Jumanne, 21 Julai 2015

UZURI WA KUKEMEWA



 
Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa; Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama” (Methali 12:1).
 
Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao” (Zaburi 141:5).
 
Umewahi kujiuliza faida za kupigwa, kukemewa, kulaumiwa, kulalamikiwa, kuulizwa, nk. mara ufanyapo jambo ambalo mwingine hakupenda au jambo ambalo si haki kufanya?
 
Nimejifunza jambo hili juu ya NAFSI ya mtu ampendezaye Mungu; huchukua maonyo, makemeo, mapigo, matukano, laumu, malalamiko, nk., kama mambo MUHIMU ya kujiweka vizuri zaidi na si mambo ya kuleta chuki, hasira, kisasi, kinyongo, mafarakano, matengano, nk. Suleiman anasema, “achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama”! Yaani, kwa binadamu BORA, kulaumiwa ni sehemu ya maisha, ili aweze kujiboresha na kubadilika, ni lazima KUPOKEA na KUFANYIA kazi malalamiko na malaumu bila KUWACHUKIA au KUWAPINGA wakulaumuo kwa maana wao ni MSAADA kwako na sio lazima kwamba ni adui zako.
 
Akusaidiaye SANA sio akusifiaye tu, bali akuambiaye MAPUNGUFU yako kwa uwazi (bila kujali sana lugha anayotumia). Mara nyingi KIBURI kimejiinua na kusema, “sawa, angeniambia ila angesema taratibu, sasa yeye ananipigia kelele”, au “mimi ni mtu mzima, naelewa ninachofanya”, “sipendi kupangiwa cha kufanya”, nk.
 
Ukiona unaambiwa MAPUNGUFU yako (kulaumiwa, kufokewa, nk.) halafu unasikia kama kuna kitu kinakukaba koo, basi ujue unamahali pa kujiweka vizuri kwa maana hiyo hali itakuangamiza. Daudi anasema, “Mwenye haki na anipige, itakuwa fadhili; Anikemee, itakuwa kama mafuta kichwani; Kichwa changu kisikatae, Maana siachi kusali kati ya mabaya yao”. Kwa Daudi, sio kukemewa tu, hata akipigwa ni sawa. Umeona jinsi ambavyo Daudi hakuchagua namna ya kukemewa? Wala hakuwafundisha wamkemeao namna ya kumkemea! Vyovyote vile, kwake ni fadhili, na kama mafuta kichwani mwake, tena anakiambia KICHWA chake (akili za nafsi yake) kisikatae maonyo (bila kujali sana yamekujaje).
 
Anaheri mtu yule AFURAHIYE aambiwapo mapungufu yake, naam, ASIYEMCHUKIA amkemeaye na kumwonya, maana huyo atakuwa BORA zaidi na ataona kuongezeka na baraka zikimfuata na kumpata. Na ajuapo KUOMBA juu ya mapungufu yake, huyo atakuwa kama meli iliyotia nanga, hatayumbishwa kamwe.
 
Frank P. Seth.KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: