Lile kundi maarufu la Glorious Celebration ambalo miezi michache iliyopita limesajiliwa kama kampuni ili liweze kujiendesha katika mfumo wa kikampuni limegawanyika na kuwa makundi mawili. mmiliki wa kundi hilo Askofu Mwakang'ata
wimbo maarufu na unaopendwa na watu wengi na ndio uliolitambulisha kundi hili
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
amewaambia wadau wa habari kuwa ameshangaa baadhi ya waimbaji kutowaona na japo amejitahidi kuwatafuta na kuongea nao imeshindikana na akaona matangazo na habari kuwa kundi hilo lina jina jipya yaani GWT(Glorious worship team).
akiongea katika mkutano huo na vyombo vya habari vya kikristo mwenyekiti wa GS alisema ameshangazwa kuona matangazo yanaonyesha watasheherekea kutimiza miaka 2 na kuzindua audio ya vol 2 wao walitakiwa waseme kuwa wanazindua kundi jipya la GWT na si kutimiza miaka 2 maana GS ndiyo inatimiza miaka 2 na tutaingia kambini kwaajili ya kuanda siku kwenye mwezi wa tatu tuazimishe hiyo miaka 2. kiongozi wa kundi jipya la GWT Emanuel Mabisa ameweza kutupiwa lawama kuwa ndiye sababu ya haya yote nguvu yake kwenye kundi imempa uwezo wa kuwa na ushawishi mkubwa kwa waliojitenga.
Mwenyekiti wa GS amesema kundi lililobaki wanaingia kambini kujifua kwaajili ya kuandaa siku ya kumshukuru Mungu kwa kutimiza miaka 2. bado kumekuwa na utata wa nyimbo ambazo zilikuwa zikiimbwa walipokuwa pamoja maana bado zimetumiwa na kundi lililojitenga ijapo Askofu mwakang'ata alisema nyimbo zote hata kama zilitungwa na kundi lililojitenga maadamu zilitungwa wakati ule wa zamani basi GS zitabaki kuwa za GS watamiliki nyimbo zote ikiwepo wimbo wa NIGUSE, NIGUSE uliolipa umaarufu mkubwa kundi hilo uliotungwa na Emanuel Mabisa.
Enzi za GS wakiwa wenye furaha |

Kundi Jipya la GWT |
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni