Jumatano, 16 Mei 2012

BAADA KUFANYA VIZURI MWAKA JANA KWENYE CAMPAS NIGHT SOS MISSION INTERNATIONAL WAANDA MKUTANO MKUBWA WA INJILI DAR

SOS Mission walikuwepo mwaka jana kwenye tamasha kubwa la aina yake la Campas Night lililokuwa na timu kubwa, wakiongozwa na kiongozi wao Past Johnnes mwaka huu wanakuja na mkutano mkubwa wa injili utakao fanyika hapa Dar kuanzia Tar 13-17 Juni mkutano huo umepewa jina la sherehe za ishara na miujiza. maanadalizi ya mkutano huo yanaendelea kwa kasi kwa kuandaa watenda kazi wengi. Timu ya maombi tayari wanaendelea na maombi katika kanisa la mito ya baraka pale Jangwani kila wiki, wachungaji na wahudumu wengine nao wanaendelea kuandaliwa ili kuhakikisha kuwa kila idara inakaa vizuri katika eneo lao.
Mch Johnnes akihubiri kwenye Campas Night mwaka jana
wana  SOS watakaokuja Dar wanakadiliwa kuwa 200 hivi na watafanya uinjilisti mitaani kwa kutumia magari na helkopta kwa kutua kwenye viwanja vya wazi na kuweza kufanya ushuhudiaji hivyo wanaobwa vijana waliookoka wanaoweza kutafsili kingeleza kuja kiswahili kujitokeza ili kuzunguka na timu hiyo na wengine watakuwa kwenye helkopta(haya ambao hamjawahi kupanda helkopta changamkia tenda hii) zaidi ya hapo wakati wa mkutano mtu atakayeleta watu 20 atapewa zawadi na watu hao watalipiwa nauli, na mchungaji atakayeleta watu 20 yeye atapewa zawadi ya vyombo vya mziki kwaajili ya huduma. hivyo jiandae kuleta watu uwezavyo ili ujinyakulie zawadi. na si hivyo tu wachungaji watapata kusaidiwa kielimu pia.

Mhubiri wa mkutano huo Mch Johnnes akiwa na mkewe.
ikiachilia uinjilisti utakao fanywa SOS band watakuwepo kutumbuiza siku zote za mkutano na waimbaji wengine wa hapa kwetu Tanzania watakuwepo kama Kinondoni Revival, Temeke Revival, the Repers ,Upendo Nkone, Christina Shusho, Bony Mwaitege na wengineo. wapendwa tunaobwa kuja na watu wasiookoka, wagonjwa na wenye matatizo mbalimbali ili wakutane na Mungu wao na kupokea miujiza yao na kama unataka kuwa mhudumu utawasiliana na no hapo chini.

kama unataka kuwasiliana na waandalizi wa mkutano huo waliopo hapa Dar no za simu ni
+255 714 503 638 au +255 762 441 719 au E-mail signsndwondersfestival_dar@vcc.or.tz

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela

Hakuna maoni: