Jumatatu, 14 Mei 2012

KAKOBE ATOKA MAFICHONI NA KUSEMA

Hatimaye Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Zachary Kakobe ambaye amekuwa kwenye maombi mazito kwa zaidi ya miaka miwili sasa. Akiwa amejifungia ndani na kuvunja ibada zote za kawaida, amevunja ukimya na kuonya kuwa, yaliyowapata mawaziri akiwepo William Ngeleja wa nishati na madini na katibu wake David Jairo, ni rasha rasha tu kwani kimbunga bado kinakuja. Kakobe amewaeleza watu wa karibu yake kuwa Mungu yu hai na huwasikia wanaomulilia. Ameendelea kuwa kwenye maombi yasiyo na ukomo mpaka pale kimbunga hicho kitakapowakumba wale anaoamini kuwa walilazimisha kupita kwa nguzo za umeme mkubwa karibu na kanisa na kukwamisha mpango wake wa kufungua kituo cha kurusha matangazo ya TV kwa ajiri ya kuhubiri injili.


Askofu Kakobe akiwa na waumini wake muda mfupi kabla ya kuingia kwenye maombi ya zaidi ya miaka miwili sasa.
Japo mawaziri 6 na manaibu waziri wao wameng’olewa katika nyazifa zao kutokana na kupata pingamizi kwa wabunge katika bunge lililopita, lakini jicho lake lililenga kwenye wizara ya madini na nishati ambayo ilikuwa na vita na Kakobe ambaye tangu Machi saba mwaka 2010 amekuwa mafichoni akiomba bila kuchoka. Askofu kakobe ameweka bayana kuwa pamoja na mabadiliko hayo makubwa, bado hatotoka katika maombi na ataendelea mpaka kieleweke na ajulikane nani Mungu wa kweli. Tangu mwaka wa 2010 Kakobe hajaonekana hadharani na analofanya ni kuhubiri ibada za jumapili tu na baada ya ibada hurudi kwenye maombi , kutokana na hilo alisimamisha mahubiri yake kwenye vituo vya TV na kutokusafiri safari yeyote. Hasira za kakobe zilikuja mradi wao wa TV kukwama kutokana na nguzo kupita kanisani kwao ambazo zinaweza kusababisha madhara kwa mitambo ya TV, alikuwa anzishe kituo hicho ili kuepuka gharama kubwa zinazokadiliwa kufikia million 500 alizokuwa akitoa kuripia kwenye vituo vingine.

Watalamu wa masuala ya mawimbi ya television wanaamini kuwa huwezikujenga kituo cha TV unapotita mkondo wa umeme Mkubwa, Kakobe ambaye amekuwa haonekani kwa muda sasa hata kusababisha habari za uzushi kutokea juu yake kuwa ni mgojwa na amepooza huku wengine wakisema kuwa amekimbia Nchi.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FACEBOOK Martin Malecela

Hakuna maoni: