Jumatatu, 14 Mei 2012

ALIKUWA CAMEROON WA UINGELEZA SASA NI BARACK OBAMA WA MAREKANI NAE ASEMA USHOGA RUKSA NCHINI KWAKE

Ule msemo unaosema kuwa chachu kidogo huchachua donge kubwa unatimia baada ya Raisi wa Marekani Baraki Obama kuruhusu ndoa za jinsia moja nchini kwake. Hii imekuja baada ya mwaka jana waziri mkuu wa uingleza kuzitaka nchi za jumuiya ya madola zikubali kuruhusu sheria ya ndoa za jinsia moja ili ziendelee kupatiwa misaada na nchi hiyo, jambo ambalo lilipingwa vikalina viongozi wan chi za afrika, tangazo hili la Obama linakuja kutia nguvu usemi wa maswahiba wao na kuwa kama moto unaotiwa petrol au msitu mkavu kutupiwa kiberiti, Raisi Obama ambaye kwa sasa anayewania urais kwa awamu nyingi amekwa akifanya vitu vingi vya kumsababishia aonekane mwema kwa kila mtu ili apate kura, kati ya washauri wake wa karibu alisema walishauriana kuwa jambo hilo si la kulisema lakini cha kushangaza yeye akalisema, Rais Obama alisema hayo kupitia TV ya NBC na kutangaza hadhalani kwa wakati umefika wa kuruhusu ndoa za jinsia moja, akifafanua alisema kuwa hayo ni mawazo yake amefikiri sana na kushauriana na watu wengi , amehudhulia mijadala mingi na mawazo yake yamekuwa yakibadili msimamo wake na anaamini wakti umefika wa kuwaruhusu.

Rais Barack Obama wa Marekani
Biblia inasema ndoa na iheshimiwe na watu wote na tangu mwanzo Mungu alipoanzisha taasisi ya ndoa alianzisha ikiwa takatifu na ni baina ya Mwanamme na mwanamke na si vinginevyo Walawi 18:22 inasema usilale na mwanamme wa mfano wa mwanamke : wala mwanamke asimame mbele ya mnyama ili kulala naye ni chukizo, lakini kwa upande wa pili makundi ya mashoga na wasagaji yamchukulia kauli hiyo kwa furaha na shangwe wakiongozwa na viongozi wao wamesema alichofanya Obama ni ushindi ya kuleta Dunia isiyo na ubaguzi, lakini mpinzani wa Obama Mitt Romney amepinga vikali kauli ya raisi huyo ambaye anakuwa kama kiraja wa dunia ambaye akisema wengine wanafuata, hii inaonyesha kuwa anataka aonekane ni mwema kwa mashoga na wasagaji ili apate kura zao lakini kwa upande mwingi si kwa kumpatia tu yeye ushindi lakini inazidi kuleta waziwazi kuwa sheria hiyo kusamba sana katika bara la Amerika na Ulaya ambako baadae tunaweza kuletewa sheria hizo hapa kwetu kwa kushurutishwa kama ilivyokuwa kwa mfumo wa vyama vingi uliletwa kwa mabavu na kutishia kuwa nchi isiyo na vyama vingi itanyimwa msaada hivyo sitashangaa na hilo nalo likija maana tuko kwenye ukolni mambo leo. hapo nyuma niliwahi kuandika makala ya kueleza kweli Tanzania hatutaki ushoga. http://martmalecela.blogspot.com/2011/11/ni-kweli-tanzania-haitaki-uashoga.html  vitabu vyote vya dini vinaeleza kuwa ni dhambi sasa huyu Cameron yeye ni mkristo wawapi ambaye hajawahi kusoma au kufundishwa na wachungaji wake na huyu Obama nae ambae yeye mpaka sasa haweki wazi kuwa yeye ni muislam au mkristo ni kweli hajui kuwa kufanya hivyo ni dhambi au kuna siri gani iliyojificha nyuma ya pazia. Wapendwa kunatakiwa tuombe sana tena kwa kukesha maana tunakoelekea si swali kabisa tunahitaji msaada wa Mungu aingilie kati maana viongozi wengi sasa wana mbeba shetani mzima mzima na kurazimisha na watu wengine wamwabudu kutokana na nafasi zao walizo

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
Chapisha Maoni