Jumatatu, 28 Mei 2012

KWETU PAZURI (Ambassadors of Christ SDA) YA KIGALI RWANDA KUTUA DAR

Kwaya ya kwetu pazuri, Ambassadors of Christ SDA ya nchini Rwanda inatarajiwa kufanya ziara ya kihuduma hapa nchini, habari zilizoifikia blog hii zina sema kuwa wanakuja kuhudumu katika mkutano wa injili unaoandaliwa na kanisa la SDA hapa Dar, mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika viwanja vya Biafra utaanza tar 2 - 16 june, kila siku kuanzia 10:00 Jioni. kwaya hiyo ambayo imejizolea umaarufu  mkubwa katika nchi za Afrika Mashriki katika miaka ya hivi karibuni, ikumbukwe kuwa mwezi uliopita walikuwa katika Nchi ya Kenya kwa ziara ya kihuduma katika nchi hiyo.

Kwaya ya kwetu pazuri ya Rwanda


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: