Ijumaa, 18 Mei 2012

MWALIMU WA KWETU PAZURI AWAASA WAIMBAJI WA INJILI

Waimbaji wa Muziki wa injili, wametakiwa kutokuimba kwa sifa, bali kuhakikisha wanaifanya kazi hiyo kwa nguvu zao zote kwa kuhubiri amani upendo na maneno ya kuwatia nguvu waliokata tamaa. Wito huo umetolewa hivi karibuni na mwenyekiti wa kwaya ya Ambassadors of Christ SDA ya Rwanda, maarufu kama kwetu pa zuri, ndugu Reuben Muvunyi alipokuwa akihojiwa na katika TV ya Citizen ya nchini Kenya walikokuwa kwa ziara ya kihuduma.

Wanakwaya wa kwaya ya Ambassadors of Christ SDA ya Rwanda
Mvunyi alisema kuwa, kwaya yao imeamua kujikita katika kutoa injili, kutangaza amani na kuhakikisha maridhiano yanafanywa na Rwanda baada ya kutokea mauaji ya Kimbari, yanaendelea. Muvunyi alisema, kwaya hiyo ilianza harakati zake mwaka 1995, baada ya mauaji ya Kimbari yaliyowaua watu zaidi ya milioni moja, ikiwa na jukumu la kujenga uchumi ulioharibika na kufufua tumaini jipya miongoni mwa watu waliokata tamaa. Tuliamua kujiita wajumbe wa kristo, kutokana na mambo mengi ambayo yametokea katika nchi yetu na hivyo baadhi ya waimbaji kuwa wakimbizi nchini Uganda tukaitwa "Abaganda" alifafanua mwalimu huyo. kwaya hiyo iliyojipatia umaarufu mkubwa Afrika mashariki ilikuwa nchini Kenya katika maonyesho ya uimbaji, ilianza ikiwa na waimbaji 10 lakini hadi sasa ina waimbaji zaidi ya 50 wanaotumika kama mabalozi wa kutangaza amani.

Mchango wa Serikali ya Rwanda
"Kama nilivyosema kuwa lengo la kwaya hii ni kuleta amani Rwanda. Serikali inapenda hilo ndiyo maana inatuunga mkono na imeturuhusu kwenda sehemu zote tunazotaka. Kwaya hii inasaidia kufanya kazi za Serikali kwa kuhubiri amani, tunaleta mshikamano, na umoja; Serikali imetufungulia milango, mzee wetu John ambaye ni mfadhili wetu amepewa kibali cha kufanya ibada kwenye magereza za Rwanda na anawabatiza watu walihusika na mauaji ya kimbari.
"Serikali ya Rwanda inatuunga mkono na ndio maana ilituma helikopta kuja Shinyanga kutuchukua tulipopata ajali," anasema Reuben.Wimbo bora zaidi
Sozzy ambaye ndiye mtunzi wa nyimbo karibu zote, anapoulizwa wimbo anaoupenda kuliko zote anapata shida kidogo kujua hilo."Kwanza nimesahau nyimbo nilizotunga, kwa sababu ni nyingi sana. Lakini wimbo ambao ninaupenda sana ni 'Huyo ni Yesu'. Naona nilifanya kazi kubwa kuutunga," anasema Sozzy.
Kuhusu wimbo wa ‘Kwetu Pazuri’ ambao unapendwa zaidi Tanzania, anasema; "Kwanza hakuna mtu ambaye amefika mbinguni, lakini nilijaribu kuangalia maisha ya kila siku ya hapa duniani na mbinguni nikaona ni tofauti kubwa sana.
"Wanasema malaria ndio inaua zaidi watu hapa Afrika, lakini nilifikiria nikaona mbinguni hakuna malaria. Kwa kifupi ambacho nilifanya ni kulinganisha maisha ya hapa duniani na huko mbinguni," anasema SozzyWimbo wa kwetu pazuri uliowapatia umaarufu mkubwa

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni