Jumanne, 1 Aprili 2014

MUNGU AMBARIKI KUTOKA KWENYE OMBA OMBA HADI KUMILIKI BIASHARA YAKE BAADA YA KUMTOLEA MUNGU


Msimulizi ni Mchungaji Peter Mitimingi wa VHM


Huyu dadani mlemavu wa miguu. ni moja ya wadada ambao wananibariki sana mimi binafsi na kuubariki moyo wa Mungu.

Nilikutananaye mara ya kwanza kwenye makutano ya mataa "traffic light" akiwa kwenye wheelchair yake akiomba msaada wanaosimamisha magari.

Alinisikia nikiongea radioni kwahabari ya kuchangia kupeleka injili vijijini akanipigia simu na kunielekeza kijiwe anachoombea pesa na akasema amejibana kwa muda mrefu ana anataka kuchangia huduma ya VHM vijijini nikachukue sadaka yake hapo barabarani.

 Tulipokwenda dada huyu alitoa Tsh 21,000 alizokusanya kwa muda mrefu. Tulimuombea Baraka baada ya hapo akasema watu walianza kumpa pesa sio tu vicoin alianza kurushiwa elfu 1, elfu, 2, elfu 5 hadi elfu kumi.

Baada ya muda dada huyo aliniita tena kwenda kuchukua sadaka yake na safari hii dada huyo alitoa elfu 50. Tukamuombea tena baada ya muda alileta doti 6 za vitenge vya wax Piece tatu tatu kwajili ya wake za wachungaji vijijini. 

Tukamuombea tena. Baada ya muda akaleta Mashuka ya 6x6 na foronya zake kwajili ya wachungaji wa vijijini tukamuombea tena. Juzi jumamosi miaka miwili baadaye nikashangaa kumuona nje ya ukumbi wa Msimbazi center nilipokuwa nimealikwa kufundisha wanandoa akiwa sio omba omba tena wa barabarani bali akiwa anamiliki biashara yake hiyo ya vitu mbalimbali kama anavyonikana katika picha.

                                                CHANGAMOTO:

kuna watu wana miguu, mikono viungo vyote, wana kazi nzuri au biashara nzuri lakini kwa swala la kumtolea Mungu wamekuwa mbinde sana na visingizio na sabubu nyingi sana SIJUI UTAJIBU NINI KWA MUNGU SIKU HIYO AKIMSIMAMISHA DADA HUYU NA WEWE KUTOA HESABU YA ULICHOFANYA DUNIANI KWAJILI YA MUNGU
tafakari.


KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com
Chapisha Maoni