Jumamosi, 26 Mei 2012

MWISHO WA DUNIA!!! KANISA MOJA HUKO MAREKANI LAWAPIGA CHAPA YA 666 WAUMINI WAKE!! MCHUNGAJI WAO AJIITA YEYE NI MPINGA KRISTO!!!

Mchungaji mmoja wa kifilipino anayeishi Marekani, ameafundisha waumini wake imani potofu na kuwapiga chapa ya 666 au SSS yaani six, kwa kusema mtu yeyote anatakiwa kuwekwa alama hiyo maana ni no yenye hekima kutokana na kifungu cha Ufunuo 13:18, upotofu huo unaenea kwa kasi sana huko bara la amerika zaidi ya nchi 25 sasa yamefunguliwa matawi ya kanisa hilo. mtu huyo ambaye anaitwa Jose Luis De Jesus Miranda, yeye amejitangaza hadharani kuwa mpinga kristo na mwisho wa Dunia utakuwa Juni 30 kwaka huu 2012. makundi mengi ya waumini wake wamepigwa chapa hizo kwenye mikono yao na wengine kwenye paji la uso, kiongozo huyo ambaye kanisa lake hilo lilianza mwaka 2007, kwa sasa amekuwa na wafuasi wengi ambao nao wanapita mitaani na mabango yenye no 666 na kuwashawishi wengine wakubali kupigwa chapa ya 666 na kusema ni namba ya hekima nna kila anyepigwa chapa hiyo anakuwa mwenye hekima.

Mtu anayejiita kuwa ni mpinga kristo Jose Luis De Jesus Miranda

Habari za mtu huyu ambazo nyingi zimezagaa katika vyombo vya habari huko bara la amerika zinasema kuwa alipohojiwa na kituo cha CNN alisema kuwa roho iliyoko ndani yake ni sawa na ile iliyokuwa ndani ya Yesu na hata yeye anatembelewa na malaika na manabii waliongelea habari zake na watu wamemsubiri kwa miaka 2000 na sasa amesha kuwepo. aliongeza kuwa watu wasimwogope hata kama bado hawajawekwa alama ya 666. akisisitiza kuizungumzia hiyo no 666 amesema vitu vingi huambatana na no hiyo, Dunia hujichungusha kwa speed ya 66.666 mph. nabii zote lazima zitimie mwaka huu 2012. kule Puerto Rican-alikozaliwa Jose Luis De Jesus (Latitude yake ni  66.6°)"
na katika birthday aliyoifanya ya kutimiza miaka 66 watu wengi waliohudhulia walikuwa na no 666 na hadi keki ilipambwa hivyo.

Keki yenye no 666 iliyotumika katika Birthday yake
kiongozi huyo mwenye kanisa linaloitwa Grace International Ministry kuanzia tar 01/ wezi huu wa May wameweka mabango makubwa mengi yenye kutangaza habari hizo.

Alama za 666 kwenye mikono
Maskini mtoto yeye haelewi kinachoendelea alama ya SSS yaani Six
Mikono yenye alama
Add caption
Mabango ya mpinga kristo yakiwa katika mitaa mbali mbali huko bara la Amerika
Mchungaji huyo ambaye anapotosha ukweli kwa kutumia Biblia anasema kuwa hakuna dhambi duniani kwa sasa maana Yesu alikufa na watu wote wakafanyika kuwa na haki Warumi 5:19(hakuna dhambi duniani) pili anasema kuwa hakuna shetani tena Duniani maana alikamatwa na kufugwa Ufunuo 12:13 na tatu anasema no 666 ni no ya hekima na wenye kuwa nayo wanakuwa ni watu wenye hekima ufunuo 13:16-18 kwa sasa wanatumia gharama kubwa kuanda vipindi ya TV na matangazo mtaa kwa mtaa wakisema kuwa siku ya kubadilisha imekaribia yaani mwisho wa Dunia tar 30/06/2012

Biblia katika kitabu cha Mathayo sura ya 24:5 kinazungumzia jinsi wanafunzi walivyomuuliza Yesu  kwa habari ya kurudi kwa na yeye mwenyewe Yesu alisema. angalieni mtu asiwadanganye, wengi watakuja kwa jina langu, wakisema mimi ni kristo nao watawadanganya wengi. hivyo wapendwa wakati tulio nao ni wa kila mtu kushika alicho nacho tazama mwovu asikunyang'anye na kama bado hujampokea Yesu kuwa Bwana wa maisha yako ni wakati wa kukata shauri sasa ili uwe na uhakika wa kwenda mbinguni.

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Chapisha Maoni