Jumamosi, 5 Aprili 2014

PICHA ZA IBADA YA KUUOMBEA MWILI WA ALIYEKUWA ASKOFU WA KANISA LA ANGLICAN DAYOSISI YA KATI GODFREY MDIMI MHOGOLO JANA

Ibada ya kuombea mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa la Anglican dayosisi ya kati huko Dodoma ilifanyika jana katika kanisa kuu la kanisa hilo, ibada hiyo ilihudhuliwa na wachungaji, maaskofu viongozi wa serikana na watu mbalimbali, mwili wa Askofu unatarajiwa kuzikwa leo katika eneo la kuzikia maaskofu lililoko katika kiwanja cha kanisa hilo mjini Dodoma.
 Jeneza likiwa na  mwili wa aliyekuwa Askofu wa kanisa la Anglican Dayosisi ya Dodoma Godfrey Mdimi Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita nchini Afrika ya Kusini alikopelekwa kwa matibabu likiwa ndani ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu wakati wa ibada maarumu.
Waumini na viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati wakilishusha Jeneza lilibeba mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo ulipofikishwa kwa mara ya kwanza tokea alipofariki nchini Afrika ya Kusini kanisani hapo kwa ajili ya kufanyiwa ibada ya maombezi.
Wachungaji na makasisi wa Kaanisa la Anglican Dayosisi ya Kati wakiwa wamejipanga nje ya kanisa la Roho mtakatifu mjini Dodoma kwa ajili ya kuupokea mwili aliyekuwa Askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo.
  Waumini wa kanisa la Anglican wakiwa kwenye mahema yaliyowekwa nje ya kanisa kuu la Roho Mtakatifu walipokuwa wakifuatilia ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo kanda ya Dodoma  aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu nchini Afrika ya Kusini.
 Wageni mbalimbali kutoka nje ya nchi wakiwa ndani ya kanisa la Roho Mtakatifu kwa ajili ya ibada maaumu ya kuuombea mwili liyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita alipokuwa kwenye matibabu Afrika ya Kusini.
 Ndani ya kanisa la Roho mtakatifu waumini wakifuatila ibada ya kuuombea mwili wa aliyekuwa askofu wa kanisa hilo Godfrey Mhogolo aliyefariki wiki iliyopita akiwa kwenye matibabu.
Baadhi ya Viongozi wa Serekali wakiwa kwenye ibada hiyo.
 Waumini wa kanisa hilo wakiwa ndani ya hema lilijengwa katika eneo la makaburi ya kuzikia viongozi wa kanisa la Anglican Dayosisi ya kati ambapo walikuwa wakiandaa sehemu ya kuuzikia mwili wa aliyekuwa Askofu wa Kanisa hilo Godfrey Mhogolo unaotarjiwa kuzikwa leo Jumamosi.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni