwa mali ya Baraza Kuu la Waislamu nchini (Bakwata) na kiliuzwa kihalali kwa kampuni hiyo," alisena.

Alitaja tuhuma nyingine kuwa ni kufanya maandamano kinyume cha sheria, ikiwamo kuweka kambi Makao Makuu ya Polisi bila kibali cha jeshi hilo wiki kadhaa zilizopita.

Kamanda huyo alisema Ponda anashikiliwa pia kwa kuwa mstari wa mbele kupambana na vyombo vya dola  na Serikali, ikiwa ni pamoja na kushawishi wafuasi wake kumdharau Rais wa nchi.

“Vilevile amekuwa akiendesha maandamano na kukusanyika Kiwanja cha Kidongo Chekundu, huku wakijitapa kuwa wana nguvu zaidi ya Jeshi la Polisi,” alieleza Kova.

Polisi pia wanamtuhumu Ponda kwa kuanzisha vurugu na vitisho dhidi ya Sheikh Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Mufti Shaaban Bin Simba na kutaka kumtoa madarakani kwa nguvu pamoja na kutaka kuvamia ofisi yake.

Alikamatwaje?
Kamanda Kova alisema Ponda alikamatwa na askari waliomuwekea mtego kutokana na yeye kuwa bingwa wa kutoroka kila akifanya matukio.

“Askari waliowekwa maalumu kwa ajili ya kumkamata walifanikiwa kumtia nguvuni saa 4:00 usiku karibu na eneo la maficho yake ambako alipelekwa na pikipiki,” alisema Kova.

“Hivi Ponda ni nani mpaka awe na uwezo wa kumpa Rais aliyechaguliwa na wananchi siku saba kuwaachia watu waliopo mahakamani yeye amechaguliwa na nani kuongoza taasisi aliyonayo na anatoa wapi nguvu za kufanya mambo yote hayo?,” alihoji Kova.

Alisema kulingana na matukio anayoyaongoza Ponda, wananchi wameanza kuona kama anaogopwa na vyombo vya dola, jambo ambalo siyo kweli.

Aliongeza kuwa polisi wana uwezo wa kumdhibiti, isipokuwa walikuwa wanatumia busara tangu alipoanza vurugu na kwa sasa uvumilivu umewashinda, hivyo wataanza kumshughulikia.

Vurugu zazuka
Kukamatwa kwa Sheikh Ponda kulizua vurugu jijini Dar es Salaam na kufanya baadhi ya wakazi wake hasa maeneo ya Mnazi Mmoja na Kariakoo, kuingiwa kiwewe baada ya polisi kutumia mabomu ya machozi na maji ya kuwasha ili kuwasambaratisha watu waliokuwa wanataka kuandamana kwa lengo la kushinikiza kiongozi huyo aachiwe.

Hali hiyo ilisababisha watu kukimbia ovyo katikati ya iji na kuongezeka kwa misongamano ya magari, jambo lililofanya usafiri wa daladala kuwa mgumu kwenda na kutoka katikati ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam.

Baadhi ya wafanyabiashara walifunga maduka yao wakihofia kuporwa mali wakati wa vurugu hizo, baada ya vibaka kujichanganya wakijaribu kufanya uhalifu huo.

Katika eneo la Mnazi Mmoja, polisi walirusha maji ya kuwasha kusambaratisha kundi la watu hao, huku wengine wakiwa wanadhibitiwa walipokuwa wakienda Makao Makuu ya Polisi ili kumtoa kiongozi huyo.

Baadhi ya mashuhuda walisema, mbali na Ponda watu hao walikuwa wanataka kwenda polisi kuwatoa watu waliokuwa wanashikiliwa kituoni hapo kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuharibu makanisa katika Kata ya Mbagala wilayani Temeke.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Jumatano, 17 Oktoba 2012

 Karibu kwenye tamasha katika kanisa la TAG magomeni ambalolitaambatana na uzinduzi wa Blog mpya ya Come and see gospel art promoters.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Jumatatu, 15 Oktoba 2012

TAMKO LA ASKOFU MKUU WA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, DK. BARNABAS MTOKAMBALI, KUHUSU MATUKIO YA UCHOMAJI WA MAKANISA MBAGALA DAR ES SALAAM.



Oktoba 12 mwaka huu, matukio mabaya na yenye kutia doa sifa ya amani umoja na Utengemano wa Taifa la Tanzania, yalijitokeza huko Mbagala Jijini Dar es Salaam, wakati watu wenye jazba wanaoaminika kuwa ni Waislamu wenye msimamo mkali walipovamia makanisa saba ...na kuyachoma moto eti kwa kulipiza kisasi cha mtoto aliyekojolea kuran katika utani wa kitoto.
Askofu mkuu wa TAG Dr Barnabas Mtokambali

Katika mkasa huo ambao ni kama muendelezo wa ghasia zingine zilizotokea kule Zanzibar miezi michache iliyopita na kuteketeza makanisa mbalimbali mbali na kuharibu mali za kanisa na zile za watu binafsi.

Tukio la Mbagala limesababisha makanisa saba kuharibiwa vibaya, mali kuibiwa na hata kuhatarisha maisha ya watanzania na kuwafanya waishi kwa hofu na kupoteza matumaini. 

CHANZO CHA TUKIO
Kwa mujibu wa walioshuhudia, Polisi na wahusika (Waislamu) chanzo cha ghasia hizo na mabishano ya kitoto baina ya watoto wa dini ya Kiislamu na kikristo, waliobishana kuwa ikiwa mtu atakojolea kuran na kuitemea mate atageuka mbuzi au nyoka.

Lakini baada ya tukio hilo la kitoto watu walilikuza na kulipeleka kwenye misikiti na hivyo kuchocheza ghasia. Kimsingi tukio lenyewe ni jepesi sana ukilinganisha na matokeo yake. Ukweli kwamba waliofanya utani huo ni watoto na chanzo chake ni mabishano ya kitoto, unatia shaka kuwa huenda kuna hoja nyuma ya pazia ambayo isipotazamwa kwa makini inaweza kulete matokeo mabaya sana.
Jambo linalonitia shaka ni kufanana kwa matukio ya kuchomwa moto kwa makanisa ya Zanziabar na ya Mbagala ambapo hakukuwa na uhusiano wa vyanzo vya ghasia na makanisa husika.

Mfano; Ghasia za Zanzibar zilizopelekea kuangamizwa kwa makanisa zinaelezwa kuwa zilitokana na kikundi cha Kiislamu cha Uamsho wa Mihadhara, kilichokuwa kikiandamana kudai mjadala wa Muungano, lakini zikaishia kwenye uchomaji wa makanisa, hapa hauonekani uhusiano wa kanisa na Muungano; nalazimika kujiuliza kulikoni?
Vivyo hivyo tukio la Mbagala halina uhusiano wa moja kwa moja na kanisa kwa kuwa hakuna ushahidi wala hata tetesi kuwa mtoto huyo alitumwa na kanisa lolote. Wahusika wa dini ya Kiislamu akiwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, analielezea tukio la kitoto kama lisilostahili hata mtu kufunguliwa mashtaka bali kuelekezwa tu. Ni vipi lisababishe uchomaji wa makanisa?

MAKANISA YALIYOCHOMWA MOTO
Katika ghasia hizo za aina yake, makanisa saba yamethibitishwa kuharibiwa kwa kuchomwa moto, kupasuliwa vioo, viti na kuibiwa vyombo vya muziki na jenereta. Makanisa hayo ni TAG Kizuiani, Agape, Kibonde maji, SDA Sabato, Mbagala Kizuiani, Katoliki Kristo Mfalme Mbagala Rangi Tatu, Anglican Mbagala Kizuiani, KKKT, Mbagala Zakhem na TAG, Shimo la Mchanga.

Pamoja na majengo hayo kubomolewa kwa viwango tofauti mengine yakichomwa moto, pia wahusika waliiba Genereta, na vyombo vya muziki vya makanisa hayo na kuvunja magari na baadhi yao kuchomwa moto.

Choko choko zilizinazoweza kuwa cahanzo cha matukio hayo ni:
Januari sita mwaka huu, kikundi kimoja kinachoitwa JUAKITA, kiliitisha kongamano la kujadili katiba mpya Tanzania, kwa upande wa Waislamu. Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam kulitolewas kauli za kichozi kama:
1. Lazima Rais ajaye atoke Zanzibar
2. Kukabiliana na ukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3. Kupinga Muungano ili kuupa nguvu Uislamu
4. Kupigana kufa na kupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.
Kauli hizo zilitolewa na Sheikh Nasoro Mohamed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadaye zikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.

Uchunguzi unaonesha kuwa uchochezi huu umekuwa ukiwaandaa watu kusubiri vijitukio vidogo tu ili kulipua ghasi. Tuliona jinsi makanisa yalivyochomwa kule Zanzibar. kwa kuwakumbusha tu makanisan yaliyoangamizwa katika tukio hilo ni: EAGT, Elimu Pentecost na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT.

Ni jambo la kusikitisha kuwa matukio haya yanatokea siku mbili tu kabla ya maadhimisho ya miaka 13, ya kifo cha Rais wa Kwanza, Mwl. Julius kambarege Nyerere. Leo hotuba na midahalo inarindima kila mahali kumuenzi Nyerere, lakini wengi wetu tukiwa tumejaa majozi baada ya nyumba zetu za ibada kuharibiwa katika matukio yanayoashiri hatari kubwa.
Hofu yangu ni kuwa, roho hii ya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere aliifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa ya Afrika kama ifuatavyo:

1. Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianza kwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaa yakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambano yasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo 500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.

2. Roho hii imekuwa ikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa la Mali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.

3. Itakumbukwa kuwa miezi michache tu ilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibuka nchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutaka eneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.

4. Katika tukio hilo inasemekana mtoto huyo alitengenezewa mabishano ya kitoto kuwa akichoma kurani atakuwa chizi naye akabisha
kisha akapewa kiberiti na kurani akachoma tena walioandaa
mzaha huo wakamkamata na kumpeleka mahakamani.
Tukio linalofanana na hilo lilitokea tena Bagamoyo mkoani Pwani
ambapo mtoto wa kike alishtakiwa na hata kuhukumiwa kifungo
kwa madai ya kuchoma kuran lakini tukio lilikuwa katika mabishano
ya midhaha ya kitoto

WITO WANGU
Natoa wito kwa Wakristo wote nchini kujiepusha na mizaha
inayoweza kutengeneza sababu za kulipuka kwa ghasi na kutengeneza
mwanya wa watu wenye nia mbaya kutekeleza agenda zao zaria Ili
kulinda amani umoja na utengemano wetu, nawasihi viongozi wa makanisa
kuonya na kukemea waumini na watoto wetu wasishiriki kwa namna yoyote ile mizaha inayopelekea kuchoma au kuharibu vitabu au nyaraka
za kidini.

Nawasihi watanzania wote kwa ujula kujiepusha na mizaha ya kidini inayoweza kuchafua amani yetu, na pale jambo lolote lenye kukera linapotokea tujiepushe kuwa mawakala wa shetani wa kueneza chuki badala ya amani na upendo.

USHAURI WANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI
Nawashauri viongozi wa Serikali ambao leo wanatoa matamko na kushiriki midahalo ya kumuenzi Mwl. Nyerere kukumbuka kuwa huyo alikuwa na mapenzi makubwa na amani na umoja wa taifa. Kwa hiyo kumuenzi kwa vitendo ni kudumisha utawala bora, unaofuata sheria usio na chembe ya ubaguzi wa aina yoyote.

Kulipuka majukwaani kumuenzi Nyerere bila kuilinda na kuitetea amani ya nchi ni kujidanganya.

Ni wajibu wa kila Mtanzania kutii sheria na mamlaka kwa kuwa zimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi. Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.

Viongozi wenzangu wa dini wakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo ni vyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu za kidini na uvunjaji wa amani.

Pia ningependa kuwashauri viongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepuka kauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewi haki.

Ni vema ieleweke kuwa matukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa haraka yanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwa wananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busara inatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta. 

Ni vyema wenye dhamana ya kuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusu kuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.
Ni vyema viongozi wa Serikali wakajizuia kufanya maamuzi yanayoashiria upendeleo kwa baadhi ya makundi ya kidini na kukiuka utawala wa sheria, mfano; kutii waandamanaji na kuwaachia bila mashrti watu waliokamatwa kwa mujibu wa sheria kuna jenga kiburi kwa makundi yenye kiu ya matumizi ya nguvu na kujenga hofu kwa pande zingine.
Ni vyema mamlaka zikasiamama katika sheria na kufanya hukumu kulingana sheria badala ya kuamua mambo ya kisheria kisiasa.

WITO MAALUMU KWA VIONGOZI WA DINI
Nitumie nafasi hii kuwasihi vingozi wenzangu wa dini, kusimama imara katika kuombea taifa na kuhubiri kwa nguvu ili kukabiliana na giza la kiroho ambalo linatishia kuifunika nchi.
Takwimu za karibuni kabisa za utafiti uliofanywa na taasisi ya Washnton DC iitwayo, Pew Research Centre, na kurushwa na Televisheni ya CNN, Katika kipindi chake cha Inside Africa, zilionesha kuwa watanzania asilimia 93, wanaamini mambo ya ushirikina na uchawi wakati Uganda ni asilimia 29 na Kenya ni asilimia 27. Tu. Mahali ambapo giza la kiroho limezingira kiasi hiki ni lazima matukio ya kishetani yashamiri tuchukue hatua.

Mwisho, natoa wito kwa watanzania wenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tuikimbie dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusu itatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikao vya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.
Imetolewa leo 14/10/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG

 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela