Jumatano, 2 Aprili 2014

KANISA LA TAG MAGOMENI YAANDAA IBADA MAALUM YA KIHISTORIA KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 75 YA TAG


 





Kanisa la TAG Magomeni katika kuhimiza miaka 75 ya TAG limeandaa ibada ya kihistoria ambayo itafanyika tar 06/04/2014. Ibada hiyo itaanza saa 08:00 asubuhi na kuendelea, ibada hiyo itajumuisha washirika wote wa zamani ambao wamekwisha hama na kama walikuwa waimbaji basi wataimba kwenye siku hiyo. Kwaya zote za zamani, Harvest, Mageni, Revival, Christ Boyz zitaimba. Ikiwepo praise team ya watu zaidi ya 50. Katika ibada hiyo mhubiri atakuwa Mch N.Sasali ambaye ndiye mwanzilishi wa kanisa hilo. Kanisa la TAG Magomeni lilianza mwaka 1978 chini ya Mch N Sasali ambye amekuwapo katika kanisa hilo mpaka mwaka 2007 na baada ya hapo kanisa hilo lilikuwa likiongozwa na Mch D Kanemba mpaka sasa. Wiki hii yote watu wengi wa zamani wamekuwa wakifika kwaajili ya maandalizi mbalimbali, na baada ya ibada hiyo kutakuwa na chakula kwa washirika wote watakao hudhulia siku hivyo.


MCH N. SASALI MWANZILISHI WA KANISA LA MAGOMENI TAG
MCH D. KANEMBA ANAYEONGOZA KANISA KWA SASA.

 
KAMA UNA MAONI YOYOTE NIANDIKIE HAPO CHINI AU TUMA UJUMBE KWENYE NO +255 715 033 671, +255 767 033 671 AU FB Martin Malecela follow me in Twetter martmalecela au tembelea page yetu na ulike martmalecela.blogspot.com

Hakuna maoni: