Maisha yake ya awali na elimu
AMES Travis Reeves
alizaliwa Agosti 20, 1923 huko Galloway,
Texas nchini Marekani, kijiji kidogo karibu na Carthage, pia alijulikana kwa jina la ushabiki la
Gentleman Jim. Alishinda skolaship ya mchezo wa riadha; ya kwenda kusoma chuo
kikuu cha Texas, alidahiliwa
kusoma kozi ya hotuba na maigizo, lakini aliacha masomo ndani ya muda wa majuma
sita tu na kwenda kufanyakazi kama kuli huko Houston. Muda siyo mrefu alirejea mchezo wake wa
nyenje/kriketi, akicheza ligi daraja la pili kabla ya kuingia mkataba na timu
ya shamba la St. Louis Cardinals
mnamo mwaka 1944 kama mchezaji mahiri mwenye kutumia zaidi mkono wa kulia. Alichezea
ligi za chini kwa miaka mitatu kabla ya kuumia kwa diski ya uti wake wa mgongo
[sciatic nerve] kujiachia akiwa uwanjani na kuhitimisha kabisa taaluma yake ya
riadha.
Uchanga wa kazi ya muziki
Reeves alianza kufanyakazi kama mtangazaji
wa redio, na aliimba nyimbo laivu redioni. Yapata miisho ya miaka ya 1940s, alipewa
mikataba na makampuni madogo ya kurekodi miziki ya Texas, lakini pasina
mafanikio. Akiwa amevutiwa sana na wasanii wa muziki wa Magharibi kama akina Jimmie Rodgers na Moon Mullican, pamoja na
waimbaji maarufu kama akina Bing
Crosby, Eddy Arnold na Frank
Sinatra, haikupita muda akajiunga na bendi ya Mullican, na kufyatua
nyimbo za awali zenye staili ya Mullican kama "Each Beat of my Heart"
na "My Heart's Like a Welcome Mat" kuanzia miisho ya miaka ya 1940s hata
mapema miaka ya 1950s. Hatimaye akaja kufanyakazi kama mtangazaji wa KWKH-AM katika Shreveport, Louisiana, ambapo
palijulikana kama kituo cha vipindi maarufu vya redio Louisiana Hayride.
Mafanikio ya awali katika miaka ya 1950s
Miziki ya kwanza ya Reeves iliyotikisa
nchi inajumuisha "I Love You"
(a duet with Ginny Wright),
"Mexican Joe", na
"Bimbo" ambao
ulishika nambari moja katika mwaka wa 1954 katika orodha ya Marekani ya miziki
bora. Mapema mwaka 1955, alipata mkataba wa miaka 10 wa kurekodi miziki katika RCA Victor na Steve Sholes, ambaye
alitoa baadhi ya kazi za kwanza za. Pia mwaka 1955, alijiunga na The Grand Ole Opry na akajitokeza
kwa mara ya kwanza kwenye jubilee ya ABC-TV, ambapo alikuwa mwenyeji kuanzia Mei–Julai
1958.
Kwenye kazi
zake za RCA, Reeves alikuwa bado akiimba kwa staili ya rekodi zake za awali
ikichukuliwa kuwa ndiyo viwango vya nchi yake na waimbaji wa Magharibi kwa
nyakati hizo. Sauti yake ilishuka akitumia ulingo mdogo huku akiimba hali mdomo
wake ukigusa kipaza sauti japo kulikuwa na mgomo wa wafanyakazi wa RCA ambao
wangeweza kumrekebisha. Reeves alikuja kujulikana kama mwimbaji mwenye hisia
kali kutokana na utajiri wa sauti nyororo. Nyimbo kama "Adios Amigo",
"Welcome to My World", na "Am I Losing You?" vinaelezea
ukweli huu. Nyimbo zake za Krismas zimekuwa zikipendwa kwa misimu yote
zikijumuisha "Krismas",
"Blue Christmas"
na "An Old Christmas Card". Pia ametumika kuzipa umaarufu nyimbo
nyingi za Injili zikiwemo "We
Thank Thee", "Take
My Hand, Precious Lord", "Across The Bridge", "Where We'll Never Grow Old"
na nyingine nyingi.
Mapema miaka ya 1960s na umaarufu
wake wa kimataifa
Reeves alipata mafanikio yake makubwa kwa
utunzi wake na Joe Allison
wa "He'll Have to Go"
na kumpatia tuzo ya shaba. Aliitoa kwa umma mwishoni mwa 1959, na kushika
nambari moja kwenye kura ya maoni ya jarida la Billboard kwenye safu ya nyimbo
kali za wasii wa ndani ya nchi mnamo Februari 8, 1960, ambayo ilishinda mara 14
mfululizo. Mwanahistoria wa miziki ya ndani ya nchi ndugu Bill Malone aliutolea
maoni wimbo huu kama wimbo unaogusa nchi nzima". Pia Malone alisifia sauti
ya Reeves akisisitiza kuwa wapenzi wake wanamfananisha Reeves na mtu mwenye
sauti laini kama kitambaa cha velvet. Mwaka 1963, alitoa albamu yake maarufu ya
nyimbo 12 za Krismas. Mwaka 1975, produza wa RCA Chet Atkins alimweleza msaili Wayne Forsythe, kuwa
"Jim alitaka kuimba tu pasina kujali utamu wa sauti ambao ndiyo nilitaka
afikie... Nilikuwa sahihi, kwa kweli. Baada ya kubadili sauti yake kuwa ya
kuvutia sana hadhira, aliibuka na kuwa maarufu sana." Umaarufu wa Reeves
ulivuma kimataifa katika miaka ya 1960s. Umaarufu wake Marekani ulisaidia
kuzipa miziki ya nchi yake soko la dunia nzima kwa mara ya kwanza.
Afrika Kusini
Mapema miaka ya 1960s, Reeves alikuwa
maarufu zaidi nchini Afrika Kusini kuliko Elvis Presley na alirekodi albamu
nyingi katika lugha ya Afrikana.
Mwaka 1963, alitalii na kutolewa kwenye filamu ya Afrika Kusini iliyoitwa Kimberley Jim. Filamu hii
ilitolewa ikiwa na utangulizi na mwisho wa kumuenzi Reeves kwenye sinema za
Afrika Kusini baada ya kifo chake zikimsifia kama rafiki wa kweli wa nchi yao.
Britania na Ireland
Reeves alitalii Britania na Ireland mwaka 1963 akiwa na kikosi cha
Reeves na the Blue Boys, alitembelea pia ngome ya kijeshi ya Marekani iliyopo
Ireland kati ya Mei 30 hadi Juni 19, 1963. Onyesho lake lilihudhuriwa na umati
mkubwa wa watu wanaokisiwa kufikia 1,700. Hapa Jim hakupendezewa na piano licha
ya kuguswa na hadhira kubwa ya watu. Licha ya umati huo mkubwa, Jim aliamua
kufanya onyesho kwenye redio na televisheni. Alirekodi nyimbo zake tatu zikiwemo
za “I love You Because”, na I won’t Forget You”. Nyimbo hizi zinakisiwa kuuza
idadi kubwa ya kanda zipatazo 860,000 na 750,000 ziliuzwa mfululizo katika
Britania pekee. Aliruhusiwa kufanya onyesho Ireland na shirikisho la Muziki la
Ireland kwa makubaliano kuwa washirikiane gharama na bendi za maonyesho za Ireland.
Norway
Kazi za Reeves zilipambanishwa huko Norway
na kufanikiwa kushinda kwa kushika namba moja. Onyesho lake lilirekodiwa na
mitandao ya TV za Norway na kupigwa mfululizo kwa mwaka mzima na kufanywa
mwanamuziki maarufu katika historia ya Norway. Kazi zake zilizong'ara kwenye
matamasha jijini Oslo Norway Aprili 16, 1964 akiwa na kundi lake la Blue Boys
na The Anita Kerr Singers
ni "You're the Only Good Thing (That's Happened to Me)", "He 'll
Have to Go", "I Love You Because".
Rekodi zake za mwisho wa uhai wake
Reeves kuelekea mwisho wa uhai wake
alirekodi "Make the World
Go Away", "Missing You", na "Is It Really
Over?". Pale nafasi ilipobaki katika mfululizo huo wa kurekodi, Jim
alirekodi wimbo wake wa mwisho kabisa na kituo cha RCA uliojulikana kama "I Can't Stop Loving You". Zipo
nyimbo ambazo alirekodi kwenye studio yake ndogo ya nyumbani ambazo RCA
haikutaka kuzitoa sokoni kutokana na kwamba hazikuwa zimewekewa lebo ya
mmiliki.
Kifo
Mnamo Julai 31, 1964, Reeves na mfanyakazi
mwenzake ambaye ni meneja aliyeitwa Dean Manuel (ambaye pia alikuwa ni mpiga
piano wa kundi la akiba la Reeves, the Blue Boys) waliondoka Batesville, Arkansas, wakielekea
Nashville wakiwa ndani ya ndege ya injini moja aina ya Beechcraft Debonair, iliyokuwa ikirushwa na Reeves
mwenyewe kama rubani wake. Wawili hawa walipata fursa ya biashara ya mashamba
lakini pia Reeves alipata fursa nyingine ambayo haikutimia ya kununua nyumba toka
katika familia ya LaGrone huko Deadwood,
Texas, Kaskazini mwa alikozaliwa Galloway. Wakati wakiruka kwenye anga
ya Brentwood, Tennessee, walikumbana
na radi kali. Uchunguzi wa awali uligundua kuwa ndege hiyo ndogo ilinaswa
kwenye dhoruba na Reeves akapata kuchanganyikiwa kwa kiasi fulani. Mjane wa
Reeves, Mary Reeves aliyeishi kati ya 1929–1999, pengine kwa kutokujuwa alianza
kusambaza habari kuwa mumewe alikuwa akirusha ndege kichwa chini akidhani
alikuwa akipaa juu zaidi kukwepa dhoruba. Hata hivyo, kulingana na Larry Jordan, mwandishi wa wasifu (bio) wa
mwaka 2011, Jim Reeves: His Untold Story, tukio hili linakanushwa na
mashuhuda waliofahamika kwa wachunguzi wa ajali hiyo ambao waliona ndege ikiwa
juu usawa wa kichwa (overhead) mara kabla ya ajali, na wakathibitisha kuwa Reeves
hakuwa akiruka kichwa chini.
|
Kushoto ni ndege aliyokuwa akiendesha Reeves na kulia ni wachunguzi wakichunguza ajali yake ambaye ilisababishwa ba hali mbaya ya hewa. |
Jordan anaandika kwa mapana kuhusu
ushahidi wa uchunguzi wa ajali hii, ambayo inapendekeza kuwa badala ya Reeves
kuelekeza ndege upande wa kulia kukwepa dhoruba (kama alivyoelekezwa na
mwongoza radar wa ndege zinazotua), Reeves yeye alikunja kushoto akitaka
kujaribu kufuata barabara ya Franklin kuelekea uwanja wa ndege. Katika kufanya
hivyo akajikuta ameelekea kwenye mvua. Akiwa ametingwa na kujaribu
kurejea/kusoma mwongozo wake wa kutua, Reeves kwa kitendo hicho alisababisha
ndege kwenda spidi ndogo na kuifanya ikashindwa kuendelea kuruka katika spidi kubwa.
Akiwa amezama katika kujitegemeza kwenye ufahamu wake binafsi zaidi ya ujuzi
aliopata kwenye mafunzo ya urubani, ushahidi ulionyesha kuwa aliongeza nguvu
zote na akipambana na mvutano kabla ya kuweka sawia mbawa za ndege—kosa kubwa
baya lakini la kawaida lilisababisha ndege kuvingirika katika hali ambayo
kuiokoa ilikuwa nadra sana. Jordan anaandika kuwa kulingana na taarifa
iliyorekodiwa kwenye mnara wa kuongozea ndege, Reeves alijiingiza kwenye mvua
kubwa majira ya saa 10:51 alasiri na kupinduka dakika moja baadaye yapata saa 10:52
alasiri.
Wakati
kifusi cha ndege kilipogundulika masaa 42 baadaye, iligundulika kuwa injini ya
ndege na pua lake vilizama kabisa ardhini kutokana na ukubwa wa nguvu ya
muanguko wake toka juu. Sehemu ya ajali ilikuwa kwenye msitu wa Kaskazini
Kaskazini-Mashariki (north-northeast) ya Brentwood takriban njiapanda ya Baxter
Lane na Franklin Pike Circle, Mashariki ya Interstate 65, na Kusini Magharibi ya uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Nashville ambapo Reeves
alipanga kutua. Kama bahati vile wote, Reeves na Randy Hughes, rubani wa ndege
iliyopinduka ya Patsy Cline
walifunzwa
na mkufunzi mmoja. Asubuhi ya Agosti
2, 1964, baada ya msako mkubwa sana wa makundi mbalimbali ya uokozi (ambao
ulijumuisha marafiki mbalimbali binafsi wa Reeves wakiwemo Ernest Tubb na Marty Robbins) mabaki ya miili
ya muimbaji na Dean Manuel yalipatikana kwenye kifusi cha ndege na majira ya saa 7:00 adhuhuri kwa masaa ya
Marekani, vituo vya redio nchi nzima ya Marekani vilianza kurusha rasmi taarifa
za kifo cha Reeves. Maelfu ya watu walisafiri kwenda kutoa heshima za mwisho
kwenye msiba wake siku mbili baadaye. Jeneza, likiwa limepambwa kwa mauwa, toka
kwa wafuasi wake, liliendeshwa kwa kupitishwa kwenye mitaa ya Nashville na
baadaye kuelekea kwenye sehemu ya mapumziko ya mwisho ya Reeves karibu na Carthage,
Texas. Inataarifiwa kuwa mabaki ya mwili wa Reeves hayakuruhusiwa kuangaliwa
kwenye zoezi la kutoa heshima za mwisho.
Masalia
Jina lake lilipewa mtaa Jim Reeves Drive katika
jiji la Texas ambapo pana ukumbi
mkubwa wa miziki maarufu huko Carthage. Reeves alichaguliwa katika ukumbi huu baada ya kifo
chake kuwa mwanamuziki maarufu mwaka wa 1967, tuzo ambayo ilimpa heshima na
kutolewa tamko kuwa, “Staili ya velvet ya Gentleman Jim Reeves ilikuwa ya
ushawishi wa kimataifa”. Utajiri wa sauti yake (vocal) ilivuna mamilioni ya
wafuasi wa muziki toka pande mablimbali za dunia kupenda muziki wa Kimarekani. Ingawa
ajali ya ndege yake ilichukuwa uhai wake, ukoo utaendeleza jina lake kuwa hai
kwa sababu watamkumbuka kama mmoja wa wanamuziki maarufu. Maandishi ya kumbukumbu
kwenye kaburi lake yanasomeka hivi: “Kama mimi mwimbaji wa chini, nikifuta
chozi, au nikipooza moyo wa mtu mmoja mnyeyekevu inayogugumia maumivu, basi aya
yangu kwa MUNGU ni nzuri, na hata ubeti mmoja hautaimbwa kwa uchungu”
|
Kaburi lake |
Matoleo baada ya kifo
Rekodi za Reeves ziliendelea kuuzwa sana
zote za zamani na albamu za baada ya kufa, mjane wake Mary aliunganisha kazi
ambazo hazikuzinduliwa na zile zilizozinduliwa akiweka midundo/beats mpya
sambamba na sauti orijino za Reeves ili kuzalisha mfululizo mwingine wa albamu
mpya baada ya kifo cha mumewe. Pia aliendesha jumba la makumbusho ya Jim Reeves
huko Nashville kuanzia katikati ya mwaka 1970 hata 1996. Kwenye kumbukumbu ya
15 ya kifo cha Reeves, Mary alimwambia mwandishi wa jarida la muziki aliyemsaili
kuwa, "Jim Reeves mume wangu ameondoka; Jim Reeves msanii anaishi."
Mwaka 1966,
wimbo wa Reeves wa "Distant
Drums" ulishika nambari moja huko Britania katika single/singo
zilizoshindanishwa. Awali RCA ilidhani kuwa wimbo huo ni kwa ajili ya matumizi
ya kujifurahisha binafsi na kwamba haukufaa kutumika kwa ajili ya umma. Ndiposa
RCA ikagundua kuwa kulikuwa na soko kubwa la toleo hilo huko Vietnam kufuatia
vita iliyokuwa ikirindima huko Vietnam na Marekani ikaingia vitani kujaribu
kuzuia kutanuka kwa ukomunisti na Marekani kujikuta ikishindwa vibaya sana
maana haikuweza kupigana vita vya gorilla [vita vya msituni]. Nchini Uingereza
wimbo huu ulishindanishwa na kufanikiwa kushika nambari moja. Reeves akaja kuwa
Msanii wa Kimarekani kwa kwanza kushinda na wimbo huo ukapewa hadhi ya wimbo wa
mwaka wa Uingereza. Mwaka huo huo mwimbaji Del Reeves [hawana uhusiano wa
kidugu] akatengeneza albamu kwa heshima ya marehemu Jim Reeves.
India na Sri Lanka
Reeves alijipatia wafuasi wengi huko India
na Sri Lanka kuanzia miaka ya 1960s, na inadhaniwa ni pekee ndiyo mwimbaji wa lugha
ya kingereza ambaye ni maarufu nchini Sri Lanka. Matoleo yake ya Krismas
yameendelea kuwa maarufu na stoo za muziki zimeendelea kuuza CDs na kaseti
zake. Nyimbo zake mbili, "There's a Heartache Following Me" na
"Welcome to My World," zilipendwa na Mwalimu wa Kiroho wa Kihindi Meher Baba. Nyakati za misimu
ya Krismas matoleo yake ya "Jingle Bells", Silent Night" au
"Mary's Boy Child" yamekuwa yakitafutwa sana nchini Sri Lanka. Robert Svoboda, katika kazi yake
ya sanaa-andishi juu ya Aghora na the Aghori Vimalananda, ametaja kwamba Vimalananda anamdhania
Reeves kuwa ni gandharva,
katika utamaduni wa Kihindi, inamaanisha ni mwanamuziki wa Kimbingu,
ambaye
amezaliwa duniani. Svoboda alipiga wimbo wa Reeves wa "Take My Hand,
Precious Lord" wakati mwili wa Vimalananda ukichomwa moto kwa desturi za
masishi ya Kihindu.
Kifo cha Mary Reeves
Mnamo mwaka 1996, Mary Reeves alikuwa
akiishi na wanyama jamii ya paka wapatao 200 kwenye shamba lake chakavu.
Alihamishiwa kwenye kituo cha mapumziko wanakolelewa watu wazee na Terry Davis
akapewa mamlaka ya kisheria (power of attorney) ya kusimamia urithi. Mapema
mwanasheria huyu akaingia mapatano ya kuuza mali za mjane Mary ikiwemo haki ya
kuweka sokoni jina la Jim Reeves kwa thamani ya dola milioni 7. Vyote
vilinunuliwa na mwendesha uwanja wa maonyesho, Ed Gregory, na uuzaji huu
ukaingia dosari tangia hapo ambapo ndugu zake Reeves's waliweka pingamizi la
kisheria kuhusu uamuzi huo. Yeyote ambaye angeshinda haki hiyo ya mnada
angekuwa na fursa ya kutengeneza mamilioni ya dola na kuwa tajiri. Mtu
anatumaini mali hizo zitawekwa sokoni na kuendelea kupendwa na wapenzi wa
masalia ya kazi za Jim Reeves. Mary Reeves alipoteza kabisa tumaini la kuishi
kufuatia mzozo huo na ilipowadia mwaka 1999 aliaga dunia na kuacha mgogoro
mkubwa wa kimahakama kuhusu mirathi ya mali alizochuma na mumewe.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni