Alhamisi, 10 Novemba 2011

NI KWELI TANZANIA HAITAKI USHOGA?

Shalom wasomaji wangu ni matumaini yangu kuwa muwazima na Mungu wa mbinguni amewakilimia neema ya kuendelea kuliona jua aliloliumba. Wiki iliyopita kuna mkutano uliisha kwa waziri mkuu wa uingleza kwa kutaka nchi zote zinazopewa misaada na inchi yake wapitishe sheria za kuruhusu ushoga ili waendelee kupewa misaada ama sivyo misaada itasitishwa. Habari hii imesumbua sana vichwa vya watu na hata waziri wetu wa mambo ya nje Mh Membe alitoa tamko kuwa Tanzania haiku tayari kuruhusu ushoga ni afadhali tusipewe misaada!!!.


Binafsi nimeshangazwa na kauli ya Mh Membe na kujiuliza maswali mengi kweli alitafakali kabla ya kuzungumza au yeye kawa kipaza sauti tu kwa kujibu alichoambiwa na mtu flani?. Ina maana huwa hawaoni hao mashoga mitaani au ndo siasa zinaletwa hadi kwenye sheria watu wana zichakachua!!!


Waziri wa mambo ya nje Mh Membe

KINACHOTUPONZA NI UMASKINI WETU

Bara la Afrika tumekuwa tukiteswa na umaskini kwa mda mrefu na umaskini huu sio wa kiuchumi bali wa kimaarifa nahii imesababisha inchi za magharibi kutuendesha kama gari bovu na kwa kukosa maarifa hukohuko viongozi wetu wa kiafrica wengi wamekuwa wakiyahusudu na kufanya kila wanaloambiwa bila kujali jambo hilo litaleta athari kiasi gani katika siku za usoni. Mambo mengi mabovu yanaletwa na wao hata misaada wanayojifanya kutoa inakuwa ni mitego kwetu na tunanaswa kwenye mitego yao na kutokuwa na namna ya kufanya bali kufuata yale wanayoyasema, ni na asiyejua kuwa vita katika nchi mbalimbali za kiafrika zinadhaminiwa na haohao, mapinduzi mbali mbali ni wao wanasababisha ili wakati mwingine wauze silaha zao au wajalibishe waone zinavyo fanya kazi kwa kweli Afrika tunaangamia kwa kukosa maarifa.

Nakumbuka sana miaka ya 90 ambapo nchi hizo za magharibi zilitaka nchi za kiafrika kuanzisha mfumo wa vyama vingi katika nchi zetu ikiwapo Tanzania, na Tanzania iliunda tume ambayo ilizunguka nchi nzima kutafuta maoni ya wananch na asilimia 80 ya watanzania walikataa mfumo wa vyama vingi na kutaka chama cha CCM kitawale milele. lakini ikatokea shinikizo kuwa kama nchi haitakuwa na mfumo wa vyama vingi basi haitapewa misaada!! Basi kukawa hakuna ujanja Tanzania ikaanzisha mfumo wa vyama vingi unaoendelea mpaka sasa. Sasa nina shaka kidogo hapa hawa wenzetu wana ushirikiano kuliko sisi inamaana kama akiwashirikisha na marafiki zake wanao toa misaada Afrika ujue ujanja utaisha, na hasa pale ambapo karibu nusu ya bajeti ya nchi inapotegemea wahisani hivi ikitokea kuwa wote wakaungana itakuwaje? Jibu unalo mwenyewe lakini si hivyo tu kumekuwa na vyama vya siri kama freemason ambao wanawatumia wanasiasa wakubwa kupandikiza sera zao za kishetani katika Dunia. najua waziri huyu David Cameroni hajakurupuka na si maamuzi yake mwenyew mi naamini ametumwa na kuna vikao vilikaa kupitisha hilo sema yeye ni msemaji tu na wanatubania pabaya kwenye misaada. swali nililo nalo na sina majibu yake ni hivi afrika bila wafadhili hatuwezi kuishi? wenye jibu wanisaidia hapo na hii nayo ni changamoto nitaielezea hapo chini.


Waziri Mkuu wa UK David Cameron ambaye babu yake aliwahi kuwa Gavana wa Tanganyika enzi za ukoloni.

NI KWELI TANZANIA HAITAKI UASHOGA?

Hili nalo ni swali la kujiuliza kama kweli nchi yetu haitaki ushoga kinachonishangaza zipo hadi sheria zinazozuia watu wa jinsia kufunga ndoa au kujamiana na adhabu ni kifungo. Lakini je? Kweli hizi sheria zinafuatwa nia mashoga wangapi tunawaona wanarandaranda mitaani bila kuchukuliwa hatua zozote au niwasagaji wangapi wapo ha vyombo vya habari (magazeti) kila siku yanatoa habari zao lakini sijawahi kusikia hata siku moja kuwa wamekamatwa na kuwekwa ndani ina maana polisi, mahakana hata yeye waziri hawajui hili au ni danganya toto sasa hapo ugumu ukowapi wakubadisha kwenye makaratasi tu!! Au bola lipi hapa ukasema hautaki na wakati unafanya? Hawa wenzetu kabla ya kufanya mambo yao wanakuwa wamesha jiridhisha na ninajua kuwa wanajua kuwa Tanzania wapo mashoga na wanaishi raha msitarehe wakifanya shughuli zao za kishoga bila bugudha na ndo maana wanatamka hivyo na zipo hata NGO na viongozi wanao watetea. Mimi nilidhani, na ningefurahi sana kama hiyo kauli ya Mh Membe ungetekelezwa kwa vitendo kwa kuwaweka ndani mashoga wote. Lakini kwa kuzungumza tu na kutotenda yanayozungumza imenifanya kujua hizi ni plopaganda za kisiasa za kujifanya hamtaki wananchi wawaone ni wazuri na sitashangaa kama baadae ikateuliwa kume na kukusanya maoni ya wanainchi najua wengi tutapinga lakini mwisho wa yote tutawaangukia wazungu watupe misaada. Jana nimeona picha na habari za mashoga wameandamana kuunga mkono habari ya waziri mkuu wa uk David Cameroon kama kweli hawataki mbona hawajawakamata na kuwaweka ndani?


Mashoga wakiandamana kuunga mkono kauli ya waziri mkuu wa UK kwaniani hawakukamatwa si hawa hapa?

CHANGAMOTO KWA KANISA.

Kwa kanisa sidhani kama kuna mtu atapinga kuwa sasa hizi ndio siku za mwisho kila siku inakuwa na vituko vyake bora ya vya jana. Wapendwa tuwe macho hasa na shetani wakati mwingine anakuja kama malaika wa nuru kumbe ni mwovu mambo yote yanayotekea sasa nyuma yako iko nguvu ya shetani chini ya mwamvuli wa vyama vya freemason na vingine. Wamekuwa wakifanya na kusapoti mambo yote maovu kwa gharama kubwa na mitandao yao imebeba watu wenye nguvu kifedha na kisiasa wenye ushawishi mkubwa mbele za jamii na wanaloongea linakubaliwa na jamii na sasa tunakoelekea mafuta na maji yanaenda kujitenda na itajulikana nani wa Mungu na nani wa shetani maana kama umesikia mchakato unaoendelea wa kuunganisha dini za kiislamu na kikristo baadae itakuwa dini ya muunganono dhidi ya walikole hapo sasa ndo itajulikana mlokole wa kweli ni nani na Yule anyeenda kupasha kiti moto. heri nife njaa kuliko kuuacha upendo wa Mungu heri niwe uchi kuliko kulidhalilisha jina la Mungu wangu heri nidharauliwe Duniani lakini nikaheshimike mbinguni.

Changamoto tuliyonayo ni kuendelea kumtegemea Mungu na kufuata maagizo yake maana yeye amesema hatatuacha mpaka utimilifu wa dahali nay eye aliye ianzisha kazi ndiye atakaye imaliza na neon linguine ambalo huwa linanitia nguvu lile lisemalo atalijenga kanisa lake katika msingi ulio imara hata nguvu za kuzimu hazitalishinda. Kazi tuliyo nayo ni kuhubili injili na kutoa mafundisho sahihi ili watu wasiasi imani waliyo nayo pindi watakapo kutana na mambo magumu. Hao freemason watapigana lakini hawata shinda sisi ni washindi na zaidi ya washindi.Ubarikiwe.


Mathayo 6:33 Utafuteni kwanza ufalme wake na haki yake na hayo mengine mtazidishiwa.
Chapisha Maoni