Ijumaa, 25 Mei 2012

MAANDALIZI YA MKUTANO MKUBWA WA INJILI JANGWANI YANAENDELEA

Zikiwa zimebaki week chache kufika kwenye mkutano mkubwa wa injili utakao fanyika katika viwanja vya Jangwani. timu ya wahudumu wapatao 190 wako kwenye maandalizi ya kusafiri kutoka Swedeni kuja hapa Tanzania kwaajili ya kuhudumia mkutano huo. wahudumu hao wamejianda kuhubiri injili ya Yesu kwa watu wengi zaidi kadri watakavyoweza kuzunguka mitaani na kwenye uwanja wa jangwani, kuombea wagonjwa, Kukemea pepo na kutarajia miujiza mingi kufanyika kwa nguvu za jina la Yesu.
Tangazo la mkutano utakao hubiriwa na Mwinj. Johannes Amritzer wa SOS MISSION

Mkutno huo uliopewa jina la sherehe za ishara na miujiza utafanyika katika viwanja vya jangwani vilivyoko katikati ya jiji hili la Dar kuanzia tar 13-17 June. sambamba na mkutano huo kutafanyika semina ya wachungaji na viongozi wa makanisa wasiopungua 2000 semina hiyo imepewa jina la Mpenyo wa kinabii (Apostolic Breakthrough) na kuna maandalizi mengi sana ambayo yamesha fanyika ili kufanikisha mkutano huo. blog hii iliandika habari hizi hapo awali fuata link hii. http://martmalecela.blogspot.com/2012/05/baada-kufanya-vizuri-mwaka-jana-kwenye.html
Uwanja wa Jangwani utakapo fanyika Mkutano
watu wote tunaombwa kuombea mkutano huo ili nguvu za Mungu zikaonekane dhahili kwa watu kufunguliwa kutoka katika ngome za shetani na uwepo wa Roho mtakatifu ukafunike na watu wabatizwe kwa moto na kwa roho mtakatifu
habari hii inatoka sos blog
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni