Alhamisi, 14 Machi 2013

PAPA MPYA ACHAGULIWA JUA WASIFU WAKE


Usiku Wa Jana Kwa Saa za Africa Mashariki Kanisa Katoliki imemchagua "Cardinal Jorge Mario Bergoglio Kutoka Argentina kuwa Mrithi Wa Papa Benedict. Baada Ya Uteuzi huo Maelfu Ya Waumini Walitambulishwa Papa Mpya atakuwa akitambulika Papa Francis Wa Kwanza.

Kuna Mambo Kumi Blog Inataka Kukujuza Kuhudu Papa Mpya Francis.

1. Papa Francis amechagua Jina hilo kutokana na Jina la Co-founder wa Jesuits Society. Kwa wanafatilia issue za Kanisa Katoliki Watafahamu kuwa Founder wa Jesuits ni Ignatius Of Loyola akishirikiana na Francis Xavier ambaye alikuwa Mspain.

2. Papa Francis ni Muumini wa Jesuits tangu Miaka ya 1960's amekuwa akifanya kazi na Jamii hii na kuwa Mtiifu Mpaka sasa alipoteuliwa kuwa Papa.

3. Papa Francis ana Pafu moja jambo ambalo linaweza kuleta ama kupelekea uchaguzi mwingine iwapo afya yake itazorota kama ambavyo Papa Benedict aliomba Kupumzika baada ya afya yake Kudadi Kuzorota.

4. Papa Francis ni Mwanaharakati anayepinga ndoa za Jinsia moja. Mwaka 2010 akiwa nchini kwake Argentina alieleza wazi yeye hana shirika na sheria za jinsia moja Nchini kwake.

5. Papa Francis alikuwa akitarajiwa kuwa Papa baada ya Benedict kwani tangu mwaka 2005  Papa Francis alijizolea maelfu ya Kura ni Papa aliyechuana na Papa Mstaafu kuwania Kinyang'anyiro hicho.

6. Mwaka 2005 alizushiwa zengwe kuelekea kwenye Uchaguzi wa Papa Kuwa Mwaka 1976 aliwa Kidnap Watawa Wawili walio katika Jesuits lakini alishinda Kesi hiyo sababu ilikuwa ni Zengwe la kutengenezwa.

7. Papa Francis kabla ya Kuwa Jesuits alikuwa anapenda kazi za kuwa Mkemia, mtu wa Maabala lakini kwa sababu kadha wa kadha mwaka 1969 akaanza kufanya kazi za Jesuits.

8. Papa Francis anapenda Kujipikia mwenyewe. Ukifatilia taarifa mbalimbali katika Mitandao utaona kuwa Papa Francis anapenda kujipikia chakula chake na kuna hatihati akiwa Vatican akaanza Kujipikia Mwenyewe.

9. Papa Francis ni Mtu wa Kujichanganya, Jana baada ya Kuongea kwenye Tv nika post Facebook kuwa Papa Francis anaonekana ni Muongeaji na Mchangamfu. Nilipofatilia kwenye Mitandao Papa Francis ni Mtu wa Kijichanganya akiwa Argentina aliacha Kukaa Nyumba Makadinari akaenda Kukaa nyumba wanazokaa Ma padri na Watawa wengine.

10. Papa Francis mbali tu na ile hali ya Kujichanganya na Mapadri Papa Francis huwa anapanda Public Buses "Dala dala". Mara kadhaa Argentina Papa Francis amekuwa akipanda Dala dala na Kujichanganya na Raia wengine katika Shida ya Mabasi (kama ipo) kama Usafiri wa wote.

KWA HISANI YA PAPAA BLOG
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela

Hakuna maoni: