Jumatatu, 2 Machi 2015

UNGANA NA MCH MARRY KANEMBA KATIKA HARAMBEE YA UKUSANYAJI WA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA MAFUNZO YA MZIKI WA INJILI

Mch Marry Kanemba ambaye pia ni mwimbaji wa nyimbo za injili, ana maono ya kuanzisha kituo maalumu cha mafunzo ya muziki wa injili. hayo yatafanyika katika kanisa la TAG tar 29/03/2015. katika harambee hiyo kutakuwa pia na uzinduzi wa DVD ya mch Marry kanemba. Lakini kubwa zaidi utakuwepo uchangiaji wa kupata fedha kwaajili ya kununua vyombo vya muziki na kuanzisha ujenzi wa kituo cha mafunzo ya muziki wa injili.
katika harambee hiyo Mch Kanemba atasindikizwa na waimbaji wengine wengi wa nyimbo za injili kutoka katika viunja vya jiji la Dar es salaam. kama The next level kutoka kanisa la TAG Upang, Jennifer Mgendi, Amos Khamisi kutoka TAG Magomeni, Ibrahim Sanga, Kiza Blessing, Linus Cosam, Magreth Maziku, Calvary Brothers, Kwaya ya revival, Deodoxah na Praise team ya Magomeni TAG. kila mwenye mzigo wa injili unaombwa usikose kwenye tamasha hilo litakaloanza saa 14:00 - 22:00 usiku. au la unaweza kuwasiliana na Mch Dunstan Kanemba kwa no 0784523399 au mch Marry Kanemba kwa no 0765858785 au unaweza kuweka mchango wako kupitia account no 0152209596200 crdb bank. 


Huu hapa ni moja ya nyimbo ambazo zitazinduliwa.
           
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni