Biblia inasema
wazi kwamba dunia yote inaongozwa na falme mbili tu:
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK martmalecela
1.
Ufalme wa Mungu (Ufalme wa
Mbinguni) ambao mfalme wake ni Yesu Kristo.Raia wa ufalme huo ni wale
wanaomwamini na kuukubali uongozi wake na mamlaka yake.
2.
Kuna ufalme mwingine unaoitwa
ufalme wa giza ambao mfalme wake ni Ibilisi, Yule malaika mkuu aliye muasi
Mungu. Ibilisi ameifanya dunia ndipo mahali pa utawala wake. Raia wa ufalme huo
ni watu wote ambao wameukataa mpango wa wokovu. Shetani na raia wake ni adui wa
Mungu.
Shetani anajitahidi kuwafanya wanadamu wawe waovu , wasio mwamini na
kumtii Mungu ili wakifa wafe katika dhambi zao, aende nao jehanamu.
Silaha yake kubwa ni Dini.
Hutumia Dini kuwalaghai
watu waamini kwamba:
1.
Kuna dini ambayo mwanadamu
akijiunga nayo anakubaliwa na Mungu kwa sababu dini hiyo pekee ndiyo dini ya
Mwenyezi Mungu. Akifa dini hiyo itamfanyia ibada na kumzika ipasavyo.
2.
Mungu humkubali mwanadamu kwa
kuyapima matendo yake mema na matendo yake mabaya. Kama matendo yake mema ni
mengi kuliko matendo yake mabaya mwanadamu huyo atakubaliwa na Mungu.
Kwa ulaghai huo
wanadamu wengi wanaukataa mpango wa Mungu wa kuwaokoa kutoka katika ufalme wa
shetani na wanakufa wakiwa watoto wa shetani, wanakufa wakiwa katika dhambi
zao.
Biblia
inatufundisha kwamba dhambi humtenga mtu na Mungu na kwamba wanadamu wote
wametenda dhambi (Isaya 59:2, Warumi 3:23). Hii inamaana kwamba wanadamu wote,
kwakutenda dhambi, hujiunga na ufalme wa shetani.
Biblia inatueleza
mpango wa Mungu wa mwenye dhambi kuweza kupokelewa kwenye ufalme wa Mungu. Njia
hiyo ndiyo njia pekee kwa watu wote:
1.
Wale wanaotubu na kuiamini
injili ndio wanaokubali mpango wa kuokolewa na ndio wanao fanyika raia katika
ufalme wa Mungu.
“Amini, amini nakuambia mtu asipo zaliwa kwa mara
ya pili hawezi kuuona…………kuuingia ufalme wa Mungu” (Yohana 3:3, 5)
“Naye alituokoa katika
nguvu (ufalme) wa giza akatuamisha na kutuingiza katika ufalme wa pendo la mwana wake( Yesu)” (Wakolosai 1:13).
2.
Wale wanaokataa wanaangamia
“Huku akiwalipiza kisasi
wao wasio mjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu watakao
adhibiwa kwa maangamizo ya milele kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu
zake”. (Wakolosai 1:8-9)
Mungu anataka watu
wote waokolewe kutoka katika ufalme wa shetani. Hataki hata mmoja aangamie.
Anataka watu wote wawe katika ufalme wake,
Swali langu ni hili: JE MUNGU AMESHAKUOKOA KUTOKA
KATIKA UFALME WA SHETANI, au umeuamini uongo wa shetani na umeukataa mpango wa
Mungu?
Kama unaamua akuokoe leo sema sala hii:
“Ee, Mungu nihurumie mimi mwenye
dhambi. Natubu mbele zako naomba unisamehe na uniokoe kutoka katika ufalme wa
shetani na unihamishe na kuniingiza katika ufalme wa Mwana wako Yesu Kristo”
Amina
Kama umesema sala
hii kwa kumaanisha; Mungu amekusamehe na
kukuokoa. Jiunge na kanisa la watu waliookoka.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni