Jumanne, 29 Mei 2012

T​AMKO LA ASKOFU MKUU WA TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD, DK.BARNABA​S MTOKAMBALI​, KUHUSU MATUKIO YANAYOASHI​RIA UVUNJIFU WA AMANI NCHINI.

Askofu Mkuu wa kanisa la TAG Mtokambali
Kwa kipindi kirefu sasakumekuwa na mfululizo wa matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani, umoja na utengamano wa taifa letu la Tanzania, haya ndiyo yanayonisukuma kutoatamko hili leo ili kuonya na kushauri.

Katika siku za karibukiumeibuka makundi mbalimbali ya kidini ambayo yalianza kutoa matamko yenyekuchochea ghasia za kidini Tanzania, na pengine kauli hizo ndizo zinazotimizwakwa vitendo hivi sasa.

Miongoni mwa matukio hayo ni:
Januari sita mwaka huu,kikundi kimoja kinachoitwa JUAKATA, kiliitisha kongamano la kujadili katibampya Tanzania, kwa upande wa Waislam. Katika kongamano hilo lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar esSalaam kauli zifuatazo:
1.    Lazima Rais ajayeatoke Zanzibar
2.    Kukabiliana naukuaji wa kasi wa dini ya Kikristo
3.    Kupinga Muunganoili kuupa nguvu Uislamu
4.    Kupigana kufa nakupona kutetea maslahi yao wakati huu wa kuandaa katiba mpya.

Kauli hizo zilitolewa naSheikh Nasor Mohameed, kutoka Zanzibar, ambaye alikuwa mgeni rasmi. Baadayezikaandaliwa kanda za CD zilizosambaza ujumbe huo.

Uchunguzi  unaonesha kuwa miongoni mwa makanisayaliyochomwa hivi karibuni huko Zanzibar ni ya EAGT, Elimu Pentecost  na TAG, Anglikana, Katoliki na FPCT, hivyokujenga taswira ya ubaguzi wa kidini ambao kama hautapatiwa dawa unawezakuligawa taifa la Tanzania kama ilivyotokea Nigeria na kwingineko baraniAfrika.


Hofu yangu ni kuwa, roho hiiya ubaguzi wa kidini ambayo Baba wa Taifa hayati Mwl. Julius Kambarage Nyererealiifananisha na dhambi ya kula nyama ya mtu, imekuwa ikiyatafuna mataifa yaAfrika kama ifuatavyo:

1.     Mwaka 2000, vuguvugu la kuanzishwa kwa utawala wa Kiislamu (Sharia), lilianzakwenye majimbo ya Kaskazini mwa Nigeria, miaka michache baadaye majimbo kadhaayakajitangazia sheria hizo na tangu wakati huo kumekuwa na mapambanoyasiyoisha. Takwimu zinaonesha kuwa katika miaka ya karibuni zaidi ya Wakristo500 wameuawa kikatili na makanisa kuchomwa moto.

2.    Roho hii imekuwaikienea kwa kasi katika maeneo mbali mbali ya Afrika ambapo imelikumba taifa laMali, majimbo ya kaskazini tayari yametangaza kujitenga na kuna vuguvugu lenye kuhusisha mapigano ya silaha.


3.    Itakumbukwa kuwawiki chache tu zilizopita vuguvugu hili la kudai utawala wa kidini liliibukanchini Kenya ambapo watu wanaojiita wanaharakati walianzisha madai ya kutakaeneo la Pwani kujitenga na Jamhuri ya Kenya na kujitangazia taifa la Kiislamu.

4.    Ni wakati huuambao kundi la Uamsho linalopinga kuandikwa kwa katiba mpya kabla ya kuitishwakwa kura ya maoni  ili wanzazibar waamuekuhusu Muungano liliibuka na kuanzisha ghasia Zanzibar ambazo zimepelekea makanisakadhaa kuchomwa moto na mali kuharibiwa, huku watu wa bara wakitishiwa maisha.

     USHAURIWANGU KWA SERIKALI NA VIONGOZI WA DINI

Ni wajibu wa kila Mtanzaniakutii sheria  na mamlaka kwa kuwazimewekwa/kuruhusiwa na Mungu, hivyo kuziasi ni Kumuasi Mungu, yaani ni dhambi.Hivyo kila Mtanzania anastahili kukumbuka wajibu wake wa kutii mamlaka.

Viongozi wenzangu wa diniwakumbuke kuwa wana wajibu mkubwa katika jamii, na jamii inawasikiliza hivyo nivyema wakawa makini katika matamshi na maelekezo yao  ili wasiwe chanzo cha kuchochea vurugu zakidini na uvunjaji wa amani.

Ni vyema wakati huu wakuandikwa kwa katiba mpya, kila kikundi kikafuata utaratibu uliowekwa badala yakuchochea ghasia ambazo madhara yake yatawakumba watanzania wote ikiwa nipamoja na wao wenyewe watoto na wajukuu zao.

Pia ningependa kuwashauriviongozi wa serikali kusimama imara katika kusimamia sheria na haki, na kuepukakauli au vitendo vitakavyofanya baadhi ya watanzania kudhani kuwa hawatendewihaki.

Ni vema ieleweke kuwamatukio kama haya ya uvunjaji wa amani yasipodhibitiwa na kukomeshwa harakayanaweza kuumba chuki ambayo inaweza kuibua mlipuko mkubwa na machungu kwawananchi na matokeo yake yakawa mabaya kwa Taifa zima. Hekima na busarainatufundisha kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.

Ni vyema wenye dhamana yakuongoza wakakumbuka kuwa wanawajibu mbele ya Mungu aliyewaweka au kuwaruhusukuingia madarakani na siku moja watatoa hesabu mbele zake.

Mwisho, natoa wito kwa watanzaniawenzangu tuulinde umoja, amani na utengamano wa taifa letu, tuikimbie  dhambi ya ubaguzi kwa kuwa tukiiruhusuitatuangamiza sote. Tuliombee taifa letu na kukiwa na mbegu ya chuki tuimalize kwa njia ya majadiliano na vikaovya pamoja vinavyohusisha viongozi wa dini zote na serikali pia.


Imetolewa leo 28/05/2012
Na Dk. Barnabas Mtokambali
Askofu Mkuu wa TAG

kutoka samuelsasali blog

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: