Jumanne, 16 Desemba 2014

WANAMUZIKI MBALIMBALI KUTOKA AFRICA WAIMBA WIMBO WA EBOLA, WAMO JOYOUS CELEBRATION, TANZANIA YAWAKILISHWA NA DIAMOND

mwimbaji wa muziki wa nje ya injili nchi Tanzania Nasibu Abdul, almaarufu kwa jina la Diamond Platnumz, ni mmoja kati ya waimbaji wengine wengi wa Afrika, walioshiriki pamoja na kundi maarufu kwa nyimbo za injili nchini Afrika kusini Joyous Celebration, kurekodi wimbo wa pamoja kupiga vita gonjwa la EBOLA, wimbo huo ambao ni wazo na utunzi wa Joyous Celebration

kazi ya kurekodi video ya wimbo huo, imefanyika katika shirika la utangazaji la SABC, nchini Afrika kusini, huku umoja huo wa wasanii walioimba wakitumia jina la wimbo maarufu la wimbo ulioimbwa na waiimbaji nyota nchini marekani wa kusaidia bara la Afrika "WE 'RE THE WORLD" ila wao wakiongezea Afrika mbele yake. ukiacha kundi la Joyous pia kulikuwa na kundi la waimbaji wengine toka Afrika kusini kama Mahottella Queens, Mafikizolo, pamoja na waimbaji wengine tokea Nigeria na pande nyingine za Afrika.

Tanzania ikiwa imewakilishwa na mwimbaji huyo ambaye amejinyakulia Tuzo tatu, kati ya nne, alizokuwa anawania ambazo ziliandaliwa na kituo maarufu cha Chanel O, huko nchi Afrika kusini

Diamond (mwanamuzi maarufu TZ) akiwa na waimbaji mbalimbali, kwenye studio za SABC,  wakiwemo na waimbaji wa kundi la Joyous Celebration  
Mwimbaji wa muziki wa nje ya kanisa nchini Nasibu Abdul almaarufu kama Diamond Platnumz ni mmoja kati ya waimbaji wengine wengi wa Afrika walioshiriki pamoja na kundi maarufu la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini kurekodi wimbo wa pamoja kupiga vita gonjwa la ebola, wimbo ambao ni wazo na utunzi wa Joyous Celebration.

Kazi ya kurekodi video wimbo huo imefanyika katika studio za shirika la utangazaji la Afrika ya kusini SABC nchini Afrika ya kusini huku umoja huo wa wasanii walioimba wimbo huo wakitumia jina la wimbo maarufu ulioimbwa na waimbaji nyota wa nchini Marekani kusaidia Afrika wa 'We are the world wenyewe wakiongeza neno Afrika mbele yake.

Ukiacha kundi la Joyous pia kulikuwa na waimbaji wengine kutoka Afrika ya kusini kama Mahottella Queens, Mafikizolo na wengineo pamoja na waimbaji kutoka Nigeria na pande nyingine za Afrika, Tanzania ikiwa imewakilishwa na mwimbaji huyo ambaye pia alijinyakulia tuzo tatu kati ya nne alizokuwa anawania zilizokuwa zimeandaliwa na kituo maarufu cha Channel O cha nchini humo. - See more at: http://www.gospelkitaa.co.tz/2014/12/diamond-platnumz-arekodi-wimbo-na.html#.dpuf


Baadhi ya waimbaji wa Joyous wakipata picha ya pamoja
                                      Baadhi Ya Waimbaji wa Joyous
Sylvester Funani wa Joyous, akiwa na waimbaji wa Mahottella Queens

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO 0784 477775 au Whatup 0784 477775 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni