Mtunga Liriki/Maneno: Horatio Gates Spafford
1828 - 1888.
Mtunga Vokali/Sauti: Philip Paul Bliss 9 Julai 1838
– 29 Desemba 1876
Mwandishi wa wimbo huu Horatio Gates Spafford alizaliwa yapata mwaka 1828 na kutwaliwa mwaka wa 1888 akiwa ameishi duniani kwa miaka ipatayo 60 tu. Mtunzi wa vokali/sauti/tuni anaitwa Philip Paul Bliss ambaye aliishi kwa miaka 38 tu hadi anatwaliwa Mbinguni. Wimbo huu hata hivyo kwa jinsi ya upako wake, umepewa sauti tofauti tofauti na zote zikiwa zina mguso ule ule zinapoimbwa.
Mtunzi wa wimbo |
Mtumishi
wa MUNGU Horatio Spafford, alikuwa mwanasheria na alikuwa tajiri sana. Aliishi
na kufanya biashara zake huko Chicago Marekani. Alikuwa na familia ya watoto
watano, mabinti wanne na mvulana mmoja. Pia alikuwa ni mkristo na mwanafunzi
mzuri wa maandiko matakatifu. Katikati ya mafanikio yake, Horatio alimpoteza
kijana wake mwaka 1870 aliyefariki kwa ugonjwa uitwao kwa lugha ya kiingereza scarlet
fever unaosababishwa na bakteria. Akiwa bado anaendelea kuomboleza kifo cha
mtoto wake mpendwa, tarehe 08 Oktoba 1871 siku ya Bwana [Jumapili] majira ya
saa tatu usiku, moto mkubwa uliopewa jina la moto mkubwa wa Chicago [The Great
Chicago Fire] ulianza na chanzo chake inasemekana ni ng'ombe aliyepiga teke taa
ya mafuta iliyokuwa katika banda lake.
Moto
huo ulisabisha vifo vya watu takribani 300 na uliteketeza eneo la karibu
kilomita za mraba 9 na uliacha watu zaidi ya 100,000 bila makazi. Ni katika
ajali hii ya moto, Mtumishi wa MUNGU Horatio alipoteza mali zake nyingi sababu
aliwekeza sana katika eneo hilo la Chicago. Wakati biashara za Mtumishi Horatio
Spafford zinaanza kufanikiwa, janga lingine likampata. Yapata mwaka 1873,
biashara zake zikakumbana na anguko kubwa la uchumi [Great Economic Depression]
lililoendelea hadi mwaka 1879. Anguko hili la uchumi lilisababishwa na sababu
nyingi ikiwemo Moto mkubwa wa Chicago wa mwaka 1871. Kutokana na matatizo hayo yote
ambayo familia yake ilipitia, Mtumishi wa MUNGU Horatio Spafford aliamua
kuipeleka familia yake nje ya Marekani kwa ajili ya mapumziko na kujaribu kupunguza
msongo wa mawazo [stress] kufuatia matukio hayo mawili ya ajali ya moto na
anguko kubwa la uchumi vilivyowaathiri kama familia.
Wakaamua
kwenda Uingereza ambako pia rafiki zake Moody na Sankey walikuwa wanafanya
huduma ya kuhubiri Injili wakizunguka dunia nzima kupitia huduma ya utalii wa
kiinjili ulioratibiwa na Pastor John
Wilbur Chapman. Kama vile Roho Mtakatifu alikuwa anamzuia, muda mfupi kabla ya
safari yao, alipata udhuru na ikambidi abaki ili kushughulikia masuala
yaliyokuwa yamejitokeza katika biashara zake. Kwa kuwa muda wa safari ulikuwa
umekaribia sana, aliiruhusu familia yake itangulie na kwamba yeye angefuata
baadaye. Yapata tarehe 15 Novemba, 1873, familia yake wakiwemo mke na watoto
wanne walianza safari kutoka New York kuelekea Ufaransa na meli iliyoitwa Ville du Havre.
Mnamo
tarehe 22 Novemba, 1873, majira ya saa nane za usiku mnene, wiki moja tu baada
ya kuanza safari, wakiwa ndani ya bahari ya Atlantiki, meli ya Ville du Havre iligongana na
meli nyingine iliyoitwa Loch Ear. Takwimu
za kikosi cha uokozi zilisema kiasi watu 226 kati ya 313 waliokuwa ndani
ya meli ya Ville du Havre, walipoteza
maisha na kusalimika watu 87 tu. Miongoni mwa waliopoteza maisha walikuwemo watoto wote wanne wa Mtumishi Horatio
Spafford. Mnamo Tarehe 1 Desemba, 1873, Mtumishi Horatio Spafford alipokea
ujumbe toka kwa mkewe ambaye alinusurika katika ajali hiyo akimweleza, “...Ni
mimi tu nimesalimika...”, “Ijapokuwa nimepata majaribu kiasi hiki [akirejea
ajali ya moto iliyoteketeza mali zake, anguko kubwa la uchumi na ajali ya meli
iliyoua watoto wake wote], nina furaha kwa sababu bado namwamini MUNGU”.
Haya
ndiyo yalikuwa maneno ya Mtumishi Horatio baada ya yale ya mke wake. Wiki
chache baadaye akiwa njiani kuelekea Uingereza alikokuwa mke wake, nahodha wa
meli aliyokuwamo aliwataarifu kuwa eneo walilokuwa wanapita, ndipo ilipotokea
ajali ya meli iliyouwa watu 226 wakiwemo watoto wake Horatio. Kwa majonzi na
uchungu mwingi, Mtumishi wa MUNGU Horatio alichukua kalamu yake na karatasi,
akaandika utenzi ambao baadaye ulikuja kuwa wimbo uitwao “Ni Salama Rohoni
Mwangu”
Baadaye tena MUNGU aliikumbuka nyumba ya Mtumishi wake Horatio na akaibariki na watoto wengine watatu, wa kiume mmoja ambaye alikuja kufariki akiwa na umri wa miaka minne na mabinti wawili. Yapata mwaka 1881, familia ya Mtumishi Horatio ilihamia Yerusalemu, Israel na wakajihusisha na harakati za kusaidia wahitaji/masikini. Kikundi ambacho uasisi wake ulitokana na mwandishi Selma Lagerlof kushinda tuzo ya nishani ya Nobel mwaka 1909 kupitia kitabu chake cha hadithi kijulikanacho kama Jerusalem.
Baadaye tena MUNGU aliikumbuka nyumba ya Mtumishi wake Horatio na akaibariki na watoto wengine watatu, wa kiume mmoja ambaye alikuja kufariki akiwa na umri wa miaka minne na mabinti wawili. Yapata mwaka 1881, familia ya Mtumishi Horatio ilihamia Yerusalemu, Israel na wakajihusisha na harakati za kusaidia wahitaji/masikini. Kikundi ambacho uasisi wake ulitokana na mwandishi Selma Lagerlof kushinda tuzo ya nishani ya Nobel mwaka 1909 kupitia kitabu chake cha hadithi kijulikanacho kama Jerusalem.
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Maoni 6 :
Weka historia za nyimbo nyingine nyingi
Barikiwa sana
Barikiwa sana
Inatia moyo Kumtegemea Mungu Kuna faida
Historia ya wimbo wa Tufani inapivuma
Mungu kwetu nipendo anatujali
Chapisha Maoni