Jumatano, 23 Mei 2012

SIKU ZA MWISHO!!,MAARIFA YATAONGEZEKA. WANASAYANSI WATENGENEZA KIFAA CHA KUDHIBITI NDOTO. UNAWEZA KUCHAGUA NDOTO ZA KUOTA!!.

Kwenye kitabu cha Biblia kinasesema kuwa siku za mwisho maarifa yataongezeka, na katika kutimizwa kwa unabii huo tunaona vitu mbalimbali vikitengenezwa kila siku ambavyo vinastajabisha na kushangaza. katika kutafuta jitihada za kupinga au kudhibiti uotaji wa ndoto mbaya vijana wawili huko Marekani walio na shahada ya sayansi ya kompyuta wametengeneza kifaa kinachoweza kudhibiti ndoto unazoota. kifaa hicho kinachovaliwa kwenye macho kama miwani wakati wa kulala kinaweza kukuwezesha kuchagua au kurudia ndoto unazoziota.

Vijana Duncan na Steve waliotengeneza kifaa cha kudhibiti ndoto
Kifaa hicho kilichopewa jina la mjongeo wa haraka wa jicho (REM) kitamwezesha mtu kuota ndoto nyepesi nyepesi zenye kureta raha kama vile kuendesha ndege, kuna chakula na Rais n.k. Uvumbuzi huo wa kipekee umefanywa na vijana wawili Duncan Frazier na Steve Mcguigan wote wenye umri wa miaka 30, ambao wana miliki kampuni ya Bitbanger Lab iliyoko New York, Marekanio.

ikiwa ni wiki moja sasa tangu kifaa hicho kianze kuvuliwa na kutumika watu zaidi ya 6,550 wameahidi kufadhili mradi huo. kifaa hicho kimewekwa taa nyekundu sita ambazo hazina mwanga mkalr wa kuweza kumwamsha mlalaji lakini ni rahisi kwa ubongo kuzisajili. hatua za kulala kugawaywa katika mikondo miwili ipo yenye mjongeo wa haraka na isiyo na mjongeo wa haraka, kwa kawaida mlalaji huenda mbele na kurudi nyuma wakati wa usiku katika hatua hizi ambazo ndoto nyingi hutukia na hudumu kwa muda mrefu hadi asubuhi.

Kifaa hicho kwa ndani.
kifaa hiki huweza kugundua hatua hii ya ndoto ndefu na na kuingia katikati ya mfumo wa ndoto. kifaa husubiri kwa muda wa saa nne hadi tano hadi mtumiaji azame katika usingizi mzito na kisha taa nyekundu huwaka. hapo kifaa cha REM huanza kufanya kazi. kwa kuwa mwongozo wa kifaa uko katika mpangilio basi kifaa kitakupa taarifa kuwa upo ndotoni. baada ya kugundua kuwa unaota, unaweza kuchagua kipi kinachofuata kama unataka kwenda marekani au kupanda safu za milima ya evarest. hivyo basi unachotakiwa ni kusubiri kifaa kikutambulishe kuwa ndoto zimeanza na wewe utapangilia ubongo wako nini cha kuota.

Vilele wavumbuzi wameweka mtandao ambo mtu anaweza kupanga ni wakati gani wa kuanza kuota au kuirudia ndoto yako. kuhusu usalama wavuumbuzi hao wamesema mpaka sasa hawajapata malalamiko yoyote ya mtu aliyeathilika kiafya kutokana na kifaa hicho.

Kifaa ninafichwa kwenye kitu kama miwani ili kuweza kuvaliwa machoni

Bidha ikiwa tayari kwa matumizi




http://www.dailymail.co.uk/news/article-2147181/Dream-come-true-Two-mad-scientists-create-sleep-mask-lets-people-CONTROL-dreams.html#ixzz1vbA9aG6v
http://www.facebook.com/SleepWithRemee

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: