Jumatano, 2 Aprili 2014

BINTI AFUFUKA BAADA YA KUFANYIWA MAOMBI. ALIKUFA GHAFLA SHULENI

Ni jambo la ajabu masikioni na machoni mwa watu kusikia kuwa mtu aliyekufa aweza kufufuka tena lakini Biblia inasema, Pozeni wagonjwa, TAKASENI WENYE UKOMA, FUFUENI WAFU, TOENI PEPO MMPETA BURE TOENI BURE. Haya ni maneno ya Yesu anayowaambia wanafunzi wake. Andiko lile lile linaloagiza kutoa pepo ndilo linaloagiza kufufua wafu, kumbe wafu wanatakiwa wafufuliwe kwa kiasi kilekile ambacho pepo wanatolewa.

Sawasawa na neno lake, ndilo lililojiri katika kanisa la UfufuO NA Uzima, tawi la Mwanza linaloongozwa na Mch. Kiongozi Samson Gwajima baada ya binti aliyekufa ghafla akiwa shuleni kuletwa kanisani hapo
MAITI YA BINTI IKILETWA KANISANI
Buhongwa Mwanza na kufufuka baada ya maombezi.

Mungu amekuwa mwaminifu katika kutimiza neno lake maana wiki chache zilizopita aliletwa mtoto mdogo kanisani hapo na kufufuka mara baada ya maombezi. Pichani kulia ni watu waliombeba binti huyo baada ya kufa shuleni wakimleta kanisani na kushoto ni mahojiahano kati ya Mch. Samson na binti aliyefufuka.

Mungu kwetu ni Mungu wa kuokoa na njia za kutoka mautini zina yeye!!!

KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni